Ni kweli Sugu kataka wawakatae hata kwa mawe viongozi wabovu?

Hawa ndio viongozi wanaotaka tuwakabidhi nchi yetu watuongoze, nchi inaongozwa na utawala wa kisheria sasa huyu Mbunge wa Chadema SUGU anasema watu wapigwe mawe yaani ni upuuzi kuwa na wabunge kama hawa, tatizo kuongozwa na wahuni 'washarobaro' pumba tupu huyu Sugu abakie kwenye bongo fleva akatoe matusi yake huku. nyie Chadema Tanzania ni nchi ya amani msituletee uhuni wenu na wabunge wenu wavuta bangi
 
Ni gazeti gani hilo? Nimesoma Mtanzania, Majira, Tanzania Daima, Mwananchi, Nipashe na Habari Leo sijaona hiyo kitu... labla kwenye mzalendo au magazeti ya Kiingereza?
 
Ni kweli alisema hivyo,ila Mh.MBOWE aliyarejea na kuyafafanua palepale mkutanoni kuwa,tuwapige mawe kwa kuwakataa wao na pamoja na sera zao.Hata hivyo,sidhani kama SUGU alimaanisha kuwapiga mawe kwelikwani akihitimisha maneno hayo alisema;tuwapige mawe,tuwakatae kabisa.Ni wajibu wa viongozi kufafanua lugha zenye utata wanazotumia wawapo jukwaani kwani tafsiri tofauti huweza kujengeka;KAMA AMBAVYO HUYO MWANDISHI ANATAKA TUAMINI,NAMNA ALIVYORIPOTI NI TOFAUTI NA NILIVYOSHUHUDIA
 
ni kweli alisema hivyo,ila mh.mbowe aliyarejea na kuyafafanua palepale mkutanoni kuwa,tuwapige mawe kwa kuwakataa wao na pamoja na sera zao.hata hivyo,sidhani kama sugu alimaanisha kuwapiga mawe kwelikwani akihitimisha maneno hayo alisema;tuwapige mawe,tuwakatae kabisa.ni wajibu wa viongozi kufafanua lugha zenye utata wanazotumia wawapo jukwaani kwani tafsiri tofauti huweza kujengeka;kama ambavyo huyo mwandishi anataka tuamini,namna alivyoripoti ni tofauti na nilivyoshuhudia




hata hivyo 'watu kushangilia kwa kiasui kile baada ya kauli hizo ni ishara ya kuwa wamekata tamaa na huenda awkaleta mabadiliko kwa gharama yeyote ile ikiwa mianya itazibwa,ni angalizo tu kwa mafisadi na viraka wao ambao wako tayari kuchafua jiji zima la mbeya kwa kusambaza vijikaratasi vya kichochezi dhidi ya maandamano ya cdm.
 
Hawa ndio viongozi wanaotaka tuwakabidhi nchi yetu watuongoze, nchi inaongozwa na utawala wa kisheria sasa huyu Mbunge wa Chadema SUGU anasema watu wapigwe mawe yaani ni upuuzi kuwa na wabunge kama hawa, tatizo kuongozwa na wahuni 'washarobaro' pumba tupu huyu Sugu abakie kwenye bongo fleva akatoe matusi yake huku. nyie Chadema Tanzania ni nchi ya amani msituletee uhuni wenu na wabunge wenu wavuta bangi
 
Mleta mada kasikia mtu anapita na redio nje,ikasema maneno ayo,mleta hoja kakaa kaandika mada! Kazi ipo! Fuatilia ujumbe mzima jaman,aya great thinkers.


Ni kweli ila mwndishi alipaswa kuripoti/kutanabaisha pia kuwa kauli hiyop ilifafanuliwa ndani ya mkutano ule ule
 
Nimesikia kwenye habari za magazetini asubuhi
hii kwamba mbunge wa mbeya mjini
ame hamasisha wana nchi wa mbeya kwamba
akija kiongozi ambaye hawamtaki,...
au kiongozi yeyote,hata kama "ni raisi" ni haki yao kumkataa
haka kwa kumpiga mawe!

Kama hii ni kweli,basi Dr.Slaa na wazee wengine ndani ya chadema
mna kazi ya kuwafundisha wabunge vijana
jinsi ya kuongea kwenye public na jinsi ya kutembea "normal" ukiwa na uheshimiwa!

Hizi sio kauli za kutolewa na kiongozi yeyote yule,...
kuna watu walio kuwa wanataka kujiunga na chadema,au walio
muunga mkono sugu,..na ambao ni wastaarabu watakua hawaja furahiswa na
kauli hii,...

na hao wataendelea kuamini kuwa chadema wana hamasisha vurugu!

Ombi:
Naomba viongozi wa chadema,walioko huko kwenye maandamano
wakanushe maneno haya (kama sio kweli kwamba sugu haku yatamka)
maana naamini kila alosikia habari hii kasikitishwa sana,...

Toa source ya habari.
Je ni gazeti gani?
Leo ni jumapili, so yawezekana hiyo habari imeandikwa kwenye gazeti lao la mzalendo...
 
Hawa ndio viongozi wanaotaka tuwakabidhi nchi yetu watuongoze, nchi inaongozwa na utawala wa kisheria sasa huyu Mbunge wa Chadema SUGU anasema watu wapigwe mawe yaani ni upuuzi kuwa na wabunge kama hawa, tatizo kuongozwa na wahuni 'washarobaro' pumba tupu huyu Sugu abakie kwenye bongo fleva akatoe matusi yake huku. nyie Chadema Tanzania ni nchi ya amani msituletee uhuni wenu na wabunge wenu wavuta bangi

Mkuu Ritz,

Tanzania haifuati utawala wa sheria kwa sababu zifuatazo:


  • CCM wanaweza kwenda benki kuu na kuiba pesa na wakaitumia kwenye uchaguzi (EPA)
  • Richmond scandle: kutofuata sheria ya manunuzi tukaingia mkenge na hakuna aliyewajibishwa kisheria
  • Raisi anakiri kuwa anaorodha ya wauza madawa ya kulevya, mpaka leo hakuna hatua za kisheria zilizochukuliwa juu yao.
Tanzania si nchi ya amani, watu wanakufa na kujeruhiwa na mabomu Mbagala, Gongo la Mboto na sijui next ni wapi...hiyo si nchi ya amani hata kidogo!!

Watu wanakufa kwa kukosa madawa hospitalini, akina mama wanakufa kwa kukosa huduma nzuri wakati wanajifungua, wananchi wengi hawana uhakika wa mlo wa siku...huwezi kuiita nchi hiyo ni ya amani kama akili yako inafanya kazi sawa sawa.

Hamuwezi kuwa na amani kama milipuko ya magonjwa kama ya kipindupindu ni wakati wowote ule...

Sugu is very right, we need to start fighting these corrupt leaders wherever they go, so they know that we are not at all happy with the manner in which they lead this country. Those days when we used to clap to corrupt leaders as they pass around stealing our resources have long since gone.

Vibaka muwaue na kuwachoma moto halafu majizi makubwa yapigiwe makofi, wapi na wapi!!
 
Nimesikia kwenye habari za magazetini asubuhi
hii kwamba mbunge wa mbeya mjini
ame hamasisha wana nchi wa mbeya kwamba
akija kiongozi ambaye hawamtaki,...
au kiongozi yeyote,hata kama "ni raisi" ni haki yao kumkataa
haka kwa kumpiga mawe!

Kama hii ni kweli,basi Dr.Slaa na wazee wengine ndani ya chadema
mna kazi ya kuwafundisha wabunge vijana
jinsi ya kuongea kwenye public na jinsi ya kutembea "normal" ukiwa na uheshimiwa!

Hizi sio kauli za kutolewa na kiongozi yeyote yule,...
kuna watu walio kuwa wanataka kujiunga na chadema,au walio
muunga mkono sugu,..na ambao ni wastaarabu watakua hawaja furahiswa na
kauli hii,...

na hao wataendelea kuamini kuwa chadema wana hamasisha vurugu!

Ombi:
Naomba viongozi wa chadema,walioko huko kwenye maandamano
wakanushe maneno haya (kama sio kweli kwamba sugu haku yatamka)
maana naamini kila alosikia habari hii kasikitishwa sana,...

Sina uhakika na habari yako kama ni muendelezo wa kujichuna gamba au kujivua gamba. Ila katika siasa kuna misamiati mingi sana hata kama amesema cha ajabu nini?, au ndiyo kutaka kupenyeza agenda mnazotaka?, mi nadhani watanzania wana akili sana zaidi ya baadhi ya waanzisha mada hapa JF na wanasiasa waganga njaa. Kauli kama hizi zimewahi tolewa mara nyingi.

  1. "CCM tuwabebe, tuwakumbatie Tuwabusu, WAPINZANI tuwachanechane tuwatupe" - TOT ya CCM - Je wanamaanisha kuwachachana wapinzani kwa visu, viwembe, au mapanga?
  2. "Hii ni vita na lazima tushinde" - JK on 2010 election Je alimaanisha kutumia jeshi la wananchi linalomtii kupigana?
  3. "CHADEMA Itakufa" - Mukama, Je alimaanisha kuua wanachadema(i.e viongozi na wanachama na wapenzi wa chama?)
JF is more than this kind of stuff, ndiyo maana siku hizi watu makini siwaoni hapa maana jamvi limevamiwa na viwavi jeshi wao hawachagui wala kuchuja, reputation ya member hujengwa na member kwa kuwa na uwezo wa kujenga hoja siyo cheap propaganda, ungeijengea hoja mada yako kuliko kuiacha ina hang hewani.
 
CCM walikuwa na wimbo maarufu sana uliokuwa ukiongozwa na kapt Komba wakisema
'wapinzani tuwachanechane tuwatupe'

Siku hizi siusikii hata kwenye kampeni mwaka jana sikuusikia,kulikoni ?
 
hapa ni swala moja ni gazeti gani hilo mkuu maana nashangaaa..:A S cry:
 
Nilisema kwenye thread zilizotangulia kuwa elimu na profile ya Sugu ni ZERO hivyo jimbo liko wazi mpaka 2015 lakini wachangiaji wenye uelewa mdogo wakanibeza. Ujumbe wangu kwa CDM ni kwamba wanahitaji kumpolish Sugu aondokane na kuropoka ki-hiphop kwa ajili ya faida ya chama. Sasa angalia huo utumbo anaoutapika mbele ya waliomchagua
 
siwezi kuchangia topic ya kijinga hivi , mimi niko mbeya na nilikuwepo kwenye huo mkutano na napenda kuwakikishia kuwa Sugu hajasema hayo bali yamebuniwa na waandishi fulanifulani wa chama fulani kwa malengo fulani , Sugu mwenyewe watu wa namna hiyo anawaita...MAKANJANJA..sasa kama kijana mpenda maendeleo siwezi kupoteza muda kujadili hoja za makanjanja...FULLSTOP!
 
sugu uwezo wake ni miziki ya kufokafoka na sio siasa, hata hivo sugu kushinda ccm walimpambanisha na mtu aliyekuwa hakubaliki ndani ya ccm yenyewe. Nilisha wahi changia kuwa Sugu uchaguzi ujao hawezi shinda tena, kwani uwezo wake ni mfinyu mno.Maneno aliyoyaongea ni kama tulivosikia na mara baada ya yeye kuchemka Slaa na Mbowe wakaona aibu na mbowe pale pale akasimama na kumkosoa vikari kwa upupu aliouongea,yaani anazidi kujizika yeye mwenyewe.waswahili tunasema mazoea hujenga tabia, sugu alizoea toka akiwa mwana muziki katika majukwaa ni kuimba miziki ya kupaka(kutukana,kujisifu ...) kwahiyo nawashauri viongozi wa chadema watu kama hao musiwape nafasi ya kusimama kwenye majukwaa.

Sio mnakaa huku hamji vinavyotokea mnasema alipambanishwa na mtu dhaifu, we ulipambanishwa na nani?, alishinda kwa kishindo hata kuchakachua ilishindikana kusema hivyo ina maana hata wapizani wote bungeni walikutana na watu dhaifu, Ni hivi nen tupa/piga... mawe haimaanishi kama unavyodhani, wewe uliyejichubua ganda
 
Nimesikia kwenye habari za magazetini asubuhi
hii kwamba mbunge wa mbeya mjini
ame hamasisha wana nchi wa mbeya kwamba
akija kiongozi ambaye hawamtaki,...
au kiongozi yeyote,hata kama "ni raisi" ni haki yao kumkataa
haka kwa kumpiga mawe!

Kama hii ni kweli,basi Dr.Slaa na wazee wengine ndani ya chadema
mna kazi ya kuwafundisha wabunge vijana
jinsi ya kuongea kwenye public na jinsi ya kutembea "normal" ukiwa na uheshimiwa!

Hizi sio kauli za kutolewa na kiongozi yeyote yule,...
kuna watu walio kuwa wanataka kujiunga na chadema,au walio
muunga mkono sugu,..na ambao ni wastaarabu watakua hawaja furahiswa na
kauli hii,...

na hao wataendelea kuamini kuwa chadema wana hamasisha vurugu!

Ombi:
Naomba viongozi wa chadema,walioko huko kwenye maandamano
wakanushe maneno haya (kama sio kweli kwamba sugu haku yatamka)
maana naamini kila alosikia habari hii kasikitishwa sana,...

Viongozi kuzomewa ishara ya umma kuchoka (2)

lC.gif
Joseph Mihangwa​
Juni 3, 2009
rC.jpg


KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya, tulichambua sababu za kuzuka kwa tabia inayozidi kuota mizizi nchini ya kuzomea viongozi. Tuliona sababu kuu ni viongozi hao kushindwa kujihusisha na matatizo ya kimsingi ya wananchi ili kutoa majibu kwa maswali kama: “Kwa vipi utajiri wa nchi unazalishwa, kusimamiwa, kugawiwa na kutumika?
Nani anamiliki uchumi wa nchi na kwa manufaa ya nani? Nini hatima ya wananchi na ya nchi chini ya serikali waliyoiweka madarakani? Je, kuna demokrasia ya kweli kuwezesha sauti ya kila mwananchi kusikika wakati wote bila ubaguzi au upendeleo?
Maswali haya hayakwepeki. Kina [Anne] Kilango wanatumia haki yao hiyo ya kikatiba [kama Wabunge] kwa niaba ya wananchi kutaka majibu, na jinsi kodi ya wananchi inavyotumika.
Na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977, ibara ya 9 [j] ipo upande wa wanaohoji; kwani inaitaka serikali madarakani kuhakikisha kwamba “shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi [kuwekwa] katika mamlaka ya watu wachache binafsi”, ambayo ndiyo hali tulimo sasa, na Viongozi wenye kukumbatia ufisadi wanajifanya kutoliona hilo!
Wanaona ufahari kuona Katiba ya nchi inavunjwa. Na kwa sababu hii, kwa nini wasizomewe huko Busanda? Mbona hawakuwapeleka Busanda wabunge wazito na mawaziri wanaowasakama kina Kilango bungeni?
Kitendo cha waziri kumkemea mbunge bungeni ni kitendo cha kuvunja Katiba ya nchi, na utovu wa nidhamu usiovumilika. Kwa jinsi hii, sauti ya wananchi imezimwa bungeni kwa ubabe na kwa ridhaa ya Spika, huku nchi ikiangamizwa kiuchumi na maharamia ambao sasa wamo mbioni kuliteka Bunge pia baada ya kuteka serikali.
Utakielezeaje, kwa mfano, kitendo cha serikali cha kunyamazia mikataba mibovu ya madini iliyo dhahiri; uporaji wa fedha za malipo ya EPA zaidi ya Sh. bilioni 133, ufujaji wa Sh. bilioni 200 za mfuko wa pembejeo [ICS]; ubinafsishaji/uuzaji wa asasi na mali za umma kwa mizengwe, kama si serikali kutekwa nyara na kundi la ki-mafia?.
Hatukuona sababu, wala mantiki, kwa Spika kumkingia kifua na “kumwokoa” aliyekuwa Waziri wa Madini na Nishati, Nizar Karamagi, kwa mashambulizi ya wabunge kuhusiana na kashfa ya kutia sahihi hotelini [bila serikali kujua], nchini Uingereza, mkataba wa madini wa Buzwagi kinyume na protokali za kiserikali.
Bunge limechukua hatua gani kwa kudanganywa mwaka jana kwamba hapakuwa na biashara haramu ya magogo, lakini baadaye serikali ikakiri kuwapo kwa biashara hiyo? Inakadiriwa kuwa thamani ya uporaji wa magogo hayo kupelekwa nchi za nje ingeweza kujenga zaidi ya madarasa ya sekondari 10,000, kila mwaka.
Serikali ya wananchi imechukua hatua gani, na nini msimamo wa Bunge kwa ujangili huo ili kuhakikishia Bunge la umma halifungwi nira na mafisadi?
Ni aibu kwa taifa kuficha maovu eti kwa hofu kwamba kwa kuchukua hatua thabiti na madhubuti dhidi ya watuhumiwa, ni sawa na kukiumbua Chama na Serikali yake.
Wananchi wa Katoro hawakufurika kumsikiliza Mama Anne Kilango akizungumzia juu ya sera za Chama, bali walikwenda kumsikiliza anasemaje kuhusu Chama kukumbatia ufisadi na mafisadi.
Na yeye alilielewa hilo. Ndiyo maana alianza kwa kujihami asijechafua sifa yake, kwa kusema: “CCM si wote ambao ni mafisadi, bali ni watu wachache binafsi walioko ndani ya Chama”.
Na kwa nini CCM kinaendelea kuwakumbatia hao wachache, wanaohatarisha amani na mustakabali wa Taifa, kama si kweli kwamba kimetekwa nyara na mafisadi hao? Na kwa nini tusiamini vivyo hivyo kwa Bunge linaponyamazia uozo huo?
Hebu shuhudia kile tunachokisema hapa chini:
Alipochaguliwa kushika cheo cha spika miaka mitatu iliyopita, Mheshimiwa Samwel Sitta aliwaahidi Watanzania kuwa angetekeleza kazi zake kwa “Standards and Speed” - Kiwango na Kasi. Akawaonya na kuwatahadharisha mawaziri juu ya mtindo uliozoeleka wa kutoa majibu dhaifu kwa hoja za wabunge bungeni, kwa kuelewa kwamba mawaziri wanawajibika kwa Bunge, na hivyo kwa wananchi.
Bila shaka Sitta alikuwa anarejea sifa ya Bunge makini la enzi za uhuru, linaloelezewa na Bwana C. Pratt, katika kitabu “Socialism in Tanzania” (uk. 226) kwamba “lilikuwa bunge la watu; mawaziri wa serikali hawakuruhusiwa kujifanya hawanazo, wala kufanya mzaha katika kuandaa na kutoa majibu [sahihi] kwa hoja za wabunge; waliwajibika ipasavyo na kikamilifu kwa Bunge na kwa Taifa kuhusu sera kuu za Serikali”.
Ukweli huu umethibitishwa pia na Mheshimiwa Pius Msekwa, katika kitabu chake, “Towards Party Supremacy in Tanzania”. Lakini, pamoja na maspika Msekwa na Sitta kuthibitisha ukweli huo, ni hao hao wamekuwa sehemu ya mfumo kandamizi wa Bunge. Kulikoni? Nini kinawasumbua? Ni u-chama au usaliti kwa umma?
Ukimwondoa Sitta ambaye “Standards and Speed” zake zinayumba na kuwakwaza kina Kilango, Msekwa naye hakufanya vizuri katika kulinda na kutetea ukuu wa Bunge [Parliamentary Supremacy] dhidi ya ubabe wa chama na Serikali.
Mfano, mwezi April 2002, Ofisi ya Rais Benjamin William Mkapa ilitangaza na kutekeleza mpango wa kuhamia Dodoma kila Bunge lilipokaa hapo kwa maelezo kwamba ilikuwa ni “kurahisisha utendaji wa kazi zake wakati Bunge likiendelea”.
Wahenga walisema, “fumbo mfumbie mjinga”. Watu walielewa mara moja kuwa, hatua hiyo haikulenga kingine bali ilikuwa ni kuwadhibiti kwa karibu na papo kwa papo wabunge “wakorofi” [kama kina Kilango] wenye tabia ya kuihoji au kuiweka kiti moto serikali bungeni.
Ubashiri huu ulithibitika kuwa ukweli, pale Rais Mkapa alipowaita na kuwakemea baadhi ya wabunge wa CCM, kwa hoja zao kali bungeni, akawaamuru waache tabia ya “kulipua mabomu dhidi ya Serikali”, na kutishia kwamba Serikali nayo ilikuwa na mabomu yake dhidi ya wabunge hao. Akaonya kuwa, yeye kama Mwenyekiti wa Chama tawala asingeridhia wabunge hao kuteuliwa kugombea ubunge tena mwaka 2005, kama wataendeleza ukorofi huo.
Rais alikwenda mbali zaidi kwa kuwaagiza wabunge wote kuacha chuki dhidi ya wawekezaji wa Afrika Kusini [ununuzi wa NBC, Menejimenti ya TANESCO], na akawataka kufunga mdomo juu ya uuzaji wa nyumba za Serikali, Mashirika ya Umma na Mikataba ya uwekezaji kwa ujumla, wakati akielewa fika matakwa ya Katiba [ibara ya 9j] juu ya usimamizi wa uchumi wa nchi, kama tulivyoyanukuu hapo juu.
Na kwa nini wabunge wakubali kirahisi kutishwa na kusalimu amri kwa mhimili wa utawala, kama si kununuliwa kwa njama za kuua demokrasia, jambo ambalo Kilango na wenzake wanalipiga vita?
Kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha sheria ya kinga za kibunge [Parliamentary Immunities Act] ya mwaka 1988, uhuru wa hotuba na majadiliano ya wabunge bungeni hayawezi kuhojiwa katika Mahakama yoyote, au chombo na mahali popote nje ya Bunge.
Uhuru huu ni wa Kikatiba pia, na umefafanuliwa vizuri kwenye ibara ya 100 ya Katiba yetu kwamba, “Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge, na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge”.
Ibara hii ya Katiba ni kivuli cha ibara ya 3 ya Sheria kama hiyo ya Uingereza [English Bill of Rights] ya mwaka 1688 tuliyoridhia, kwa maana kwamba kinga waliyo nayo wabunge wa Uingereza ndiyo kinga waliyo nayo wabunge wetu; lakini hatusikii vituko kama vya hapa kwetu huko Uingereza juu ya kubaka na kusigina Katiba, demokrasia na utawala bora.
Pamoja na kauli mbiu yake butu ya “Uwazi na Ukweli”, na kitendo cha kuwatisha wabunge wa CCM ili wamsujudie, Mkapa alijua dhahiri kuwa alikuwa anavunja Katiba ya nchi; na huo ni ujambazi wa kisiasa unaopaswa kukoma ili demokrasia ishamiri.
Kwa kuling’oa Bunge meno, Mkapa alifungua mlango kwa ufisadi nchini, ukatamba bila hofu ya kuhojiwa. Lakini kama angezingatia dhana ya mgawanyo wa madaraka, nchi yetu isingegubikwa na maovu kama ubinafsishaji usiojali [NBC, ATC, Williamson Diamonds, Viwanda mbali mbali]; uporaji wa mali za umma [EPA, ICS], Mikataba ya kifisadi, IPTL, Richmond, Buzwagi, TICTS], ununuzi uliosheheni rushwa wa ndege ya Rais, Rada na ufisadi mwingine ambao umeitupa nchi yetu katika umasikini wa kutupwa.
Majuto ya Mkapa hivi karibuni kwamba Serikali yake “ilifanya makosa makubwa kwa kuingia mikataba isiyojali bila kujua kwanza uhalisi wa faida ambayo nchi ingepata”, hayatusaidii kwa kuwa alikwishalijeruhi taifa, lakini itoshe tu kwamba hili liwe fundisho sasa kwa watawala madarakani.
Na kwa sababu hii, wasishangae, na wakubali kuzomewa na umma wanapoutonesha vidonda. Hayo yaliyowafika baadhi ya Viongozi wetu kwenye kampeni za Busanda yataendelea kutokea kama hawatabadili mitizamo yao kwa kuweka mbele maslahi ya walio wengi.
hs3.gif



Viongozi kuzomewa ishara ya umma kuchoka (2)
 
Acha wivu wa kike wewe... Sugu alipata kura 48,000 na kumuacha mpinzani wake kwa kura 27,000. Sio ushindi wa kubeza hata kidogo na hapo uchakachuaji
ulifanyika. Kura za sugu ni nyingi <br />
kuliko za wabunge wote wa CCM Zanzibar
ukizijumlisha kwa hiyo sio wa kubahatisha kama akili yako mbovu inavyokudanganya. Suala la kuelezea hisia halizingatii kuwa watu kama wewe watafurahia au la, kama kiongozi hamumpendi mzomeeni tu, na hao viongozi tusiowataka wakija Mbeya tunawazomea vilevile. Mbona hata Slaa alizomewa na mujahidina pale Tabora, kwani kuna mtu alilalamika? Watu walikuwa wanatoa hisia zao za kiislam
&lt;br /&gt;<br />
<br />

Acha ubaguzi na pumba zako za kidini.Zingatia hoja na utoe comment zenye mashiko na sio kurukaruka kama changudoa.Usiweke ushabiki ata kwenye vitu vya kipuuzi.MR. II ni kijana wa mtaani kwa maana ya purukushani zisizo na nidhamu,mbali na kupata ubunge kibahati lakini pia hajajiandaa kukaa kiuongozi zaidi ya kufikiri siasa ni kama rap zake za sugu.Tufikie maana tuseme ukweli juu ya tabia za aibu za huyu na wala si kushabikia na kutoa mifano ya mbona.........na.......sijui tabora....waislam.
 
Nilisema kwenye thread zilizotangulia kuwa elimu na profile ya Sugu ni ZERO hivyo jimbo liko wazi mpaka 2015 lakini wachangiaji wenye uelewa mdogo wakanibeza. Ujumbe wangu kwa CDM ni kwamba wanahitaji kumpolish Sugu aondokane na kuropoka ki-hiphop kwa ajili ya faida ya chama. Sasa angalia huo utumbo anaoutapika mbele ya waliomchagua
Pumba hz. Huwezi kujilinganisha na sugu wewe.
 
siwezi kuchangia topic ya kijinga hivi , mimi niko mbeya na nilikuwepo kwenye huo mkutano na napenda kuwakikishia kuwa Sugu hajasema hayo bali yamebuniwa na waandishi fulanifulani wa
chama fulani kwa malengo fulani , Sugu mwenyewe watu wa namna hiyo anawaita...MAKANJANJA..sasa kama kijana mpenda maendeleo siwezi kupoteza muda kujadili hoja za makanjanja...FULLSTOP!
<br />


Mbona mnafiki wewe!Wenzio wanakili kutamkwa maneno hayo na kisha Mbowe kuyavunja ukali.Sasa wewe ulikuwa ukihusudu maandamano tu na kushindwa kusikiliza hotuba za viongozi wako akina Sugu!!!!!!
 
Back
Top Bottom