BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa vipindi vya Radio, utagundua kuwa kuanzia saa 12 asubuhi kipindi cha Good Morning kutoka Wasafi FM kinasikilizwa sana mitaani, kwenye madaladala, magari binafsi kuliko ilivyo Power Breakfast ya Clouds FM. Nimeshindwa kuelewa tatizo ni nini kwa Clouds kupoteza usikilizwaji kiasi hiko.
Kipindi cha Good Morning kinafanywa na Salma Dakota, David Rwenyagira, Oscar Kawau, Zungu, Charles William na Babu Zembwela wakati Power Breakfast inaanza na Matei, Khan then wanafuata Fatma (DJ Fetty), Masoud Kipanya, Ceazer, Sasali na Bonge. Tangu kuondoka kwa Gerald Hando ni kama hawajawahi kukaa sawa, bado wakamuondoa Barbara Hassan kumpeleka kwenye TV ndio kabisaaa.
Kwa kiasi kikubwa Clouds kwasasa inabebwa na Leo Tena, Amplifaya na Jahazi, ila PB, XXL, Sports Extra, Ala za Roho vyote vinakufa taratibu.