Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
Wakuu mambo ya Tanzania, sio kama huko majuu sio lazima iwepo any standing policy ili kuwanyima wananchi kutosoma JF, binafsi ninajua for a fact kuwa hiyo kitu ipo, hairuhusiwi kusoma JF katika ofisi za serikali bongo hakuna mtu anahitaji a standing law on that,
Majuzi nilikuwa ninaongea na mbongo mmoja akaniambia kuwa nimewasikieni huko kwenye mtandao, nasikia mna maneno sana lakini hamuelewi vizuri matatizo yetu wananchi, njaa tuliyonayo akitokea mtu anagombea ubunge akanipa kilo tano za mchele nitampa kura yangu tena bila wasi wasi hata kama simjui, nasikia huko kwenu ni dhambi kubwa sana,
akasema bosi wangu akisema saini hii karatasi mimi ni kusaini tu bila kuuliza, lakini nasikia huko kwenu mnasema hamtasaini, akasema Mungu awajalie sana msije fanya kazi kwenye serikali maana hamtaamini yanayofanyika na sisi wananchi tumeridhika saafi! Maana nikisha sain karatasi ya bosi ambayo sijui ni ya nini the mext thing ninapewa trip ya kwenda Europe kuhudhuria mkutano, ninakula perdiem na kule pia ninamnunulia bosi wangu zawadi nzuri sana, na sometimes mimi mwenyewe kabla ya kuondoka ninamuuliza bosi wangu kama anahitaji spare ya gari lake, aksiema ndio mimi ni kumnunulia tu, akasema nyie endeleeni na maneno yenu huko mtandaoni!
Jamani tuweni wakweli hata kama tunataka kuelezea jambo muhimu.
Kama mtu atahongwa kilo 5 kwa ajili ya kura, sidhani kama atakuwa anahitajika kusaini makaratasi ya bosi na kupigwa kitripu chenye padiemu ulaya.
Kama ni stori basi iwe ni stori, kama ni fakti, jamani naomba zibaki kama faktis.