Grand Master Dulla
JF-Expert Member
- Jul 20, 2012
- 411
- 146
Kwa wale wakazi wa kilwa na maeneo ya karibu yake nadhani mtakuwa mnalijua au mmeshakulisikia jina hili la Enji Bin Nuuti inasemekana kwamba jamaa alikuwa ni mtu wa kale sana aliyetokea kaskazini na sifa yake kubwa ni kwamba alikuwa ni mrefu sana,inasemekana kwamba jamaa aliletwa ili apime kina cha bahari ya mwambao wote wa pwani yetu mbaka arabuni basi hata maji yawe na kina kiasi gani yalikuwa yanamfikia magotini tu.!!
Inasemekana kuwa huyu jamaa alikuwa anakwenda baharini anakamata samaki anayemtaka halafu ananyoosha mkono juu hafu samaki anakauka kwa jua mara moja ndio anamla.Wapemndwa tusishangae sana mana kizazi hiki itakuwa kilikuwepo tu duniani si mnakumbuka kwa wale wasomaji wa biblia kuwa kulikuwa na kizazi cha majitu kilichotokana kati ya bin adam na malaika? Au kwa waliosoma kitabu cha Enoki anawaelezea hawa watu ni wa namna gani vizuri zaidi !!!
Iinavyoonekana huyu bwana alikuwa wa mwisho wa kizazi chake cha majitu.Kisa kingine ni kwamba jamaa aliletwa kupima kina cha bahari na hawa wageni labda waarabu au waajemi na alipofika pwani ya kilwa inasemekana kuna sehemu alikuta kina kirefu sana maji yalimfikia kiunoni akaweka alama hadi leo nasikia alama alizoweka zipo.
Hadithi hii mimi nilihadithiwa na babu yangu aliyekuwa na umri wa miaka yapata 107 sasa ni marehem (rip) na alinihakikishia kuwa stori hii ni kweli na akaniambia kuwa hapo kilwa hadi leo kaburi lake lipo!!! ila alisema lipo pembezoni karibu na bahari.
Na yeye history hii alihadithiwa na mzee wake.hivyo basi wana JF tunawaomba kama kuna mtu alishawahi kusikia habari yeyote kuhusu sahaba huyu naomba atujuze maana hili ni jambo la kihistoria kwetu na nchi yetu kwa ujumla na ni utalii tosha.