Ni kweli kuwa watu wote walioko kwenye ndoa au waliooana wanapendana?

Si kweli WOS wengine waliingia kwenye ndoa kwa sababu ya fashions na wao waonekane wanandoa :A S-rose:
Wengine waliingia kwenye ndoa kwa kujilazimisha
Wengine walibeba mimba ikawalazimu kuingia kwenye ndoa
Wengine wamefata pesa au mali ndani ya ndoa
Wengine wanajiegesha jua litulie kisha waendelee na safari
Wengine wapo kwa ajili ya heshima ya wazazi.
wengine ni kweli wanapendana..:A S-rose:
NK. Nk.
very true mamito, but waliopendana kiukweli hadi wakafunga hizo pingu za maisha ni wachache, na nafikiri ni bahati ila ukimshirikisha Mungu, na kuwa mwaminifu ktk amri zake kwa kumaanisha, waweza kuwa katika kundi la wenye bahati, otherwise kama ushabugi step u have to carry your burnens & sorrows.
 
walioolewa/oa na ambao bado wote tuna heshima kwenye jamii/wazee wetu.....cku hizi vwengi waliopo kwenye ndoa ndio wamepoteza hiyo heshima kwenye jamii na mifano hai ninayo....kwingine tupo sambamba.

nyamayao kuna jamii na jamii ..........
jamii ya kwetu kama hujaolewa hata uwe na miaka 50 bado unaonekana mtoto.............hutapewa majukumu ya kijamii na mtoto mdogo wa miaka 18 kama kaolewa atapewa yeye majukumu.

wazee pia katika jamii zetu wanaridhika zaidi kama umeolewa ( that is the reality........maybe sio reality tunayoipenda lakini hali iko hivyo)
 
We mdanganye mwenzio tu....

Hamna mtu namwamini kama NYAMAYAO humu jf! Sijawahi kuona unafiki kwenye post zake(i feel that way)She always call a spade a spade,not a big spoon.
(Sore mchumba,wewe nakuamini 0.10%)Nisamehe kama nimekukwaza.
 
Je, kuna umuhimu wa wapenzi kukaa pamoja (under one roof) kwa muda fulani, say, mwaka mmoja au miwili kabla ya kufunga ndoa, ili waweze kufahamiana tabia zao?

Labda kama kukaa huko hakuta involve tendo la ndoa!

Tatizo kubwa watu wanataka kuoa/olewa na malaika wakati wao wenyewe sio malaika. Mara nyingi tunaona matatizo ya wenza wetu na kushindwa kuona yetu. Na ndio maana ukisikiliza migogoro mingi katika ndoa, kila mmoja anamnyooshea mwenzake kidole. Na mara kadhaa kwa kukosa maarifa tunapambana na dalili za matatizo badala ya kupambana na tatizo lenyewe na mwisho wa siku tunaishia kulalamika tu "huyu mtu habadiliki!" na pengine ndoa zinavunjika.
 
nguli wengine tumeshatosa sababu lakini jopo limezipinga na kusema sababu ni mahitaji ya kiwiliwili tu! kazi kweli kweli
 
nyamayao kuna jamii na jamii ..........
jamii ya kwetu kama hujaolewa hata uwe na miaka 50 bado unaonekana mtoto.............hutapewa majukumu ya kijamii na mtoto mdogo wa miaka 18 kama kaolewa atapewa yeye majukumu.

wazee pia katika jamii zetu wanaridhika zaidi kama umeolewa ( that is the reality........maybe sio reality tunayoipenda lakini hali iko hivyo)
Kwa hiyo umeolewa ili uiridhishe jamii?
 
Labda kama kukaa huko hakuta involve tendo la ndoa!

Tatizo kubwa watu wanataka kuoa/olewa na malaika wakati wao wenyewe sio malaika. Mara nyingi tunaona matatizo ya wenza wetu na kushindwa kuona yetu. Na ndio maana ukisikiliza migogoro mingi katika ndoa, kila mmoja anamnyooshea mwenzake kidole. Na mara kadhaa kwa kukosa maarifa tunapambana na dalili za matatizo badala ya kupambana na tatizo lenyewe na mwisho wa siku tunaishia kulalamika tu "huyu mtu habadiliki!" na pengine ndoa zinavunjika.

halafu mie naona mwanamke anaeangalia mbele hawezi kwenda tu kuishi na mwanaume ili mradi, na hapo blu baadhi ya wanawake wenye kufikiria leo tu ndio kwanza atabeba mimba ili jamaa awahi kuhalalisha mambo....wadada mcje kufanya kitendo cha kuhamia kwa mwanaume ki reja reja tu hivyo.
 
Hamna mtu namwamini kama NYAMAYAO humu jf! Sijawahi kuona unafiki kwenye post zake(i feel that way)She always call a spade a spade,not a big spoon.
(Sore mchumba,wewe nakuamini 0.10%)Nisamehe kama nimekukwaza.
Hahahahaha! Haya bana, ila kitafika kipindi utagundua huu upupu naouandika huku kimasihara kuwa ni UKWELI tena UKWELI MTUPU. Time will tell.
 
Naomba utueleze mfano wa hizi tabia ambazo sio rahisi kuzijua kabla ya kuoana..........

Japo swali halijaelekezwa kwangu, lakini naomba nitoe mifano kwa ufahamu wangu.

1. Uaminifu - kama wapenzi wanakutana kwa appointment tu; mtu ambaye siyo mwaminifu anaweza kuhakikisha hagoganishi magari.

2. Uchafu - kuna wavulana siku akiwa anatembelewa na mpenzi wake ndipo ataweka nyumba soap soap na kuiweka ikiwa more organized, subiri uje umvamie siku moja bila taarifa inaweza kuwa aibu. Pia wapo wasichana ambao siku akiwa na date na bf wake ndipo anajiweka soap soap na anakuwa na kufuli special za kuendea kwenye hizo date, ukimvamia nyumbani unakuta kalunda vikufuli havijafuliwa wiki nzima, na hata kitanda kinaweza kuwa hakijatandikwa kwa wiki nzima.

3. Kupika - msichana kila mkipanga date anakupa/anaomba offer ya kula nje, huwezi jua kama anaweza kupika au la. Na kwa kuwa mapenzi yako fire fire wala mwanaume hawezi kushituka kulazimisha kwamba anataka kula chakula kilichopikwa na mpenziwe. Na kama msichana ni mtoto wa geti kali, ukianza kumwambia kupika unahisi mtapoteza muda zaidi badala ya kuendelea na yale mambo mengine ya chumbani ama kukaa pamoja mkipiga stori.

4. Ulevi - nina mfano hai. Nina cousin wangu (msichana) alikuwa anakunywa pombe kama hana akili nzuri lakini mchumba wake alikuwa hajui na mpaka wakaja kufunga ndoa. After 3 yrs ndio mume anakuja kugundua kwamba mkewe anakunywa pombe.

Lakini kasoro zote hizo inategemeana sana na closeness iliyopo kati ya wahusika, je wanatembeleana mara kwa mara? Pia distance iliyopo kati ya wahusika, siyo mmoja yuko Dodoma na mwingine yuko Dar hapo ndio hasara kabisa maana ukiwa unaenda kumtembelea lazima utoe taarifa ili ku-avoid kukutana na kufuli mlangoni.

Pia wahusika wanatakiwa kuwa huru, waweze kutembeleana any time hata bila miadi. Lakini kama msichana anaishi kwa wazazi ama walezi nafasi hiyo inakuwa ngumu na matokeo yake ni maumivu.
 
Shauri yako! mchagua sana nazi hupata koroma.kwani wewe malaika? Utaendelea kuchagua mkapa Yesu anarudi

tatizo cku hizi ni mpaka wakaka wapate cjui mdada mwenye kukaribia kurusha ndege, cjui manager mahali, mtoto wa mjini anaejua viwanja vyote, ndio mana ndoa zipo zipo tu, hawataki wadada descent wanataka hao machakaramu anaemkuta na kila kitu na kazi ya mcmamo hana na hujiulizi amewezaje miliki vitu hivi kwa shughuli ndogo aliyonayo.
 
Kwa hiyo umeolewa ili uiridhishe jamii?

nilitoa orodha ya sababu ................kwa kuwa siwezi kusema kuwa nimeolewa kutokana na mapenzi tu au mahitaji ya mwili tu. Hapana wanawake wengi na mimi nikiwa mmoja wapo wanafikia kuolewa kwa mchanganyiko wa sababu kadhaa.

mtu anaweza kutaka kuridhisha jamii/ au wazee lakini akasubiri mpaka apate na mtu anaempenda ndio aridhe hiyo jamii ( kuridhika yeye binafsi kipaumbele zaidi)

au nikiiweka kwa maneno mengine ni kuwa unapotizama pros za ndoa ( hapa nitazungumzia wasichane wa jamii nitokayo mimi)............unahisabu na kuridhisha wazee na jamii pia
 
Hahahahaha! Haya bana, ila kitafika kipindi utagundua huu upupu naouandika huku kimasihara kuwa ni UKWELI tena UKWELI MTUPU. Time will tell.

Hapo kwenye blue sikuwa nimeona kitu, wewe umeonaje au umeongeza mwenyewe??

Kuna mambo watu wanaandika hapa lakini ukweli uko pale pale,... ni vigumu kujihakikishia kuwa huyu mtu ndo Mr au Mrs right wangu. Kuna element kubwa sana ya kamari katika ndoa. Wale wanaoishia kuliwa na kuumia basi tuwafariji na kuwapa pole.
 
nilitoa orodha ya sababu ................kwa kuwa siwezi kusema kuwa nimeolewa kutokana na mapenzi tu au mahitaji ya mwili tu. Hapana wanawake wengi na mimi nikiwa mmoja wapo wanafikia kuolewa kwa mchanganyiko wa sababu kadhaa.

mtu anaweza kutaka kuridhisha jamii/ au wazee lakini akasubiri mpaka apate na mtu anaempenda ndio aridhe hiyo jamii ( kuridhika yeye binafsi kipaumbele zaidi)

au nikiiweka kwa maneno mengine ni kuwa unapotizama pros za ndoa ( hapa nitazungumzia wasichane wa jamii nitokayo mimi)............unahisabu na kuridhisha wazee na jamii pia
Ama kweli ndio maana ndoa nyingi siku hizi huwa hazidumu.

Kwangu Mimi ndoa ni taasisi inayojitegemea. Isiyofungamana na upande wowote. Yenye maamuzi yake yenyewe. Yenye menejimenti yake yenyewe.
 
chrispin ...........wanawake hata wakisema wanakupenda jua hiyo si sababu pekee ya kukubali/kutaka kuolewa na wewe

weshapiga hesababu nyengine hapo ................na mara nyingi influence ya wazee au jamii inaingia.

kuna wengine wanakataa kuolewa na fulani kwa sababu mama mdogo wake ameolewa kwenye ukoo huo huo ( hapa anaogopa ghadhabu za jamii tu ingelikuwa hili halipo angeolewa)
kuna wengine hawezi kuolewa na mtoto wa baba mkubwa ( kwa kuhofia jamii/ wazee ...........japo wanapendana)
mwengine ataolewa na mtu ambae jamii yake haimkubali lakini kwa kuwa anauhakika na security yake anakubali ( mapenzi + security hapa yanashika hatamu)

nitamalizia kwa kusema ................wanawake wanaolewa kwa Mapenzi tu (bila ya kufikiria faida nyengine ni wachache mno)
 
Back
Top Bottom