Ni kweli Sugu kataka wawakatae hata kwa mawe viongozi wabovu?

Ni kweli ameyasema haya, na ni makosa makubwa sana kwake kisiasa....tatizo ameshindwa kutofautisha ethics za Bongo Fleva na Ubunge..mwenyekiti alifanya kazi ya ku-qualify statements za Sugu palepale jukwaani..ilikua ni aibu sana aiseee..

Aibu ya wapi wewe?mnalalamika kuhusu wizi alafu wenyewe tena mnatetea wizi,namuunga mkono SUGU tena napenda wazo hilo liingie kwenye katiba,we unasemaje?
 
mkuu,sijui wengine wataonaje kitu hiki!
ila mimi naona ni kama kuichafua chadema,na hii haitakiwi kuachwa hivi,...
1.kama ni kweli sugu aonywe kutoa kauli za ajabu ajabu hivi
2.kama sio kweli,basi wakanushe habari za gazeti hili,....

In any ways,wakilikalia kimya bila kuangalia ukweli uko wapi lita waghalimu sana

Lazima umesikia kutoka kwenye gazeti la CCM
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wheather amesema au hajasema -lazima tuanze kubadilika naona speaker umelishikia bango saana suala hili thread nzima ni wewe -hawa mafisadi hawastaili kupigwa mawe tu wanastaili kupelekwa mahakamani wawajibishwe lakini kwa kuwa wamechakachuwa mpaka huo mkondo njia rahisi ni wananchi kuwakataaaa na kuwaambia hutuwataki mnatunyonya, mnatukandamiiza na mnatufanyahali zetu za maisha kuwa ngumu saana. Sugu sio mnafiki -nchi hii inaporomoka shimoni kwa sababu ya unafiki unafiki unafiki uliopitiliza, wewe unajua hawa ni mafisadi na ndio wanaotupeleka shimoni halafu unasema wabembelelezwe mpaka lini?????? tuache unafiki jamani utatua ----big up Sugu songa mbele -vita ya kulikomboa taifa toka kwa mafosadi sio lelemamama lazima tutambue.

Naunga mkono mkuu,sheria zote wameishazinunua MUNGU mwenyewe ameshakasirika,ametupa kila aina ya utajiri lakini bado tunashida,kwa sababu ya hawa wezi why tubembelane?
 
&lt;br /&gt;<br />
<br />

Acha ubaguzi na pumba zako za kidini.Zingatia hoja na utoe comment zenye mashiko na sio kurukaruka kama changudoa.Usiweke ushabiki ata kwenye vitu vya kipuuzi.MR. II ni kijana wa mtaani kwa maana ya purukushani zisizo na nidhamu,mbali na kupata ubunge kibahati lakini pia hajajiandaa kukaa kiuongozi zaidi ya kufikiri siasa ni kama rap zake za sugu.Tufikie maana tuseme ukweli juu ya tabia za aibu za huyu na wala si kushabikia na kutoa mifano ya mbona.........na.......sijui tabora....waislam.

Naomba utueleze vizuri,unasema SUGU ni kijana wa mtaani wengine ni ni vijana wa wapi?ni sehemu gani ambapo hakuna mitaa?au unalopoka tu ili mladi.
 
Tunataka tujue alichoongea ili nasi tujue tunachosema tusije tukawa au ili tukawe wote akili sawa. Wajinga, wapumbavu, werevu ama wenye hekima kama wewe speaker.
 
Nimesikia kwenye habari za magazetini asubuhi
hii kwamba mbunge wa mbeya mjini
ame hamasisha wana nchi wa mbeya kwamba
akija kiongozi ambaye hawamtaki,...
au kiongozi yeyote,hata kama "ni raisi" ni haki yao kumkataa
haka kwa kumpiga mawe!

Kama hii ni kweli,basi Dr.Slaa na wazee wengine ndani ya chadema
mna kazi ya kuwafundisha wabunge vijana
jinsi ya kuongea kwenye public na jinsi ya kutembea "normal" ukiwa na uheshimiwa!

Hizi sio kauli za kutolewa na kiongozi yeyote yule,...
kuna watu walio kuwa wanataka kujiunga na chadema,au walio
muunga mkono sugu,..na ambao ni wastaarabu watakua hawaja furahiswa na
kauli hii,...

na hao wataendelea kuamini kuwa chadema wana hamasisha vurugu!

Ombi:
Naomba viongozi wa chadema,walioko huko kwenye maandamano
wakanushe maneno haya (kama sio kweli kwamba sugu haku yatamka)
maana naamini kila alosikia habari hii kasikitishwa sana,...

Hivi ulishawahi kuona mtu mstaarabu akiwa na njaa? Ustaarabu ni baada ya tumbo kushiba. Namuunga mkono Sugu kwasababu serikali ya CCM iliamua kutokufuata sheria kwa kuwapa mafisadi msamaha huku watoto wachanga wakifa kila leo kwa malaria, watoto wakikosa madawati na waalimu wa kuwafundisha huku wao wakifanya usanii wakuwatembelea kwenye maeneo yao na magari yenye thamani zaidi ya garama za vibanda vyote wanavyoishi watu vijijini. Hao wastaarabu waache wabakie kwenye chama chao cha magamba tuone mwisho wa siku nani kati ya sisi na wao wanamhitaji mwingine. Tuone kama wataendelea kuwa wastaarabu wakikosa sehemu ya kuchota ili washibishe matumbo yao. Hakuna ustaarabu kwa mtu mwenye njaa na shida! Sugu koleza moto mpaka kieleweke acha watuite majina yote wakishayamaliza warudie sense zao kwamba wakati ukuta!
 
Nimesikia kwenye habari za magazetini asubuhi
hii kwamba mbunge wa mbeya mjini
ame hamasisha wana nchi wa mbeya kwamba
akija kiongozi ambaye hawamtaki,...
au kiongozi yeyote,hata kama "ni raisi" ni haki yao kumkataa
haka kwa kumpiga mawe!

Kama hii ni kweli,basi Dr.Slaa na wazee wengine ndani ya chadema
mna kazi ya kuwafundisha wabunge vijana
jinsi ya kuongea kwenye public na jinsi ya kutembea "normal" ukiwa na uheshimiwa!

Hizi sio kauli za kutolewa na kiongozi yeyote yule,...
kuna watu walio kuwa wanataka kujiunga na chadema,au walio
muunga mkono sugu,..na ambao ni wastaarabu watakua hawaja furahiswa na
kauli hii,...

na hao wataendelea kuamini kuwa chadema wana hamasisha vurugu!

Ombi:
Naomba viongozi wa chadema,walioko huko kwenye maandamano
wakanushe maneno haya (kama sio kweli kwamba sugu haku yatamka)
maana naamini kila alosikia habari hii kasikitishwa sana,...

Speaker lisemwalo lipo...huu ni wakati muafaka wa kuwapima viogozi wetu vision zao na wanako taka kutupeleka. Kama ni kweli basi naamini kwamba CDM pia kuna viongozi wamechaguliwa because of situational na sio viongozi. Na kama mwendo ni huu tutapata fursa nzuri kujua je ni sahihi CDM kuingia madarakani au tubaki na ZIMWI LETU kwani ZIMWI LIKUJUALO ALIKULI LIKAKWISHA.1
 
kila mtu atapewa nafasi ya kugombea na kuwa kiongozi ndani ya chadema,..
na kila mtu ata fundishwa jinsi ya ku-act kama kiongozi!

Hakuna aliye kamili,kosa atakalo fanya sugu ni kuto jifunza baada ya jama kukemewa
Amekemewa ama ameshauriwa?
 
CDM bado sana kuongoza nchii tuanofikiri ni viongozi wengi wao sio kabisa hamna kitu!!! just wait TIME WILL TELL.
 
Kama ni kweli sugu katamka maneno hayo viongozi wa juu wa CDM wanapaswa kumkanya kumpa adhabu maana anakiweka chama pabaya. Ni kauli mbovu ambazo hata wana chadema hawawezi kuzifurahia.
Wabunge wana misimamo yao binafsi ambayo inaheshimiwa hata kama haikipendezi chama.Zito rooted for DOWANS.Anaweza akawa ameongea kauli hatarishi Mh Sugu.Lakini adhabu?I dont think so.Ashauriwe tu kwamba wezi wafikishwe kwenye vyombo vya sheria badala ya kupigwa mawe.Acheni unafiki!Mnachoma moto vibaka daily na kuwaponda majabali halafu mnaleta unafiki.Ama kwasababu wengine ni wezi wakubwa?Sugu anazungumza yale yaliyoko kwenye jamii....Kwamba wanabondwa mawe.Acheni kupiga mawe vibaka na kuwaua kwanza kabla hamjaongea upupu kwamba vibaka wa ngazi za juu waombwe radhi.
 
Lazima umesikia kutoka kwenye gazeti la CCM

Nyie ndo mkiambiwa mme wako anatembea na house gal, mnasema "hamsikilizi maneno ya majirani",...
sometimes umbea wa majirani ni muhimu,..unakusaidia kujijua
 
Tunataka tujue alichoongea ili nasi tujue tunachosema tusije tukawa au ili tukawe wote akili sawa. Wajinga, wapumbavu, werevu ama wenye hekima kama wewe speaker.

nahisi upo kwanye category ya ubwege,uzezeta,umbumbu!
ungekua na hekima japo kidogo ungesoma post za atleast page mbili ungejua nini kinaongelewa humu!
 
Nyie ndo mkiambiwa mme wako anatembea na house gal, mnasema "hamsikilizi maneno ya majirani",...
sometimes umbea wa majirani ni muhimu,..unakusaidia kujijua

Tatizo speaker ni ukweli wako kwani umeguza pasipo gusika lakini hawajui kuna kupitiwa na kujirekebisha. Ukisema ukweli basi wewe ohoo umepata kwa majirani hooo sijui nin? baba we endelea kuleta mambo na nafikiri wewe ni speaker mwenye viwango vya mzee six!!!!
 
Naombeni kuwauliza,...
1.hao mlio wataja ni binadamu pia,wakijisaidia haja kubwa milangoni kwao na nyie mta waiga?
2.kwa maana hiyo kila kitu inabidi kifanywe "kwa sababu ccm wamefanya"?
3.nini tofauti kati ya chadema na ccm?
4.mnataka kusema kwamba,chadema ikishika madaraka
wakatokea mafisadi ndani ya serikali ya chadema tusiulize kwa
sababu tutajibiwa "mbona waliwahi kuwepo wa ccm kama RA,EL etc"?

Tumieni akili kidogo,sio kujibu kama tabwe hiza kila kitu

Mkuu naona bado hujanipata, haimaanishi kuwa kila kinachofanywa na CCM lazima kiigwe na wengine, Ila tunapoongelea jamii ya watanzania hasa ukirudi darasani kwenye somo la kiswahili kuna kitu kinaitwa "misimu na misemo" katika fasihi simulizi hizi hubeba maana fulani inayokubalika na jamii, sasa ikitokea kuwa mtu anapotosha maana katika jamii ni lazima aambiwe kuwa you are wrong. Hoja kama hii haina tofauti na GOP ambao mwaka 2008 walimshambulia Obama kuwa kamwita Sarah Palin "Pig" kwa kusema kuwa, " You can put lipstick on a pig but it is still a pig" Wakasahau kuwa hata mtu wao aliutumia msemo huo mara kibao na mwisho wakabaki vichwa chini kwa kuambiwa ukweli.
Huwezi kumtuhumu mwanasiasa anachochea ghasia kwa kutamka maneno yanayoeleweka kwa wananchi kwa mtazamo mwingine, ndiyo maana nasema kama ukiona limekuuma basi na wenzio liliwauma. This nonesense of trying to define your opponents sometimes go back to yourself. CCM mara ngapi wamemwita Dr. Slaa kuwa mwizi wa wake za watu?. I am non partisan but I am pro democracy that's why siwezi kukaa kimya kuona watu wanatumia mbinu chafu kuua demokrasia. Tanzania itaendelea pale walio madarakani watatumikia wananchi na hilo linawezekana kama tu wananchi wataachwa kuchagua viongozi wao halali bila hila na mabavu toka CCM. Madaraka ni dhamana na siku wenyewe wakiwa na nguvu ya kumuweka wanayemtaka ni dhahiri atawatumikia wao.
 
Atleast kwenye post hii umepunguza mori.
Mimi siko Mbeya, pengine wewe pia. Lakini tuna jambo la kulijadili.
Umeongea kuhusu misimu, mimi nitaongeza na tungo tata ambapo ili kujua maana katika mazingira ya namna hiyo uwasilishaji ni muhimu sana.
Ni rahisi sana kujua mtu anamaanisha ni anaposema maneno kama "kichaa", "kanga" au "barabara" pamoja na kuwa na maana zaidi ya moja kutokana tu na namna yalivyowasilishwa.
Watu wanayajua hayo ndiyo maana hata hukusikia malalamiko labda wapinzani wametakiwa "kuchanwa na kutupwa" kama Tot walivyowasilisha.
Kwa taarifa tulizipata hapa ni dhahiri kuwa Mbilinyi alitamka hayo kwa maana ambayo wewe hutaki kuiamini, haikuwa fasihi kama ambavyo ungependa. Ndiyo maana Mbowe aliamua kuokoa jahazi kama unavyofanya wewe hapa.
Kwa maoni yangu, the mp should never behave like that especially before the public! Huku mitaani siyo ishu, yanaongewa na kufanywa zaidi ya hayo.
Speaker kaongea mengi sana ya kujenga tena with option, kama kweli amesema na kama ni uzushi au propaganda. Mambo yanayowafanya wengi wanaoyapinga wakose hoja, wanabakia na ushabiki tu kitu ambacho hakina tija kwa Chadema, hakina tija kwa Tanzania...
 
Mkuu naona bado hujanipata, haimaanishi kuwa kila kinachofanywa na CCM lazima kiigwe na wengine, Ila tunapoongelea jamii ya watanzania hasa ukirudi darasani kwenye somo la kiswahili kuna kitu kinaitwa "misimu na misemo" katika fasihi simulizi hizi hubeba maana fulani inayokubalika na jamii, sasa ikitokea kuwa mtu anapotosha maana katika jamii ni lazima aambiwe kuwa you are wrong. Hoja kama hii haina tofauti na GOP ambao mwaka 2008 walimshambulia Obama kuwa kamwita Sarah Palin "Pig" kwa kusema kuwa, " You can put lipstick on a pig but it is still a pig" Wakasahau kuwa hata mtu wao aliutumia msemo huo mara kibao na mwisho wakabaki vichwa chini kwa kuambiwa ukweli.
Huwezi kumtuhumu mwanasiasa anachochea ghasia kwa kutamka maneno yanayoeleweka kwa wananchi kwa mtazamo mwingine, ndiyo maana nasema kama ukiona limekuuma basi na wenzio liliwauma. This nonesense of trying to define your opponents sometimes go back to yourself. CCM mara ngapi wamemwita Dr. Slaa kuwa mwizi wa wake za watu?. I am non partisan but I am pro democracy that's why siwezi kukaa kimya kuona watu wanatumia mbinu chafu kuua demokrasia. Tanzania itaendelea pale walio madarakani watatumikia wananchi na hilo linawezekana kama tu wananchi wataachwa kuchagua viongozi wao halali bila hila na mabavu toka CCM. Madaraka ni dhamana na siku wenyewe wakiwa na nguvu ya kumuweka wanayemtaka ni dhahiri atawatumikia wao.

Mkuu umeongelea mfano wa obama kumuita mwenzake pig,...
umeongelea pia mfano wa Dr.slaa kuitwa mwizi wa wake za watu,...
sawa,.

lakini haya ya sugu yanaashiria kuumiza mtu,kuua mtu,..(inategemea baada ya kupigwa mawe mangapi nasijui kama atapona).

Nimetoa mfano wa pinda kusema "wauaji wa albino wauawe pia",...kauli ile ni kinyume na haki za kuishi
alizonazo kila mtu,ilimtoa machozi bungeni!

Kuitwa mwizi,pig,nk hakudhuru au kuondoa uhai wa mtu,...
kumponda mtu mawe kunaweza kuondoa uhai wake,...

angesema zomeeni nisinge shangaa,infact nimewahi zomea sana,...lakini kuponda mawe?
nayo ni fasihi,usemi?

haya,pondeni mawe,hamasisheni kuponda mawe,...ila mkumbuke kuzika mlowaponda mawe pia
 
Aibu ya wapi wewe?mnalalamika kuhusu wizi alafu wenyewe tena mnatetea wizi,namuunga mkono SUGU tena napenda wazo hilo liingie kwenye katiba,we unasemaje?

Hakuna anayebisha kwamba mapambano ni muhimu....strategies ni lazima ziwepo,kumbuka CHADEMA wamejijengea heshima kama watu makini, sasa unadhani mbele ya wakazi wa Mbeya sura ya chama ingeonekana vp kwa maneno ya kisela kama yale??? Mafisadi wanatakiwa wauawe ikibidi, lakini kila jambo lina utaratibu ndugu, mambo hayalipuki kama vichomi tu....
 
Wewe ni speaker hewa kwanini niulize?

1. hujui unachoandika,
2. huna sours ya habari hii,
3. Umesema umesikia redioni na redio ilikuwa ndani wewe uko njee na hukujua i redio gani kwa mtu makini hustahili kumshauri hata kichaa kwa maana inawezekana kichaa akamshauri mwerevu....futa hii thread wewe ni hewa kama maoni yako, huna cha maana cha kuongelea bali ni siasa na kuchafuana tizama ma air phone yako utadhani una avoid altitude sickness kajiandae upya kwa ajili ya kuwadanganya wajinga wenzako

so mtu akipigwa ndo useme endeleeni kumpiga?
sidhani kama wata muachia hili lipite hivi hivi
 
nimesikia imani wakisema mbowe amzodowa sugu kisa sugu awahamasisha kuwatwnga mawe mafisadi akiwemo jk walio sikia yaliyo semwa watuhabalishe
 
Back
Top Bottom