Ni kweli mabinti wa Tanzania ni omba omba sana katika mahusiano au wanaume ndio mabahili?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,660
46,325
Kumekuwepo na malalamiko mengi pamoja na mijadala mingi sana ya wanaume wa bongo wakilalamika kuombwa pesa au kuhudumia kila kitu kwa wanawake wanaoingia nao kwenye mahusiano hata kabla ya ndoa(girlfriends)

Wengi wanalalamika kwamba ndani ya siku au wiki tu za kuinguia kwenye mahusiano mabinti hugeuka kama yatima au kuwageuza wao kama wazazi wao wakiomba huduma za kila kitu kuanzia kodi, gesi, luku, chakula, kusuka nywele n.k

Je malalamiko au madai haya ni ya kweli na kama ni kweli yanasababushwa na nini hasa? Ni ishara ya umasikini wa wabongo au tabia mbaya tu za baadhi ya mabinti kupenda kitonga bila ulazima?

Je hii tabia ni kwa mabinti wa mjini au hata huko vijijini hali ni hivyo?
 
Tunaishi kwenye jamii zenye tamaduni ya kumfanya mwanaume, baba, kama kichwa cha familia, provider na mbeba majukumu yote ya kiuchumi, jamii zetu za kiafrica zimeishi hivyo toka karne na karne hivyo mwanaume automatically anatakiwa kuhakikisha familia yake, mpenzi wake, na wanaomzunguka wanapata mahitaji muhimu, sina tatizo katika hilo kama mwanamke, binti na familia watakubali kuishi kutokana na kipato cha muhusika.

Shida iliyopo katika zama na kizazi hiki cha utandawazi, mabinti wamejawa tamaa ya vitu wasivo navyo wala kuwa na uwezo navyo, wanaona kupitia social medias jinsi wenzao wanavyokuwa spoiled na material things, simu nzuri, fancy dates n.k tamaa huwaingia na kuona aliyenae hana maana hasa anaposhindwa kupata vile anavyoona kwa wenzake, mbaya zaidi binti akiwa na muonekano wenye kuvutia wanaume wenye uwezo wao basi haoni sababu kuendelea na wewe unga unga, hohehae, kajamba nani, kwangu pakavu tia mchuzi, ata kuacha na ukwale wako na njaa zako na kwenda kwa wenye maisha safi ambao nao siku hizi wanajua ugonjwa wa wanawake wa mujini, atakununulia macho matatu na yeye atakuomba jicho moja atakuharibu kinyeo, atakupeleka vacation dubai, zanzibar, akishajiridhisha amekutumia kisawa sawa basi anakudump na kuendela na circle ya kuchakata warembo wengine, na wewe unaangukia kwa pedeshee mwingine wa mujini and the loop is infinity.
 
Hii ni tabia inayokua kwa kasi kipindi hiki, nawaonea huruma sana vijana wa kileo kwa kulea tabia hii hata kwa wanawake wenye vipato. ndoa zao zimeshikiliwa na uzi mwembamba nao ni kipato cha uhakika cha mwanaume.
Nafikiri hakuna shida sana kwa walio katika ndoa mwanaume kuhudumia kila kitu kwa sababu huo ndio umekuwa utaratibu wa karibia binadamu wote kwa mke na mume. Tatizo ni kwa watu waliokutana tu hata hawajamaliza mwezi kuanza kubebeshwa majukumu ya mume au baba mzazi kwa mwendokasi.
 
Tunaishi kwenye jamii zenye tamaduni ya kumfanya mwanaume, baba, kama kichwa cha familia, provider na mbeba majukumu yote ya kiuchumi, jamii zetu za kiafrica zimeishi hivyo toka karne na karne hivyo mwanaume automatically anatakiwa kuhakikisha familia yake, mpenzi wake,
Mkuu ni sawa mwanaume kumplia ada ya chuo, kodi na mahitaji mengine mengi mpenzi tu ambaye wanaweza kuachana hata kwa meseji muda wowote??
 
Back
Top Bottom