Ni marufuku kuimba wimbo wa Taifa bila kibali maalumu cha Wizara ya Mambo ya Ndani

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Wizara ya Mambo ya Ndani imepiga marufuku kutumia wimbo wa taifa isivyo sahihi. Katika tangazo hilo lililosambaa mitandaoni serikali imepiga marufuku kuimba wimbo wa taifa mahali popote pale bila kibali isipokuwa kwenye dhifa au shughuli za kitaifa.

Katika hatua nyingine serikali imekataza matumizi ya neno njano kwenye bendera ya taifa. Kwa mujibu wa serikali bendera ya taifa ina rangi nne ambazo ni
BLUE
NYEUSI
DHAHABU na
KIJANI
Hii ni tofauti na inavyofahamika na wengi ambao huitaja rangi ya njano kama mojawapo ya rangi za bendera ya taifa badala ya rangi ya dhahabu inayotambuliwa katika sheria mbalimbali.

FB_IMG_1544563138819.jpeg
Screenshot_2018-12-12-00-34-16.jpeg
Screenshot_2018-12-12-00-34-00.jpeg
IMG-20181211-WA0104.jpeg
 
Back
Top Bottom