Ni marufuku kufungua mtandao wa JF ukiwa katika ofisi za Serikali

Wapuuzi tu hawa magamba na serikali yao ya kifisadi, mimi naingi humu na kisimu changu cha mchina hata nikiwa kijijini. Siku zote mfa maji haachi kutapatapa.
 
Soma hii habari then piga picha na habari ya Mugisha tuone kama panaweza kuwa na ukweli .Maofisa habari waonywa kwa kuuza siri za serikaliVeronica MhetaDaily News; Saturday,June 21, 2008 @00:01Serikali imesema kuwa baadhi ya maofisa habari wamekuwa wakivujisha siri za serikali kwa kuziuza kwenye magazeti wapate fedha kama mgawo kwa kufanikisha uuzwaji wa siri hizo, na kwamba sasa itachukua hatua za kisheria kukomesha hali hiyo. Inadaiwa kuwa maofisa habari wengine huwapigia simu wahusika wa magazeti na kuwapatia siri hizo wazichapishe magazetini. Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Kassim Mpenda, wakati akitoa maazimio ya mkutano uliofanyika mjini Morogoro hivi karibuni mbele ya maofisa habari kutoka wizara zote za serikali. Mpenda alisema kutokana na udhaifu wa maofisa hao, magazeti yamekuwa yakinunua siri za serikali na kuzichapisha kutokana na uuzaji wa siri hizo unaofanywa na maofisa hao. Alisema ofisa habari yeyote atakayebainika kuuza au kutoa siri za serikali ili ziandikwe magazetini atachukuliwa hatua kali za kisheria. "Jamani tushirikiane kuhakikisha siri za serikali hazitoki nje au kwenye magazeti hivyo tuhakikishe tunazilinda siri hizo. Si vyema kuandikwa magazetini na kama kuna ofisa atabainika kuuza siri hizo atachukuliwa hatua kali za sheria," alisema Mpenda. Alisema baadhi ya mapendekezo yaliyopendekezwa na maofisa habari ni kuimarisha Idara ya Habari (MAELEZO) ili iratibu shughuli za vitengo vya Habari, Elimu na Mawasiliano ili kufanikisha utoaji taarifa za serikali kwa umma. Aliwataka maofisa habari kuhakikisha wanaandaa taarifa za mipango watakayoifanya kwa mwaka mzima kurahisisha kutoa habari zinazohusu maendeleo ya kila wizara husika. Aliiomba serikali iangalie jinsi ya kushughulikia vyombo vya habari binafsi vinavyoipinga serikali kwa kupotosha umma na alizitaka wizara zitumie vyombo vya habari vya serikali kutoa taarifa zake kwa umma.
Kwa hiyo ikivuja habari itakayo pelekea kukosoa serikali kwa kufuchua uovu wao, hiyo inageuka siri na ndio tatizo, mbona hawalalamiki ikiwa habari hizo zitasifia serikali??Maafisa habari endeleeni kutoa hizo habari msikubali kuzibwa midomo kama mtaona kwa kutoa habari hizo mtafichua uovu.
 
Mnyetishaji amenipa habari hizi anasema kuna waraka na uamuzi umeptishwa kwa wakuu wote wa Idara Serikalini na mashirika ya Umma kwamba ukikamatwa uko kwenye mtandao wa JF ukiwa ofisini basi na kazi huna .Nina omba mwenye nyeti zaidi aje atupe ukweli zaidi na sababu ya Serikali kuogopa mtandao huu usitembelewe ila unaweza kutembelea hata mitandao ya ngono ila si JF .
Kama ni kweli hatua hii ya CCM na serikali naifananinisha na baadhi ya wtu kabila fulani(....)Ambao wanatabia kwenda haja kubwa mbugani,vichochoroni kwa kifupi adharani wanapofanya tendo hilo ufumba macho wa kidhani kwa kufanya hivyo hawaonekani!.
 
Ndivyo tulivyo anayekataza wenzie wasisome jf yeye ndiye wa kwanza kuzamia jf hataki wenzie wafaidi ni wivu wa kike haufai kwenye jamii ya wanaoitakia mema nchi yetu,lakini wanawezaa?????inabidi wanunue marobot yatakayo simama mbele ya kila mfanyakazi kuangalia kama ameingia kenye jf yamripotie au wanunue cctv nyingiiii daaaa!!!!!na simu za mkononi je??????JK ama kweli kazi unayo,dawa wala sio hiyo ila ni kuwa na uadilifu ,fuateni maadili ya kazi,kila mtu akiamua kuiba nchi hii vijana wetu watakuwa wageni wa nani kwenye hizi jumuiya zinazoibuka??????na wageni wakijua tunaiba wao si ndio watafilisi????.
 
Si Serikalini tu, hata maofisi ya binafsi. Khee, Mnanshangaza. Mnaenda kufanya kazi huko au kuingia mitandao isiyohusiana na shughuli zenu.
 
Ni social networks zote haziruhusiwi kwenye maofisi, wafanyakazi wanalipwa kwa ajili ya kufanyakazi na si kuchat, watu wanatakiwa kuheshimu sheria na kanuni za maofisi wanayofanyia kazi.

Wakati mwingine hata kutumia yahoo, hotmail au gmail pia haziruhusiwi.
 
Once upon a time ilikuwapo JAMBOFORUMS, wakamtumia Said Mwema na kuupachika kuwa ni Mtandao wa KIGAIDI, wakawatia msukosuko baadhi ya vijana wazalendo wakakosa sababu za msingi za kuwashitaki wakaishia kuwaachia, baadae Jamboforums ikavuliwa gamba na kuwa Jamii forums japo sumu na genes ni zilezile tena sumu ikawa kali sana kama Nape anavyosema nyoka akijivua gamba ndiyo sumu inaongezeka kuwa kali.

JF si tu inawaamsha watawala ila pia inawasaidia sana katika kujua na kufahamu mawazo ya watanzania mbali positive and negative. JF ni mimi wewe, JK, na mawaziri na kila aina ya Mtanzania. Anayekuja na policy ya kipuuzi ni dhahiri anataka kulala fofo na huyo hatakiwi kuwa kiongozi. Ni kweli kabisa kuwa ili kuhakikisha ufanisi ni dhahiri inatakiwa watu watumie muda mwingi wa ofisini katika kutekeleza majukumu yao, Ila unapo target mtandao mmoja kati ya alfu moja kama sababu basi ni dhahiri sababu hizo ulizotoa si za kweli.

Serikali hii ambayo ina mitandao ambayo haiwi updated miaka miwili mitatu minne, ni dhahiri hata huduma ya mitandao kwenye ofisi nyingi za serikali haipo. Kama hii habari ni ya kweli suluhisho si kuangalia effect bali ni kuangalia cause ya kwa nini watu wanaichukia serikali?. Fanyia kazi mambo hayo watu watarudisha imani kwako. Acha uonevu bungeni, mahakamani, polisi, mahospitalini, ofisi za umma, acha kulinda walanguzi wa nchi waliojivisha ngozi ya uanasiasa na uongozi. Haki ni msingi wa maendeleo na amani. Huwezi kujipaka kinyesi halafu ukaanza kushutumu na kuchukia watu kuwa wanaziba pua zao pale unapowakaribia.
 
Kama ni kweli basi wafunge na kwenye simu na internet cafe zote mijini
 
ati kama walivyotumia mbinu ya kupandisha kodi ya mafuta ya taa kudhibiti uchakachuaji, vivyo hivyo mgao wa umeme una lengo la kupunguza muda wa wafanyakazi kusoma jf.
Wanaakili kama za mtu aliyeuza baskeli kununua pampu ya kujazia tairi upepo ya baiskeli aliyoiuza.
 
Hakun kitu kama hicho hata wanaopiga marufuku pia wana account,wengi tu hata usalama wana acc hii ni hiari ya mtu ..wajanja wote wana acc
 
Once upon a time ilikuwapo JAMBOFORUMS, wakamtumia Said Mwema na kuupachika kuwa ni Mtandao wa KIGAIDI, wakawatia msukosuko baadhi ya vijana wazalendo wakakosa sababu za msingi za kuwashitaki wakaishia kuwaachia, baadae Jamboforums ikavuliwa gamba na kuwa Jamii forums japo sumu na genes ni zilezile tena sumu ikawa kali sana kama Nape anavyosema nyoka akijivua gamba ndiyo sumu inaongezeka kuwa kali.

JF si tu inawaamsha watawala ila pia inawasaidia sana katika kujua na kufahamu mawazo ya watanzania mbali positive and negative. JF ni mimi wewe, JK, na mawaziri na kila aina ya Mtanzania. Anayekuja na policy ya kipuuzi ni dhahiri anataka kulala fofo na huyo hatakiwi kuwa kiongozi. Ni kweli kabisa kuwa ili kuhakikisha ufanisi ni dhahiri inatakiwa watu watumie muda mwingi wa ofisini katika kutekeleza majukumu yao, Ila unapo target mtandao mmoja kati ya alfu moja kama sababu basi ni dhahiri sababu hizo ulizotoa si za kweli.

Serikali hii ambayo ina mitandao ambayo haiwi updated miaka miwili mitatu minne, ni dhahiri hata huduma ya mitandao kwenye ofisi nyingi za serikali haipo. Kama hii habari ni ya kweli suluhisho si kuangalia effect bali ni kuangalia cause ya kwa nini watu wanaichukia serikali?. Fanyia kazi mambo hayo watu watarudisha imani kwako. Acha uonevu bungeni, mahakamani, polisi, mahospitalini, ofisi za umma, acha kulinda walanguzi wa nchi waliojivisha ngozi ya uanasiasa na uongozi. Haki ni msingi wa maendeleo na amani. Huwezi kujipaka kinyesi halafu ukaanza kushutumu na kuchukia watu kuwa wanaziba pua zao pale unapowakaribia.
Hili nimeligundua katika serikali ya chama tawala CCM mradi wowote unaoanzishwa ni" deal" Hata kama mradi huo ungelikua nia nzuri.Ukipitia vifungu katika bajeti za serikali katika wizara na taasisi za serikali ni wazi utakuta kifungu cha pesa kwa ajiri ya websities lakini ukizitembelea websities hizo utakuta hazifnyiwi uptodate ingawa bajeti ya kufanya hayo inatengwa.Uozo katika chama cha CCM na serikali imefikia wakti mbapo mradi wowote unaoanzishwa sio kwa lengo la kuwanufaisha wananchi bali ni upenyo wa kuchota pesa kifisadi.MUNGU IBARIKI TANZANIA/
 
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa yeye ni Mtaalam wa mambo ya compyuta (bila kukosea shahada yake ya uzamili ni katika mambo ya IT).
Kwa yeye kusema hivyo sio jambo geni kwa tunaomfahamu tangu alipokuwa mkuu wa Wilaya.
Na usishangae ukakuta kuwa naye ni mwana JF.
Asije akawa Bujibuji, maana naona siku hizi amepotea labda yupo kwenye ziara za kujenga rangi za kijani na njano au anatembelea wananchi walioathirika na mafuriko.
 
Mnyetishaji amenipa habari hizi anasema kuna waraka na uamuzi umeptishwa kwa wakuu wote wa Idara Serikalini na mashirika ya Umma kwamba ukikamatwa uko kwenye mtandao wa JF ukiwa ofisini basi na kazi huna .Nina omba mwenye nyeti zaidi aje atupe ukweli zaidi na sababu ya Serikali kuogopa mtandao huu usitembelewe ila unaweza kutembelea hata mitandao ya ngono ila si JF .

Yale yale ya Mkurugenzi wa PPF aliyefukuza kazi watu kwa ajili ya JF. Nafikiri watu wenye mtazamo huu dhidi ya JF ni wale waliowekwa kwenye nafasi walizonazo kwa kuwa wako katika tabaka la watawala - watoto wao, ndugu zao au watoto wa wanamtandao ambao lazima walinde maslahi ya tabaka lao watawala.

Nakumbuka kusoma threads na posts za Mama Tibaijuka humu, na kina Mwigulu nk. Naona kama ni kweli kuna huo waraka waanze kwa kuwafukuza kazi wao.

JF ni kioo cha jamii kama vilivyo vyombo vingine vya habari, kutia ndani na magazeti yao yebo yebo. Nina uhakika JF ni jukwaa linalotoa changamoto nzuri sana kwa maendeleo ya nchi hii, sasa kama baadhi ya viongozi (watawala) wanaona moshi umezidi jikoni waondoke wao humo jikoni, sio kuwaambia wapishi waache kupika.

Pia hii iwe ni changamoto kwa JF kutojipendekeza sana kwa serikali kwa kufuta thread nyingi zenye mantiki zinazokosoa utendaji fulani serikalini. Msifikiri wale jamaa wanaowafuata kuwataka msiruhusu thread fulani fulani ni rafiki zenu. Ni heri mkaacha wakosolewe ili wajirekebishe kwa manufaa ya Watanzania wote.

JF mnawajibika kwa wananchi wa kawaida, sio watawala wenye ubinafsi ambao hawastahili hata kuitwa viongozi.
 
Back
Top Bottom