Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,138
- 12,590
Binafsi sipingi suala la baba kujitoa kuhudumia familia lakini napinga huu mtindo wa maisha wa vijana wa sasa tena hata kabla hawajaingia katika ndoa.Nafikiri hakuna shida sana kwa walio katika ndoa mwanaume kuhudumia kila kitu kwa sababu huo ndio umekuwa utaratibu wa karibia binadamu wote kwa mke na mume. Tatizo ni kwa watu waliokutana tu hata hawajamaliza mwezi kuanza kubebeshwa majukumu ya mume au baba mzazi kwa mwendokasi.
Ubinafsi wa jinsia ya kike kwa mwenza wake unakua kwa kasi sana hasa katika kipato na mali na tabia hii inaonekana ya kawaida tu wala haina tatizo hata kwa wanaume.
Binafsi sipendezwi na ubinafsi wa jinsia ya kike iwe katika uchumba hata katika ndoa tena hasara zaidi ubinafsi ukiwepo hata katika ndoa. Ndoa hiyo itakuwa imeshikiliwa na uzi mwembamba wa fedha za mwanaume siku account ya mwanaume ikikata au kipato kuyumba au ujira kupotea hakutakuwa na uhai wa hiyo ndoa tena.
Hizi tabia ulizo andika hapa ndizo hizo tabia zinazo zalisha ubinafsi wa kimali wa jinsia ya kike mpaka kukomaa ndani ya ndoa.
Leo hii vijana wanaona sio ajabu mwanamke mwenye kipato kikubwa kabisa cha kueleweka kushindwa kujihudumia mahitaji yake ya msingi na kutegemea fedha za mwanaume wake hata zile kidogo unabaki kujiuliza pesa yake mwanamke wa kileo inafanya kazi gani ?
Mama zetu walishindwa kuwa na mchango mkubwa wa kifedha katika familia kutokana na kuwa mama wa majumbani ila katika shughuli ndogo ndogo walizokuwa wakifanya hata za kuuza nyanya pesa ndogo walizopata wali wasaidia wazee wetu hata madaftari madogo wali tununulia na hakuna mahali walilalamika na kuona baba zetu hawatimizi wajibu wao ila kwa hawa wanawake wa kileo kama sio kutangazwa mtaa mzima basi hiyo ndoa inayumba.
Unajiuliza kwa nini wanaume wa kisiasa wanafagilia ubinafsi wa mwanamke ambao ni hatari kwao na kwa ndoa yao ? Unashindwa kuelewa akili zao.
Mwanamke ombaomba kiasili ni mbinafsi aliye pindukia ambae chake kibaki kuwa chake pasipo kufahamu kinafanya nini wala kinaenda wapi ila chako kiwe chake huu ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni hatari kwa ustawi wa ndoa