TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,720
- 10,220
Kutana na unju bin unuq.👇🏾
Unaambiwa huyu jamaa unju bin unuq alikua ni mkazi wa pwani. Huyu unju alikua na nambo ya ajabu, moja ya mambo ya ajabu ya mtu huyu ni urefu wake, inasadikika unju alikua na urefu mkubwa ulioweza kumfanya atembee baharini na miguu yake kugusa chini.
Pia alikuwa akitembea kutoka nchi hadi nchi kutokana na urefu wake. Inasimuliwa kuwa mmoja kati ya nyayo zake unapatikana kwenye jiwe alilokanyaga huko Tabora, Tanzania, wayo wa mguu wa kushoto wakati wayo wa mguu wa kulia ulionekana kwenye jiwe alilokanyaga huko Kongo.
Inasimuliwa pia akitaka kula alikuwa akichukua samaki baharini kwa mkono na kuchoma katika jua kisha anakula. Kuhusu maisha yake inasimuliwa kuwa Unju bin Unuk hakuoa wala kuolewa kutokana na umbo lake.
Sehemu nyingine ya hadithi yake ni alipokufa Unju , aligawanyika vipandevipande kutokana na urefu wake na inasemekana kidole chake chenye urefu wa kilometa moja kasoro ndicho kilichopatikana na kuzikwa pale Bagamoyo, lakini hakuna simulizi mwili wake uliobaki uliangukia wapi.
Unju bin Unuq alikuwa na ndugu yake aliyejulikana kama Geofrey bin Unuk, huyu alipatikana maeneo ya Dodoma. Au kwamba Unuq baada ya kupotea kwa muda wa miaka mingi ndugu zake wa mbali sana wameonekana katika mkoa wa Dodoma.
Hii ni story ya kweli kama wewe ni mtu lazima utakua ushakutana na hii story, au kama ushawahi kwenda makumbusho ya bagamoyo basi utakua ushakutana na hii story.