Ni kweli ndoa ya Clouds Fm na CCM ishafungwa?

Wakuu nimegutushwa jambo hapa hivi kweli mshahara wa 315000 mara wafanyakazi 350000 kwa miezi 12 ni trillion 6? Au rais kutusanii kama ilivyo kawaida yake?


315,000 x 350000 =110,250,000,000.00 x 12=1,323,000,000,000.00

6trillion maana yake ni Tsh 6,000,000,000.00
Kuna Balance ya Tsh 5,000,000,000.00
Balance analipia safari za ndege kwenda kutembelea nchi za ulaya kutafuta wawekezaji.
Haya ni mawazo yangu tu.
 
Ruge na Kusaga wana Akili kuliko Mkwere na timu yake pale IKULU, hawa jamaa wanaexposure nzuri na wanajua jinsi ya kutafuta hela hasa kwa mtu mwenye upeo mdogo wa kufikiria

hawa jamaa RUGE na KUsaga pamoja na wapambe wao (gardener na KIbonde), walimbeba jamaa (JK) mpaka leaders club ili akauze sura huku wao wakipiga hela kwenye kampeni ile ya ZINDUKA, hapa ni kama kulipa fadhira tu kwa jamaa na jamaa asivyokuwa makini anaona kampeni zake zinaenda vizuri

mimi nina wasiwasi na uwezo wa jamaa upstair kama mchumi, hivi kweli mchumi mwenye degree unaweza kuletewa figure za uongo za fani (proffessional) yako na ukashindwa ku analyse kweli? inakuwaje raisi upewe makaratasi na kuambiwa nenda kasome na wewe unaenda kusoma kama ROBOT bila kuipitia kwanza, raisi gani mwenye visasi na asiyawapenda wananchi wake?, sasa mambo ya kunyimwa kura katika uchaguzi wa mwezi wa kumi unayazungumziaje leo? ANA UHAKIKA GANI KUWA NEC (CCM)WATAMPITISHA?

INAUMA WAUNGWANA
SAA YA UKOMBOZI NI SASA

"TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMENYONYWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA. UNYONGE WETU NDIO ULIOTUFANYA TUONEWE, TUNYONYWE NA TUPUUZWE, SASA TUNATAKA MAPINDUZI, MAPINDUZI YATAKAYO TUFANYA TUSIONEWE, TUSINYONYWE NA TUSIPUUZWE" (JK Nyerere, Azimio la Arusha 1967)
 
315,000 x 350000 =110,250,000,000.00 x 12=1,323,000,000,000.00 6trillion maana yake ni Tsh 6,000,000,000.00 Kuna Balance ya Tsh 5,000,000,000.00 Balance analipia safari za ndege kwenda kutembelea nchi za ulaya kutafuta wawekezaji. Haya ni mawazo yangu tu.

No kwa hili mtakeni radhi. Kwani kabla ya hii 315,000 wafanyakazi walikuwa hawalipwi mishahara? Ukiongeza kufikia kiwango hicho wale wengine nao wataongezwa kutofautisha madaraja. Tafuta previous salaries, i think ni trillion kadhaa kisha kutakuwa na ongezeko la hii ya sasa.
 
Hao waongozaji wa jahazi waongezeni katika kundi la 'wazee wa dsm'.
 
Si unajua kuna ubunge wa viti maalum kwa wanawake? Labda watangazaji wanawania!
 
Clouds imefikia wakati nadhani wamejisahau. Ni kweli wanaburudisha ila sasa wamepitiliza hadi wanakosa mwelekeo. Ni jana tu nimesoma gazeti moja Kipindi cha LEO tena kimeburuzwa mahakamani na Advocate mmoja anadai Dina Marios na Gea Habib walimhoji mke wake kwa kumhusisha na tuhuma zisizo za kweli!

Sasa na JAHAZI nao vilevile, sijui wanania gani!!!!!?????
 
Hakika Clouds wamepotoka. Nakubaliana na wachambuzi wenye bongo zinazofanya uchambuzi wa kina na wa kisayansi kuwa Radio Clouds ni ya kubeza, haina jipya na hawawezi kumbadili mfanyakazi anaeelewa maana ya future yake ni nini. Chama cha wafanyakazi kama TUCTA duniani pote ndivyo kinavyofanya kazi. Uelewa wa kina Kibonde ni wa kitoto hawana elimu ya kuchambua masuala kwa undani. Wanajifanya watoto wa mjini lakini wanatoa PUMBA sana.

kibonge poyoyo yule,hana lolote analojua, jamaa mnafiki yule mi najiuliza sijui anaishije na mke wake wallah!! gadna ni toto la mama lisilojua chochote...watoto wa mjini watakuwa wale viazi tuu!!kibonde sijui kaanza kupanda ndege juzi juzi yule maake anavosimuliaga i mean ataingizia stori ya kupanda ndege hata pasipotakikana kufanya hivyo..machizi wotee!!
 
Uzuri ni kuwa watanzania wanaona na wameanza kuelewa. Inawezekana waendeshaji wa kipindi cha jahazi wana akili nyingi sana ndio maana wanaweza kusema lolote wanalojisikia kusema.
Kazi ipo maana kila kitu kina mwisho bwana.Mtu akijisahau ni rahisi kuanguka. Kwenye recession iliyopita kuna kampuni iliishi miaka zaidi ya mia moja na ikadondoka kifo cha mende. Clouds wakijisahau tutawaona mbele ya safari wamepumzikia wapi!!
 
Ndoa ilikwisha fungwa toka enzi ya uhai wa marehemu Amina Chifupa. Halafu hiyo hesabu nafikiri atakuwa amesaidiwa na mwenyekiti wa WAMA Foundation.
 
Ukitizama kwa uhakika na kwa umakini juu ya mambo yanayofanywa na Clouds/ Primetiem na watangazaji wao wa aina ya Kibonde utagundua mambo kadhaa yatakayokufanya ujiulize kama una akili timamu
1. Clouds waliaandaa tamasha la kukataa malaria rais akaalikwa na kiingilio kikatozwa ilhali tamasha lile lilidhamini kwa asilimia zote, sababu za malipo walizotoa ni kuwa ulinzi kwa rais. Hapa hatuongelei kuhusu suala la Mr II kudhulumiwa na kina Ruge
2 Asilimia kubwa ya watangazaji wa redio hii ni wasemaji wa maneno tu, ninawajua watangazaji ambao hawana elimu kubwa sana lakini ipindi vyao vina maana sana na vinavutia kusikiliza ama kutazama, tazama tbc na hasa asubuhi, pale pana vitu vizuri
Kibonde ni mganga njaa mkubwa anayetumika na kutumiwa kwa maana yake


FONT=Century Gothic]AKILI SAFI HAIPIMWI NA TBS[/FONT]

UNDERLINE, Mwisho wake unakalibia
 
mimi binafsi mpaka leo uwa sijui hii redio clouds uwa ni ya nani,yaani wafanyakazi uwa wanajilopokea wanavyoona wao hawana ethics za kiutangazaji.sina uhakika kama wana training yeyote kwa kazi wanayoifanya.kuna wakati wanatamka maneno kama watoto wako karibu unazima redio.maneno machafu bila kuwa na aibu.nadhani mwisho wao umefika wanajichimbia kaburi.
 
Jamani huyu Mkwere hata hesabu zinamshindinda. Ukiwalipa wafanyakazi 350,000 Tshs 315,000@mwezi kwa mwaka ni sawa na:

350,000*315,000*12=1,323,000,000,000 sasa hiyo Tsh 6trillion aliyoitaja inatoka wapi?

mimi nadhani huyu bwana ni kilaza na mwongo mkubwa. Kazi yake kusoma taarifa bila kuzifanyia uchambuzi. Aibu tupu!

Ndugu yangu WASP pamoja na wengine, nadhani kuna point mmeiacha mahali fulani. Kuzidisha hicho kima cha chini mara idadi ya wafanyakazi sio sahihi. Kumbukeni, tunaposema kima cha chini ni 315,000/= maana yake kuna wengine wanaolipwa kima cha kati na wengine kima cha juu. Sasa fikiria huyu wa 104,000/= akiongezewa ili mshahara wake ufikie 315,000/= Je yule wa kima cha juu, ambaye kwa mfano mshahara wake wa sasa ni 4M au 9M atafikia wapi. Ukishapata mishahara hiyo yote mipya kulingana na kima cha kila mmoja, ndipo ujumlishe hiyo mishahara yote. Labda ndiyo hesabu alizotumia. Japo kwasababu hatujuai hiyo mishahara mingine bado hatuwezi kuridhika na maelezo ya JK maana hatuwezi kuthibitisha.
 
ndugu yangu wasp pamoja na wengine, nadhani kuna point mmeiacha mahali fulani. Kuzidisha hicho kima cha chini mara idadi ya wafanyakazi sio sahihi. Kumbukeni, tunaposema kima cha chini ni 315,000/= maana yake kuna wengine wanaolipwa kima cha kati na wengine kima cha juu. Sasa fikiria huyu wa 104,000/= akiongezewa ili mshahara wake ufikie 315,000/= je yule wa kima cha juu, ambaye kwa mfano mshahara wake wa sasa ni 4m au 9m atafikia wapi. Ukishapata mishahara hiyo yote mipya kulingana na kima cha kila mmoja, ndipo ujumlishe hiyo mishahara yote. Labda ndiyo hesabu alizotumia. Japo kwasababu hatujuai hiyo mishahara mingine bado hatuwezi kuridhika na maelezo ya jk maana hatuwezi kuthibitisha.

mkuu, nadhani madai ya wafanyakazi ni kuongezeka kwa kima cha chini hadi kufikia laki 3 na buku kumi na tano, na si kwamba wote waongezewe hapana, kwa nilivoelewa mm, na wote mr. President na baadhi ya wachangiaji humu wamepotoka, huwezi zidisha laki tatu na kumi na tano mara laki tatu na hamsini idadui ya wafanyakazi kwa sababu sio wote wanapokea kiasi hicho, unless mwere alimaanisha kuwa idadi ya wafanyakazi 350,000 ndo wanaopokea kima cha chini...tunazungumzia kima cha chini hapa na si cha kati na cha juu, lets be realistic hapo..
 
Hao watangazaji ni njaa tu na pia elimu hakuna pale.
Hao watangazaji wana wake/waume zao majumbani? Watoto je, wanao? Maana huenda hawajakabwa na majukumu ya kifamilia ndo maana wanaona mishahara inatosha!
 
Clouds ni taswira ya mabogus mengi yaliyojaa nchini yanayojifanya ni mataalamu ya kuset trend ya mwelekeo wa hali ilhali wao wenyewe wako gizani totoro. Hakuna msomi kati yao wale wanapaswa kuelimishwa hata kama hawataki elimu.
 
Back
Top Bottom