Ni marufuku kuimba wimbo wa Taifa bila kibali maalumu cha Wizara ya Mambo ya Ndani

UZALENDO== 000
Aliyetoa waraka huo ATUMBULIWE.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Wizara ya Mambo ya Ndani imepiga marufuku kutumia wimbo wa taifa isivyo sahihi. Katika tangazo hilo lililosambaa mitandaoni serikali imepiga marufuku kuimba wimbo wa taifa mahali popote pale bila kibali isipokuwa kwenye dhifa au shughuli za kitaifa.

Katika hatua nyingine serikali imekataza matumizi ya neno njano kwenye bendera ya taifa. Kwa mujibu wa serikali bendera ya taifa ina rangi nne ambazo ni
BLUE
NYEUSI
DHAHABU na
KIJANI
Hii ni tofauti na inavyofahamika na wengi ambao huitaja rangi ya njano kama mojawapo ya rangi za bendera ya taifa badala ya rangi ya dhahabu inayotambuliwa katika sheria mbalimbali.

View attachment 965324View attachment 965325View attachment 965326View attachment 965327
 
Kwenye civics imeandikwa Yellow siyo Golden sasa inawekazana tumepata maono mapya yatakayosababisha tupate dhahabu nyingi
The flag of Tanzaniaconsists of a yellow-edged black diagonal band, divided diagonally from the lower hoist-side corner, with a green upper triangle and blue lower triangle. Adopted in 1964 to replace the individual flags of Tanganyikaand Zanzibar, it has been the flag of the United Republic of Tanzania since the two states merged that year. The design of the present flag incorporates the elements from the two former flags.

Tanzania

Use
 
Hivi kuna rangi ya dhahabu eeenheeee,,,,,anywayz miaka naenda rudi tulifundishwa na tunafundisha kwamba moja ya rangi ya bendera ya Taifa ni njano.

Leo hii tubadili pasipo kubadili iyo rangi,, kitukoooooo!!!
 
SHULE ZA MSINGI WANAIMBA KILA SIKU ASUBUHI.HII INAWAJENGEA URAIA. WATAFURAHI SANA KUTOIMBA. HILI NI SAWA?NCHI ZOTE DUNIANI WIMBO WA TAIFA WATOTO WANAIMBISHWA ILI KUJENGA UZALENDO SASA ITAKUWAJE? SHULE ZIKAOMBE KUTUMIA HUU WIMBO? NANI HAPA ANAYETUPOTEZA?
 
Kumbe toka shule ya Msingi ile Njano ilikuwa ni Uongoo???Alafu dhahabu ni nyekundu eeh...Mawaziri vilaza kama hawa ni mzigo tu kwa serikali...Fukuzaaa
 
Wimbo wa Taifa ni dua kwa Mungu ya kuliombea bara letu, nchi yetu na viongozi wake. Kwa wakristo tuna sala maalum Sala ya Bwana binafsi nauona wimbo wa taifa kama sala maalum pia sasa ndio wanataka tuombe kibali ili kuitumia sala hii kuzungumza na Mungu wetu? Anyway tutafika tu.

Ila kuhusu bendera binafsi naona rangi inayozungumziwa inashabihiana zaidi na njano kuliko dhahabu, na kwa tafsiri ya hizo rangi njano inawakilisha madini naona ilikuwa imekaa poa sana tu.

Kitu ambacho nadhani wangekiangalia ni ka- ubaguzi ktk rangi za bendera hasa rangi nyeusi, kama nitakua sijakosea naamini tafsiri yake ni hii:-

Bluu: inawakilisha "water bodies" i.e. bahari etc
Njano/dhahabu: inawakilisha madini
Kijani: maliasili
Nyeusi: rangi ya wananchi

Sasa kitu cha kujiuliza, je taifa letu lina watu weusi tu, albino, wahindi, waarabu, wazungu na watu wengine wasio na rangi nyeusi ambao ni raia wa Tanzania na wana haki zote kama raia kwa nini wamebaguliwa ktk utambulisho huu?

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom