Ni marufuku kufungua mtandao wa JF ukiwa katika ofisi za Serikali

watakuwa wamefika mahali wamechoka wenyewe tu lakini they used to have waraka going around enzi la Lowasa na mapambano dhidi ya JF .Hapa JF hata JK ni member tena wa siku nyingi yet waraka ulikuwepo mzungukoni .
 
Ndugu

hizo offisi hazina internet user manual - office zote zenye heshima zao kila mfanyakazi anatakiwa awe na user manual hiyo ambayo anatakiwa kuweka sahihi yake mwenywe kwamba hata jihusisha na mitandao yoyote ambayo inashiriki siasa au mambo yoyote ambayo hayana maslahi kwa idara husika , ila wengi kama wana server huwa administrator huwa ana block baadhi ya tovuti moja kwa moja haina haja ya kuja kusumbuana na watumiaji
 
Mnyetishaji amenipa habari hizi anasema kuna waraka na uamuzi umeptishwa kwa wakuu wote wa Idara Serikalini na mashirika ya Umma kwamba ukikamatwa uko kwenye mtandao wa JF ukiwa ofisini basi na kazi huna .Nina omba mwenye nyeti zaidi aje atupe ukweli zaidi na sababu ya Serikali kuogopa mtandao huu usitembelewe ila unaweza kutembelea hata mitandao ya ngono ila si JF .

Maoni yangu yamechelewa maana siku nyingi sikuwapo, lakini bado nitayasema. Nadhani ni sahihi kabisa kuzuia kufungua mitandao ambayo haihusiani na kazi ya huyo mtumishi, maana hapo atakuwa anafanya mambo binafsi kwa gharama za mwajiri wake. Kama uko kwenye ofisi ya umma au hata mwajiri mwingine yeyote, tumia muda huo kufanya kazi uliyoajiriwa hapo. Muda huo ukiisha, na kwa resources zako (mfano internet cafe au nyumbani mwako), jimwage kwa raha zako na mitandao yenye habari unazopenda.

Pia si kweli hata kidogo kuwa ati serikali inaruhusu kuangalia mitandao ya ngono. Mbona hiyo imekatazwa kabisa, na inapigiwa kelele kila kukicha?

Uhuru wa habari haumaanishi kutumia muda wa kazi na vifaa vya mwajiri wako kufanyia mambo yako binafsi yasiyohusiana na kazi uliyoajiriwa. Kama ni kweli limetolewa agizo kama hilo, ni sahihi kabisa, ilimradi lisisitize kuwa siyo kufungua JF tu kunakokatazwa, bali jambo lolote nje ya majukumu ya mwajiriwa.
 
Hawawezi na hawatauweza moto. Kwa sababu kwa kutokufikiri kwao wanadhani wataiua JF na kuhofia pia kuvuja kwa siri zao humu kumbe ndio wanaipa na kuiongezea umaarufu JF. Ni kweli sasa hivi inafanywa mipango ya kuipunguza makali JF hasa ukizingatia mambo yote ya kifisadi yanaanzia hapa na kuwekwa hadharani.
 
wakikataa kuangalizia JF kwenye maofisi ya Serikali hata kwenye cafe za Internet tutaangalia wakati tukienda kupata lunch. Mimi na JF ni kama samaki na Maji.
 
wakikataa kuangalizia JF kwenye maofisi ya Serikali hata kwenye cafe za Internet tutaangalia wakati tukienda kupata lunch. Mimi na JF ni kama samaki na Maji.

Mwenzio mie na JF kama chupi na tak
icon10.gif
 
Mi nafikiri swala la msingi hapa ni kwamba wasizuie wafanyakazi kuingia JF na kwingineko ili mradi kila mtu atimize wajibu na majukumu yake kazini kama inavyotakikana. Sehemu kama JF kuna mambo mengi sana ya kujifunza hasa kwa wafanyakazi wa serikali ambao wengi wao wako kama wana mtindio wa ubungo.
 
Kila kitu chini ya jua kinawezekana, hakuna sehemu ngumu kufanya kitu chochote kwa kumulikwa na camera kama hapa nilipo, bado nachangia mada sana na hawana kitu cha kunifanya.

Jana nilikuwa nasikiliza bongo flava, bosi wangu kapita akazimia wimbo wa tutaonana wabaya nikampa website aingie afanya kazi kwa amani huku akiburudika. Msiendekeze watu waliopo kutufanya watumwa. Kama kazi haipo haipo tu si kwa ajili ya kuchat.
 
huu ni uonevu tena uliokubuhu, tumejua hila na jaja yao, mafisadi wakubwa, waoneee kwanza kazi kunenepusha mavitambi tu. jamani mi nawachukia hawa mafasadi kuliko swijui nini.
 
Siri gani za serikali zinatolewa humu Ndugu Mpenda? Ukifichua ufisadi uliofanywa na kiongozi wa serikali umetoa siri za serikali?

Kama kuna anayejua siri ya serikali iliyotolewa humu mtandaoni naomba atufahamishe.

Kama una lengo la kulinda ufisadi kama siri ya serikali basi wewe ni mtu mbaya sana.
 
Tangu huu waraka umesambazwa enzi hizo wamezuia wangap kuingia JF? Ninachoona JF imekua mara mia moja tangu kipind hicho mpk sasa inajadiliwa bungeni..na kwa mwono wangu watembeleaji na member wengi wamo kwny ofisi za serikali..maana huko ndiko hamna kazi za kumwaga..matokeo yake ni wadau kuona heri waingie JF wapige soga la siasa na maendeleo, matokeo yake ni kuvujisha siri kisha watu makini wanafuatilia na kupata ukweli na kuwapata MAFISADI..mwisho wanaishia kusema eti JF inawachafua! CONGRATS JF FOUNDERS
 
Serikali ya ccm kwa kutoa maagizo wanaongoza japo ngoma ipo ktk utekelezaji ni ziro.Hata warukeruke vipi sikio haliwezi kuzidi kichwa.
 
weeh wala usihofu, marufuku ziko za kutosha lakini hazifanyiwi kazi ( enforced). kama wamewashinda mapacha 3 kuwatimua, wataweza mitandao yoote ya watumishi wa umma tz nzima? achana nao, wee jimwage tu!
Mnyetishaji amenipa habari hizi anasema kuna waraka na uamuzi umeptishwa kwa wakuu wote wa Idara Serikalini na mashirika ya Umma kwamba ukikamatwa uko kwenye mtandao wa JF ukiwa ofisini basi na kazi huna .Nina omba mwenye nyeti zaidi aje atupe ukweli zaidi na sababu ya Serikali kuogopa mtandao huu usitembelewe ila unaweza kutembelea hata mitandao ya ngono ila si JF .
 
Great Thinkers wanataka watu wasifanye kazi badala yake wawe wanasoma JF, halafu wanataka maendeleo. Great Thinkers mnachekesha, manataka JUA au MVUA ?
 
Great Thinkers wanataka watu wasifanye kazi badala yake wawe wanasoma JF, halafu wanataka maendeleo. Great Thinkers mnachekesha, mnataka JUA au MVUA ?
 
Unajua huu mtandao unaogopwa sana na viongozi wa serikali kwani wanajua ni mtandao hatari sana
kwa maslahi yao ndoo maana hawataki watu wengi waufuatilie ili wajue maovu ya serikali yao na kuwafumbua macho,,,,,,
 
Ila tutafika kwani hata serikali ikiwakataza hao watumishi wao kuusoma huu mtandao wakiwa maofisini naamini wakiwa majumbani watasoma tuu....
 
Back
Top Bottom