Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimefuatilia baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Instagram na Telegram kuhusu haya makundi ya watu wanaotamani kuuangusha utawala wa Rais Magufuli. Kwa kiswahili wanasema kuwa hayo ni maandamano ya Amani. Ila kwa Kiingereza wanatamka Tanzania Revolution.
Kwa uelewa wangu, Maandamano tafsiri yake kwa Kiingereza ni Demonstration au Protests. Na Revolution maana yake kwa kiswahili ni Mapinduzi. Kwa uelewa wangu finyu, busara huweza kutumika katika kudeal na maandamano ikiwa ni pamoja na matumizi kiduchu ya nguvu. Ila Mapinduzi hapo lazima ujidhatiti kukabiliana nayo. Hapo silaha za moto na nzito hutumika na ni haki ya vyombo vya dola kutumia nguvu zote ili kulinda himaya dhidi ya maadui wa ndani na nje.
Kingine, Maandamano hudhibitiwa na Jeshi la Polisi. Ila Mapinduzi hapo wanaume wa kazi, JWTZ huingia mzigoni. Hapo silaha zinazotumika ni za moto tu. Hawajafundishwa kutumia TEAR GAS hao.
Kwa hiyo, ni vema wale wanaotamani kuona utawala wa Rais Magufuli unaangushwa wakatafakari upya ni nini hasa wanataka kufanya siku hiyo na nini madhara yake. Ni vema wakaweka wazi je wanataka kuandamana ama wanataka kufanya mapinduzi? Maandamano YES ila MAPINDUZI ni BIG NO. Watu wasije kufumuliwa vichwa wakifanya mapinduzi then wakaanza kulalamika kuwa jeshi la polisi na JWTZ wametumia nguvu ya ziada.