Ni maandamano au ni mapinduzi?

Wabongo nawajua sana!

Hakuna wa kutia Kwato barabarani

Maandamano yatakuwa kwenye Page ya Mange ya Unstagram pekee na page za Mashabiki wake
Mitaani tutaendelea na Mapumziko ya Muungano
ni hawahawa waliosema mbeya pasingekalika kama sugu angefungwa.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimefuatilia baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Instagram na Telegram kuhusu haya makundi ya watu wanaotamani kuuangusha utawala wa Rais Magufuli. Kwa kiswahili wanasema kuwa hayo ni maandamano ya Amani. Ila kwa Kiingereza wanatamka Tanzania Revolution.

Kwa uelewa wangu, Maandamano tafsiri yake kwa Kiingereza ni Demonstration au Protests. Na Revolution maana yake kwa kiswahili ni Mapinduzi. Kwa uelewa wangu finyu, busara huweza kutumika katika kudeal na maandamano ikiwa ni pamoja na matumizi kiduchu ya nguvu. Ila Mapinduzi hapo lazima ujidhatiti kukabiliana nayo. Hapo silaha za moto na nzito hutumika na ni haki ya vyombo vya dola kutumia nguvu zote ili kulinda himaya dhidi ya maadui wa ndani na nje.

Kingine, Maandamano hudhibitiwa na Jeshi la Polisi. Ila Mapinduzi hapo wanaume wa kazi, JWTZ huingia mzigoni. Hapo silaha zinazotumika ni za moto tu. Hawajafundishwa kutumia TEAR GAS hao.

Kwa hiyo, ni vema wale wanaotamani kuona utawala wa Rais Magufuli unaangushwa wakatafakari upya ni nini hasa wanataka kufanya siku hiyo na nini madhara yake. Ni vema wakaweka wazi je wanataka kuandamana ama wanataka kufanya mapinduzi? Maandamano YES ila MAPINDUZI ni BIG NO. Watu wasije kufumuliwa vichwa wakifanya mapinduzi then wakaanza kulalamika kuwa jeshi la polisi na JWTZ wametumia nguvu ya ziada.

Laiti kama Polisi polisi wangejua kwamba mabadiliko huwa hayazuiliwi ila yanaongozwa, wangekaa kimya wakalinda maandamano na kuyaongoza ili yaende katika mkondo sahihi.
Kuzuia maandamano ya wananchi nchi nzima ni sawa na kusimama kwemye maporomoko ukijaribu kuzuia maji yasianguke.

Hakuna aliyejuu ya mabadiliko. Na mabadiliko hayawezi kuzuiliwa. Siku zote wazuiao mabadiliko, hubadilishwa na mabadiliko yenyewe. Mabadiliko yakikubadilisha, yatakupeleka hata usikotaka kwenda. Heri kukubali badiliko ili uyaongoze katika njia sahihi na yenye ubora na faida kwa kiwango kikubwa.
 
Lugha Inayo tumika kweli sio sahihi.
nadhani wanakusudia maandamano ya kutoridhika na utawala wa Magufuli. Hivyo maandamnao ya kushikiza ajiuzulu au bunge lichukue uamuzi mgumu wa ku mu impeach kwa kushindwa kuilinda katiba na kutekeleza majukumu yake bila ya upendeleo
nadhani wanakusudia hili. ila lugha labda kidogo wanayo tumia sio sawa.
nimeona Mange akisema hawataki hata ccm kuondoka in fact wanataka Mama Samia apewe serikali.
hivyo tatizo sio serikali bali mtu mmoja
hapo sasa sielewi kama ni mambo ya polisi au JwTZ.....
Haya bado ni mambo ya kiraia na kisiasa...hivyo police ndio yana wahusu kama watahisi wazuie kunafaa ama kuachia

kWANI wewe hujui utaratibu wakumuondoa mtu aliyechaguliwa kidemocrasia au na wewe ni wale wale tu.Katiba imeweka utaratibu mmeufuata?? Nyinyi jipangeni mnavyotaka mkono wa chuma unawasubiri,na safARI HII lazima fundisho litolewe kwa wazembe wa kufikiria mnadhani tumefurahi na propoganda zenu chafu za kitoto
 
Laiti kama Polisi polisi wangejua kwamba mabadiliko huwa hayazuiliwi ila yanaongozwa, wangekaa kimya wakalinda maandamano na kuyaongoza ili yaende katika mkondo sahihi.
Kuzuia maandamano ya wananchi nchi nzima ni sawa na kusimama kwemye maporomoko ukijaribu kuzuia maji yasianguke.

Hakuna aliyejuu ya mabadiliko. Na mabadiliko hayawezi kuzuiliwa. Siku zote wazuiao mabadiliko, hubadilishwa na mabadiliko yenyewe. Mabadiliko yakikubadilisha, yatakupeleka hata usikotaka kwenda. Heri kukubali badiliko ili uyaongoze katika njia sahihi na yenye ubora na faida kwa kiwango kikubwa.
Mapinduzi yanazuiliwa kaka. Huwezi kusema unataka kumuondoa Rais Magufuli Madarakani then ukataraji vyombo vya dola vikuchekee tu
 
Mapinduzi yanazuiliwa kaka. Huwezi kusema unataka kumuondoa Rais Magufuli Madarakani then ukataraji vyombo vya dola vikuchekee tu

Wewe unaongelea mapinduzi. Mimi naongelea mabadiliko. Hayo mapinduzi mtayafanya huko ccm lakini sisi watanzania tunataka mabadilko murua na maandamano yetu ni ya amani, hata box la biscuits hatutakuwa nalo!
 
Maandamani ni haki ya kikatiba kama ilivyo vyama vya kisiasa labda ikiwa kifungu hicho kimeondolewa. Mambo ya watu wachache kuondoa haki iliyotolewa kikatiba ni uhuni ambao ukichekewa utatuletea majuto
kifungu kipi cha katiba kina neno maandamano au kilichoruhusu maandamano
 
kWANI wewe hujui utaratibu wakumuondoa mtu aliyechaguliwa kidemocrasia au na wewe ni wale wale tu.Katiba imeweka utaratibu mmeufuata?? Nyinyi jipangeni mnavyotaka mkono wa chuma unawasubiri,na safARI HII lazima fundisho litolewe kwa wazembe wa kufikiria mnadhani tumefurahi na propoganda zenu chafu za kitoto
Mbona povu..
 
Wanaongozwa na Mnyonya koni. Mapinduzi kote duniani hudhibitiwa kwa silaha za moto. Na ndivyo itakavyotokea siku hiyo wakithubutu
Lizaboni kweli umechanganikiwa, nakupa mapungufu ya kipumbavu nilioyaona kwenye bandiko lako...nachelea kusema ya kipumbavu kwa sababu ni ya kipumbavu hujayapa makalio yako nafasi ya kufikiri;-

1.Revolution ni mapinduzi...lakini neno mapinduzi halilengi katika kuondoa tawala tu!!!, Tazama mambo yalivyo katika nchi yetu!!, katiba ya kishenzi, unafiki wa kifikra kama ulionao wewe...kuyabadilisha haya ni sehemu ya mapinduzi.....

2.Hao unaowaomba wakae barabarani na mashine za moto....amini nakwambia, hata gabbo wa ivory cost, pindi anaondolewa, wale waliomlinda, ndio qwaliomshinikiza aongozane nao apelekwe jela kistaarabu...akibisha na yeye aone cha mtyema kuni...kwa mantiki hii basi...kwanza unatakiwa kujua...mzee baba, sio sehemu wa hao jamaa kumpenda...kifupi mzee baba hapendeki hapo.

ukitaka kujua, hao jamaa, pia wanasikitikaga sana, na tabia za madharau kwao yatokanayo na mtoto wa mzee baba, na mzee baba mwenyewe...mugabe nae alikua analindwa nao...ila uliona.

usijitoe akili....hawa ni sehemu ya jamii...ndio mliowaondolea duty free shop, kwa ahadi ya kuwaongezea mishahara ambayo hamjawaongeza.

kalagabahooooo

Ila mjue tu...ipo siku, nyie tutakua tunapishana...mkilelekea mahakama ya kisutu kujibu mashtaka ya ndani....sisi tukiwabeza kama mfanyavyo sasa....ni muda tu!!!
 
Mimi nilifikiri namna bora na sahihi ya kukabiliana na maandamano ni kufahamu madai yao na kuyafanyia kazi hilo la nguvu ndogo and nguvu kubwa halitatui kilichowafanya waandamane.

Mh Raisi aagize wakuu wote wa mikoa (kama ni kweli) wapokee hayo maandamano na kuchukua malalamiko yao na kuyapeleka serikali (Kwa Mh. Raisi) ili yale ya kweli yafanyiwe kazi
Hawana wabunge? wapeleke kero zao kwa wabunge wao halafu wabunge wapeleke kunakohusika
 
kWANI wewe hujui utaratibu wakumuondoa mtu aliyechaguliwa kidemocrasia au na wewe ni wale wale tu.Katiba imeweka utaratibu mmeufuata?? Nyinyi jipangeni mnavyotaka mkono wa chuma unawasubiri,na safARI HII lazima fundisho litolewe kwa wazembe wa kufikiria mnadhani tumefurahi na propoganda zenu chafu za kitoto
Braza. Vipi ?
Wakija kumi mtaua wrote ??
Jee wakija Mia moja mtauwa wrote ???
Jeee wakija Elfu moja mtauwa wooteee ????

Bas sawa. Pata picha watu elfu moja wamelala chini hapo DSM kwa risasi !!!!!!
 
Wewe unaongelea mapinduzi. Mimi naongelea mabadiliko. Hayo mapinduzi mtayafanya huko ccm lakini sisi watanzania tunataka mabadilko murua na maandamano yetu ni ya amani, hata box la biscuits hatutakuwa nalo!
Mtajitahidi kubadili chupa mpya lakini mvinyo yenu imesikika harufu yake na hainyweki kwa watanzania
 
Back
Top Bottom