Ni muda muafaka wa ku-excercise ''open marriages''..?

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,272
1,035
Haya haya wana MMU.....!

Teamo anaona ni busara zaidi kama tutaelezana facts kuhusu ndoa na mahusiano ya kizazi hichi...(kizazi cha nyoka,kudadadeki)...!

-uchakachuaji umezidi sana tu TENA SANA
-imefikia mahala sasa hizi ndoa za ''mume mmoja na mke mmoja'' zinaonekana kufail kabisa kabisa
-imefikia mahala sasa inadhihirika wazi kwamba theory ya ''mume mmoja na mke mmoja'' ni kama imepitwa na muda,HIWEZEKANI TENA
-Vyanzo vyetu vya uchunguzi vimetanabaisha wazi kwamba ile dhana ya ''uvumilivu'' kwenye hizi old skul marriages inachangia sana hizi ndoa kuonekana za kawaida sana na za kutimiza wajibu.
-Inaonekana wazi kabisa mahusiano mengi ya 'mume mmoja na mke mmoja'' sio ya kweli.BEHIND THE SCENE kuna vitu vingi sana vinaendelea kwa jinsia zote mbili(hapa tusihojiane sana wakuu,mnajua)

sasa teamo anajiuliza kwanin tusihalalishe na kueksasaiz OPEN MARRIAGES?labda tuielezee open marriage kwa kingereza hapa:

Open marriage typically refers to a marriage in which the partners agree that each may engage in extramarital sexual relationships, without this being regarded as infidelity.

according to teamo na research yake ya ujanja ujanja ni kwamba kuna ndoa kumi za watu maarufu kabisa duniani ambazo ni ''OPEN MARRIAGES'' zinamafanikio makubwa sana.Kwa leo nitaanza na ndoa ya Will Smith na Jadda pinkett ambayo kwa sasa ina miaka 11

NI MUDA MUAFAKA WA KU-EXCERCISE ''OPEN MARRIAGES''..?
 
sio muda muhafaka na wala haitafika kuwa ivyo, kutokana na tamaduni zetu.

wanandoa wengi wanatoka nje ya ndoa zao pasipo mwenzake kufahamu anatoka muda gani
 
sasa ili kulikabili hili swala...

kwanin tusiipractice OPEN MARRIAGE?...

mi nadhani itakuwa safe zaidi,maanake lazima tutawekkeana principles
 
Mkuu open marriage kwa mazingira yetu haya ya kiafrika it doesn't work kama unataka watu watoane roho hivi unafikiri nani anayeweza kuvumilia a open marriage ni bora usijue kuwa mamsapu wako anamegwa kuliko kujua anamegwa halfu bado manaendelea kuishi wote nyumba moja, Teamo honestly speaking hii kitu inahitaji moyo na guts mpaka mmefikia makubaliano ya kuwa na open marriage sidhani kama kuna haja ya kuendelea kuishi pamoja mazingira yetu huku yako tofauti sana.
 
Mkuu open marriage kwa mazingira yetu haya ya kiafrika it does work kama unataka watu watoane roho hivi unafikiri nani anayeweza kuvumilia a open marriage ni bora usijue kuwa mamsapu wako anamegwa kuliko kujua anamegwa halfu bado manaendelea kuishi wote nyumba moja, Teamo honestly speaking hii kitu inahitaji moyo na guts mpaka mmefikia makubaliano ya kuwa na open marriage sidhani kama kuna haja ya kuendelea kuishi pamoja mazingira yetu huku yako tofauti sana.

Sasa mkuu hii biashara ya MAZINGIRA,na WIVU mi nadhani ni kitu ambacho tunaweza kujitune na kukizoea tu
unajua kwa namna tunavyoishi ni sahihi zaidi kama tutakuwa ''formal'',na kajisystem fulani hivi i mean
 
Naiteua ndoa ya mufalme ya amani iwe pilot open marriage project....ikifanikiwa nitarithisha hili wazo kwa wanangu.....
 
wee bana hebu nambie je,hudhani kwamba ni muda muafaka wa kuwa na open marriages?usipindishe mada bana we
 
Anza na wewe kwanza wengine ndo tufate uje utupatie matokeo. Halafu acha kudanganya wewe unakwenda kula chakula cha mchana na usiku na familia halafu unatuambia sie tuwe nda ndoa za open wapi na wapi bana
 
Sio muda muafaka....acha tuinjoi infidelite kidogo...japo kwa miaka 100 ijayo....
 
Anza na wewe kwanza wengine ndo tufate uje utupatie matokeo. Halafu acha kudanganya wewe unakwenda kula chakula cha mchana na usiku na familia halafu unatuambia sie tuwe nda ndoa za open wapi na wapi bana

ahahahahaha!
wakuu nimeuliza swali tu wakuu

sijaweka commands
 
Sasa mkuu hii biashara ya MAZINGIRA,na WIVU mi nadhani ni kitu ambacho tunaweza kujitune na kukizoea tu
unajua kwa namna tunavyoishi ni sahihi zaidi kama tutakuwa ''formal'',na kajisystem fulani hivi i mean
Teamo ki ukweli kabisa aslimia kubwa ya mapenzi yanaongozwa au yanachochewa na WIVU sasa sidhani kama mtu yuko radhi kuona MKE/MUME anamega/kumegwa huku yeye akiwa anajua ni bora usijue tu, vile vile kiini cha nyie wawili kukubaliana hadi kuwa na OPEN MARRIAGE ni nini haswa je kuna vitu ambavyo mmeshindwa kutimiziana basi labda kwa kuwa na OPEN MARRIAGE kila mtu atapata kile anachohitaji?

Kwa wenzetu inafanya kazi kutokana na malezi waliyonayo tokea mwanzoni wenzetu wanaanza relationship wakiwa na 15 years na ni mambo mengi wanayojifunza sisi huku wengine your first GF/BF unaweza kumpata labda ulikuwa una miaka 20 au 23 kwahiyo ni mambo mengi hatufundishwi tukiwa wadogo tunafundishwa tukiwa wakubwa kwahiyo unakuta vitu vingine its hard to swallow
 
Haya haya wana MMU.....!

Teamo anaona ni busara zaidi kama tutaelezana facts kuhusu ndoa na mahusiano ya kizazi hichi...(kizazi cha nyoka,kudadadeki)...!

-uchakachuaji umezidi sana tu TENA SANA
-imefikia mahala sasa hizi ndoa za ''mume mmoja na mke mmoja'' zinaonekana kufail kabisa kabisa
-imefikia mahala sasa inadhihirika wazi kwamba theory ya ''mume mmoja na mke mmoja'' ni kama imepitwa na muda,HIWEZEKANI TENA
-Vyanzo vyetu vya uchunguzi vimetanabaisha wazi kwamba ile dhana ya ''uvumilivu'' kwenye hizi old skul marriages inachangia sana hizi ndoa kuonekana za kawaida sana na za kutimiza wajibu.
-Inaonekana wazi kabisa mahusiano mengi ya 'mume mmoja na mke mmoja'' sio ya kweli.BEHIND THE SCENE kuna vitu vingi sana vinaendelea kwa jinsia zote mbili(hapa tusihojiane sana wakuu,mnajua)

sasa teamo anajiuliza kwanin tusihalalishe na kueksasaiz OPEN MARRIAGES?labda tuielezee open marriage kwa kingereza hapa:

Open marriage typically refers to a marriage in which the partners agree that each may engage in extramarital sexual relationships, without this being regarded as infidelity.

according to teamo na research yake ya ujanja ujanja ni kwamba kuna ndoa kumi za watu maarufu kabisa duniani ambazo ni ''OPEN MARRIAGES'' zinamafanikio makubwa sana.Kwa leo nitaanza na ndoa ya Will Smith na Jadda pinkett ambayo kwa sasa ina miaka 11

NI MUDA MUAFAKA WA KU-EXCERCISE ''OPEN MARRIAGES''..?
Open marriage=Tamaa tupu.
 
Teamo ki ukweli kabisa aslimia kubwa ya mapenzi yanaongozwa au yanachochewa na WIVU sasa sidhani kama mtu yuko radhi kuona MKE/MUME anamega/kumegwa huku yeye akiwa anajua ni bora usijue tu, vile vile kiini cha nyie wawili kukubaliana hadi kuwa na OPEN MARRIAGE ni nini haswa je kuna vitu ambavyo mmeshindwa kutimiziana basi labda kwa kuwa na OPEN MARRIAGE kila mtu atapata kile anachohitaji?

Kwa wenzetu inafanya kazi kutokana na malezi waliyonayo tokea mwanzoni wenzetu wanaanza relationship wakiwa na 15 years na ni mambo mengi wanayojifunza sisi huku wengine your first GF/BF unaweza kumpata labda ulikuwa una miaka 20 au 23 kwahiyo ni mambo mengi hatufundishwi tukiwa wadogo tunafundishwa tukiwa wakubwa kwahiyo unakuta vitu vingine its hard to swallow

kwa hiyo mpwa wangu finest unataka nambia uzao wetu huu wakianza mahusiano at their 15s wataimudu open marriage?

kwa hiyo mpwa wangu finest unataka niambia kwamba kwakuwa tunaanza mapenzi at our 20s ndio sababu pekee ya kuishindwa open marriage?

kwa hiyo mpwa wangu finest unataka nambia kwamba kati kati ya miaka 15 na 22 kunakuwa na mafunzo ya kuzikabili open marriages kwa wenzetu first world countries?
 
Teamo mbona mada nzuri sana hii ila watu wanaingia mitini kuchangia wanaogopa nini l.o.l
 
sasa ili kulikabili hili swala...

kwanin tusiipractice OPEN MARRIAGE?...

mi nadhani itakuwa safe zaidi,maanake lazima tutawekkeana principles

Teamo ni bora hizo principles zisiwepo, mapenzi yanajengwa na wivu na kama mtu hana wivu hakuna mapenzi
 
Mie nadhani ni muda muafaka kila mtu awe mkweli kwa mwenzi wake. KAma wanataka hio type ya ndoa wakubaliane wenyewe, wala wasihusishe chombo chochote kutaka kueleweka nacho.
Tatizo ni pale mmojawapo wa wanandoa anapotaka YEYE ndio awe open ana aendelee kupata benefit kama za closed.
Ndoa ni give and take, ni mkataba, ni hiari, mkataba unatakiwa uwe wazi na wa kueleweka. ijulikane yanayoufunga huo mkataba, na yanayoufungua.
ndoa ni mkataba kati ya watu wawili.
hakuna haja ya public kuujua wa la kuuingilia.

Mie siutaki, wala watoto wangu wa kike na wa kiume singependa wauingie siku moja unless wamelazimika.
Baadhi ya watu unaongea nao hapa wanapractice closed marriages, ila kuna kuteleza hapa na pale.
 
kwa hiyo mpwa wangu finest unataka nambia uzao wetu huu wakianza mahusiano at their 15s wataimudu open marriage?

kwa hiyo mpwa wangu finest unataka niambia kwamba kwakuwa tunaanza mapenzi at our 20s ndio sababu pekee ya kuishindwa open marriage?

kwa hiyo mpwa wangu finest unataka nambia kwamba kati kati ya miaka 15 na 22 kunakuwa na mafunzo ya kuzikabili open marriages kwa wenzetu first world countries?
Kwenye BLUU sio necessary 15 lakini kuna kitu tunachoita msingi wenzetu inawezekana walianza karne mbili au tatu nyuma yetu sisi amabao tunaoanza leo inakuwa ngumu sana pia ni wazazi wachache sana wanaokaa na watoto wao wakaanza kuongea nao masuala ya mahusiano wengi wao wanawaonea aibu watoto zao hicho nacho ni chanzo unakuta mzee anaongea na mwanae mambo ya mahusiano wakati mwanawe ameishafika chuo

Kwenye RED kuanza mapenzi at our 20's sio sababu ya kushindwa kuwa na OPEN MARRIAGE lakini je ni wangapi leo hii wanajua nini maana ya OPEN MARRIAGE kama ukiuliza watu ni wachache sana pia ukumbuke hiki kitu kwetu ni kigeni sana.

Kwenye NYEUSI inawezakana hakuna lakini malezi na mazingira wanayoishi kwa namna moja ua nyingine yanaweza kusababisha wakaona OPEN MARRIAGE kama kitu cha kawaida kama wanaweza wakafanya three some huyu akalala na BF wa mwenzake na huyu akalala na GF wa mwenzake sidhani kama OPEN MARRIAGE itawashinda, sasa kwetu haya ni mambo ambayo kuya-adapt ndipo hapo mtu unaanza kuambiwa TUMELAANIWA.
 
Back
Top Bottom