Ni kweli kuwa watu wote walioko kwenye ndoa au waliooana wanapendana?

Duh sijui nimemiss vipi hii mada jana!! Naomba na miye thumuni yangu kutokana na uzoefu wangu. Jibu la kwanza na la haraka ni kuwa "Si kweli" wote walioko kwenye ndoa, siyo wote wanaopendana kwani wengine wameoana kwa ajili ya makaratasi!

Baada ya jibu hilo naomba nizame kidogo.

Kwanza tunakabiliwa na matatizo ya kufafanua "upendo" ni nini hasa kiasi cha kusema kuwa fulani na fulani wanapendana. Sote tunajua kuwa baba wazazi wanawapenda watoto wao, ndugu wanapendana, rafiki wanapendana na wapo ambao wana upendo wa kwa wanyama wao! Tunapozungumzia upendo basi tunazungumzia mchanganyiko wa hisia nyingi sana ambazo tunazo juu ya vitu na watu mbalimbali.

Hata hivyo tunapofika kwenye masuala ya mapenzi tunazungumzia aina ya upendo ambao ni tofauti na upendo wa mzazi kwa mtoto, mtu kwa ndugu yake au rafiki au mtu kwa kitu kingine. Tunazungumzia upendo ambao unahusiana moja kwa moja na tamaa za kijinsia. Wenzetu Wagiriki waliupa upendo huu jina la Eros ambapo kutoka kwalo tunapata neno la Kiingereza "Erotic". Ni upendo wenye tamaa za mwili vile vile na kuzaa - Eros mwenyewe alikuwa ni mungu wa wagiriki wa kale anayehusiana na mambo ya mapenzi na uzazi.

Ndoa kwa upande mmoja ni taasisi ambayo jamii mbalimbali za binadamu zimekuwa zikiitumia kwa mtindo mmoja au mwingine kuelekeza huu upendo. Yaani, mahali halali pa kutumia tamaa za mwili na kuzaana. Matokeo yake ndoa vile vile ni chombo cha malezi ya kizazi kipya cha jamii. Kutokana na hili tangu kale jamii mbalimbali zimekuwa na utaratibu wake wa kuwahalalisha wana ndoa.

Msingi wa ndoa hata hivyo ni kujitoa kwa mtu mmoja kwa mwingine kuwa sehemu ya maisha yake ili kuweza kutimiza tamaa ya mwili na kulea familia. Lakini ingekuwa hivyo tu ingekuwa inatosha lakini ndoa ni zaidi ya tamaa za mwili na familia. Ndoa ni sehemu ya upamoja wa watu wawili (au zaidi) katika maisha na kuweza kusaidiana, kushirikiana na kusindikizana katika safari ya maisha hadi pale ambapo unafikia mwisho wake wa asili au pale ambapo inaonekana haiwezekaniki tena.

Sasa, katika maisha mtu anaweza kujikuta anampenda fulani katika maana zote mbili yaani kutaka kuwa pamoja naye na katika kushirikiana tamaa za mwili. Hilo la kuwa pamoja mara nyingi ni zaidi ya hisia za mwili, mara nyingi ni uamuzi wa kiakili (rational choice) kwa watu kuwa pamoja. Kwa vile kuwa pamoja ni rational choice wakati mwingine halizingatii sana kina cha tamaa za mwili baina yao. Hivyo, hata kama tamaa za mwili haziridhishwi ipasavyo mtu bado anajikuta anampenda mwenzie.

Hapa ndipo linatokea tatizo. Mtu anaweza kuwa na mtu anayependa kuwa naye pamoja katika safari ya maisha na kushare vitu vingi maishani vikiwemo familia. Lakini, inakuwaje kama sehemu yake ya tamaa za mwili hairidhishwi na mtu yule? Inakuwaje kama msisimko wa mapenzi umeshakoma, je hampendi huyo mtu mwingine? Ni rahisi kwa mtu asiyekuwepo kwenye mazingira hiayo kuweza kuelewa utata huu.

Ni utata wa kujua kabisa kuwa x ni mtu wake na unampenda na kumjali lakini kwenye tamaa za mwili hakuwashi kama zamani. Katika mazingira haya basi wanandoa hujikuta wakilazimika kufanya mambo mbalimbali ili "kuyafufua mahaba" kati yao na pale ambapo kweli inashindikana basi mtu anaweza kuamua kutoka kwenye ndoa na kupata talaka.

Wengine hawataki kutoka kwenye ndoa (kwa sababu bado anamepnda yule mwingine) lakini anaamua kwenda nje ya ndoa kutafuta eros!

Lakini katika maisha haya haya kunawakati mtu katika ndoa anapoteza vyote viwili, yaani hana tamaa na mwenzie na hamfurahii mwenzie. Yaani wanageuka na kuwa kama watu wawili ambao hawawezi kukaa mahali pamoja wakaelewana. Katika mazingira hayo kuna uwezekano wa kuanza kutoka vurugu (abuse) baina yao na hata matumizi ya nguvu na udhalilishaji (violence). Nimepata bahati ya kufanya internship katika mambo ya Domestic violence ambapo nimeyaona mengi ya aina hii.

Katika mazingira ambapo mtu hana vyote viwili ni kwanini basi mtu bado anabakia kwenye ndoa? Jibu la swali hili haliwezi kutolewa na kujibu matatizo ya watu wote. WEngine wamedokeza kuwa kama alivyoimba Johnny Taylor "its cheaper to keep her"! Maana yake kuna gharama kubwa zaidi kuachana kuliko kuendelea kukaa pamoja hasa kama hakuna ugomvi wa wazi, vurugu au kuvunjiana heshima. Hivyo, kama watu ambao waliweza kuwa marafiki na wamepoteza ule upendo wa awali na kurudi kwenye upendo wa urafiki basi wanaona ni bora kukaa pamoja kwani ndoa aidha itavuruga maisha yao, hadhi zao, familia zao n.k

Kwa wale ambao wanaona ni vigumu kuendelea kuwa pamoja ndio hufanya kama walivyofanya Al Gore na Tipper wiki chache zilizopita ambapo baada ya miaka 40 ya ndoa waliamua kuachana.

Lakini swali jingine la kuzamia ni hili: Ni upendo kiasi gani unahitajika kudumisha ndoa? Ukiniuliza mimi nitakuambia unahitajika upendo kidogo tu wala si mkubwa kama wawakati wa uchumba au wakati wa mwanzo wa ndoa.

Wazee wetu walijifunza hili kwani utakuta wengine walifungishwa ndoa hata bila kufahamiana sana lakini wakaweza kukua katika upendo na wakadumu licha ya changamoto nyingine njiani. Na hata wale ambao walianza kwa kupendana kwa kadiri maisha yanayvoenda wanajua wamefikia mahali pa kujua kuwa upendo mdogo walionao ndio kamba idumuyo yenye kuwaunganisha mioyo yao. Kwa hawa utaona kuwa matatizo ya kukosekana eros ya mara kwa mara ni matatizo madogo zaidi kuliko upendo wao.

Upendo basi katika ndoa ni muhimu lakini siyo kitu pekee kinachodumisha na kufurahisha ndoa kwani kuna vikolombwezo vingine ambavyo endapo vitakuwepo basi ndoa yaweza hata ya kuwa na furaha.

Vitu kama kuelewana, kupingana bila kupigana, kuheshimiana, kulindana bila kuvurundana, kusaidiana na kuinuana.

Vitu hivyo ni muhimu sana kwenye ndoa kuliko mtu kukuambia "nakupenda" wakati hana vitu hivyo. Kosa kubwa ambalo watu wanafanya hasa wanandoa wachanga ni kudhania upendo ni kuwa na tamaa ya mwili kwa huyo mtu mmoja tu na mtu akianguka au kwenda nje ya ndoa maana yake amepoteza upendo.

Kwa wale ambao wamewahi kucheat (najua wapo) na hata wale wenye kuendelea kuchat (wakati unasoma hili) utajua kuwa yawezekena unacheat zaidi kwa ajili ya eros kuliko upendo wa moyoni. Kwamba, unapata raha fulani ya kimwili na huyo mtu wa pembeni ambayo huipati kwa mwenzio wa ndoa lakini moyo wako bado uko kwa huyo mwenzio na usingependa kabisa ije kugundulika kwa sababu "unataka kulinda ndoa yako". Ndio maana nimesema kwenye ndoa ni pamoja na kuinuana na kusaidiana.

Ushauri kwa vijana, endapo mwenzio ameanguka kwenye majaribu ya eros, muinue na umsaidie bila ya wewe mwenyewe kujiweka majaribuni au katika hali ya kutishia maisha yako. Kwa mfano, kama mwenzio ameenda nje ya ndoa au ya mahusiano na ukatambua hilo, na hutaki kuvunja ndoa yenu basi ni muhimu kuhakikisha mnapimwa na kuhakikisha wote mko salama na kutumia kinga ili kutojiweka hatarini. Wakati mwingine inabidi uende kwa dizaini ya Tina na Waziri kwa muda ili kuweza kurudisha timamu katika ndoa.

Samahani, nilikuwa najibu swali gani?
 
mwenzangu hata nimesahau nilianzia wapi! uzee huu..

Usijali. Ulipoishia ni muhimu sana kuliko ulikoanzia. Inataka moyo kusoma makala ndefu lakini ukishaimaliza ndipo unapogundua kuwa umechota mengi sana na kwamba inalipa. Hii tungeipata jana ingetusaidia wakati huo mzuko ulikuwa juu sana.

Hapo karibu na mwisho, nimekutana na nadharia ambayo nadhani inahitaji nguvu ya roho wa bwana kuitekeleza. Kwamba ukimnasa mwenzio anagawa chakula ya mwenyewe umpe nafasi na ushauri nasaha (+ massage) ili arudie hali ya kawaida muendelee. Hapa inabidi uwe na roho ya paka! Sina hakika kama mimi ninayo.
 
pole sana.. miye nilifikia huko na nikagundua upendo ni zaidi ya kumcontrol mwenzio kwenye tamaa za mwili! usimwambie mtu
 
Mwanakijiji Heshima yako ndugu yangu!
Nadhani umedadavua yale yote muhimu ... wenye macho wasome na kuelewa!
 
Ahsante M'kijiji. Nilishapitia makona ya kutosha na nadhani sasa niko kwenye highway (may be M5). Kwani kuishi na mtu uliyekutana naye wote mna meno 32 na kushare naye karibia kila kitu kwa zaidi ya miaka 10 si haba ati? Ila hilo la kuvumilia kuibiwa sijui itakuwaje. Ngoja nisipate ugonjwa wa moyo bure kwa kuwazia jambo ambalo labda halipo!
 
Mwanakijiji Heshima yako ndugu yangu!
Nadhani umedadavua yale yote muhimu ... wenye macho wasome na kuelewa!

Da WoS, unadhani macho hawana? Macho wanayo/tunayo sana. Ila kwenye haya mambo ya mahusiano nadhani ile milango 5 ya fahamu yote haifanyi kazi. Labda kuna mwingine!
 
ok I missed this topic...very Good Topic WOS... you can have your own TV show WOS....
 
Duh sijui nimemiss vipi hii mada jana!! Naomba na miye thumuni yangu kutokana na uzoefu wangu. Jibu la kwanza na la haraka ni kuwa "Si kweli" wote walioko kwenye ndoa, siyo wote wanaopendana kwani wengine wameoana kwa ajili ya makaratasi!

Baada ya jibu hilo naomba nizame kidogo.

Kwanza tunakabiliwa na matatizo ya kufafanua "upendo" ni nini hasa kiasi cha kusema kuwa fulani na fulani wanapendana. Sote tunajua kuwa baba wazazi wanawapenda watoto wao, ndugu wanapendana, rafiki wanapendana na wapo ambao wana upendo wa kwa wanyama wao! Tunapozungumzia upendo basi tunazungumzia mchanganyiko wa hisia nyingi sana ambazo tunazo juu ya vitu na watu mbalimbali.

Hata hivyo tunapofika kwenye masuala ya mapenzi tunazungumzia aina ya upendo ambao ni tofauti na upendo wa mzazi kwa mtoto, mtu kwa ndugu yake au rafiki au mtu kwa kitu kingine. Tunazungumzia upendo ambao unahusiana moja kwa moja na tamaa za kijinsia. Wenzetu Wagiriki waliupa upendo huu jina la Eros ambapo kutoka kwalo tunapata neno la Kiingereza "Erotic". Ni upendo wenye tamaa za mwili vile vile na kuzaa - Eros mwenyewe alikuwa ni mungu wa wagiriki wa kale anayehusiana na mambo ya mapenzi na uzazi.

Ndoa kwa upande mmoja ni taasisi ambayo jamii mbalimbali za binadamu zimekuwa zikiitumia kwa mtindo mmoja au mwingine kuelekeza huu upendo. Yaani, mahali halali pa kutumia tamaa za mwili na kuzaana. Matokeo yake ndoa vile vile ni chombo cha malezi ya kizazi kipya cha jamii. Kutokana na hili tangu kale jamii mbalimbali zimekuwa na utaratibu wake wa kuwahalalisha wana ndoa.

Msingi wa ndoa hata hivyo ni kujitoa kwa mtu mmoja kwa mwingine kuwa sehemu ya maisha yake ili kuweza kutimiza tamaa ya mwili na kulea familia. Lakini ingekuwa hivyo tu ingekuwa inatosha lakini ndoa ni zaidi ya tamaa za mwili na familia. Ndoa ni sehemu ya upamoja wa watu wawili (au zaidi) katika maisha na kuweza kusaidiana, kushirikiana na kusindikizana katika safari ya maisha hadi pale ambapo unafikia mwisho wake wa asili au pale ambapo inaonekana haiwezekaniki tena.

Sasa, katika maisha mtu anaweza kujikuta anampenda fulani katika maana zote mbili yaani kutaka kuwa pamoja naye na katika kushirikiana tamaa za mwili. Hilo la kuwa pamoja mara nyingi ni zaidi ya hisia za mwili, mara nyingi ni uamuzi wa kiakili (rational choice) kwa watu kuwa pamoja. Kwa vile kuwa pamoja ni rational choice wakati mwingine halizingatii sana kina cha tamaa za mwili baina yao. Hivyo, hata kama tamaa za mwili haziridhishwi ipasavyo mtu bado anajikuta anampenda mwenzie.

Hapa ndipo linatokea tatizo. Mtu anaweza kuwa na mtu anayependa kuwa naye pamoja katika safari ya maisha na kushare vitu vingi maishani vikiwemo familia. Lakini, inakuwaje kama sehemu yake ya tamaa za mwili hairidhishwi na mtu yule? Inakuwaje kama msisimko wa mapenzi umeshakoma, je hampendi huyo mtu mwingine? Ni rahisi kwa mtu asiyekuwepo kwenye mazingira hiayo kuweza kuelewa utata huu.

Ni utata wa kujua kabisa kuwa x ni mtu wake na unampenda na kumjali lakini kwenye tamaa za mwili hakuwashi kama zamani. Katika mazingira haya basi wanandoa hujikuta wakilazimika kufanya mambo mbalimbali ili "kuyafufua mahaba" kati yao na pale ambapo kweli inashindikana basi mtu anaweza kuamua kutoka kwenye ndoa na kupata talaka.

Wengine hawataki kutoka kwenye ndoa (kwa sababu bado anamepnda yule mwingine) lakini anaamua kwenda nje ya ndoa kutafuta eros!

Lakini katika maisha haya haya kunawakati mtu katika ndoa anapoteza vyote viwili, yaani hana tamaa na mwenzie na hamfurahii mwenzie. Yaani wanageuka na kuwa kama watu wawili ambao hawawezi kukaa mahali pamoja wakaelewana. Katika mazingira hayo kuna uwezekano wa kuanza kutoka vurugu (abuse) baina yao na hata matumizi ya nguvu na udhalilishaji (violence). Nimepata bahati ya kufanya internship katika mambo ya Domestic violence ambapo nimeyaona mengi ya aina hii.

Katika mazingira ambapo mtu hana vyote viwili ni kwanini basi mtu bado anabakia kwenye ndoa? Jibu la swali hili haliwezi kutolewa na kujibu matatizo ya watu wote. WEngine wamedokeza kuwa kama alivyoimba Johnny Taylor "its cheaper to keep her"! Maana yake kuna gharama kubwa zaidi kuachana kuliko kuendelea kukaa pamoja hasa kama hakuna ugomvi wa wazi, vurugu au kuvunjiana heshima. Hivyo, kama watu ambao waliweza kuwa marafiki na wamepoteza ule upendo wa awali na kurudi kwenye upendo wa urafiki basi wanaona ni bora kukaa pamoja kwani ndoa aidha itavuruga maisha yao, hadhi zao, familia zao n.k

Kwa wale ambao wanaona ni vigumu kuendelea kuwa pamoja ndio hufanya kama walivyofanya Al Gore na Tipper wiki chache zilizopita ambapo baada ya miaka 40 ya ndoa waliamua kuachana.

Lakini swali jingine la kuzamia ni hili: Ni upendo kiasi gani unahitajika kudumisha ndoa? Ukiniuliza mimi nitakuambia unahitajika upendo kidogo tu wala si mkubwa kama wawakati wa uchumba au wakati wa mwanzo wa ndoa.

Wazee wetu walijifunza hili kwani utakuta wengine walifungishwa ndoa hata bila kufahamiana sana lakini wakaweza kukua katika upendo na wakadumu licha ya changamoto nyingine njiani. Na hata wale ambao walianza kwa kupendana kwa kadiri maisha yanayvoenda wanajua wamefikia mahali pa kujua kuwa upendo mdogo walionao ndio kamba idumuyo yenye kuwaunganisha mioyo yao. Kwa hawa utaona kuwa matatizo ya kukosekana eros ya mara kwa mara ni matatizo madogo zaidi kuliko upendo wao.

Upendo basi katika ndoa ni muhimu lakini siyo kitu pekee kinachodumisha na kufurahisha ndoa kwani kuna vikolombwezo vingine ambavyo endapo vitakuwepo basi ndoa yaweza hata ya kuwa na furaha.

Vitu kama kuelewana, kupingana bila kupigana, kuheshimiana, kulindana bila kuvurundana, kusaidiana na kuinuana.

Vitu hivyo ni muhimu sana kwenye ndoa kuliko mtu kukuambia "nakupenda" wakati hana vitu hivyo. Kosa kubwa ambalo watu wanafanya hasa wanandoa wachanga ni kudhania upendo ni kuwa na tamaa ya mwili kwa huyo mtu mmoja tu na mtu akianguka au kwenda nje ya ndoa maana yake amepoteza upendo.

Kwa wale ambao wamewahi kucheat (najua wapo) na hata wale wenye kuendelea kuchat (wakati unasoma hili) utajua kuwa yawezekena unacheat zaidi kwa ajili ya eros kuliko upendo wa moyoni. Kwamba, unapata raha fulani ya kimwili na huyo mtu wa pembeni ambayo huipati kwa mwenzio wa ndoa lakini moyo wako bado uko kwa huyo mwenzio na usingependa kabisa ije kugundulika kwa sababu "unataka kulinda ndoa yako". Ndio maana nimesema kwenye ndoa ni pamoja na kuinuana na kusaidiana.

Ushauri kwa vijana, endapo mwenzio ameanguka kwenye majaribu ya eros, muinue na umsaidie bila ya wewe mwenyewe kujiweka majaribuni au katika hali ya kutishia maisha yako. Kwa mfano, kama mwenzio ameenda nje ya ndoa au ya mahusiano na ukatambua hilo, na hutaki kuvunja ndoa yenu basi ni muhimu kuhakikisha mnapimwa na kuhakikisha wote mko salama na kutumia kinga ili kutojiweka hatarini. Wakati mwingine inabidi uende kwa dizaini ya Tina na Waziri kwa muda ili kuweza kurudisha timamu katika ndoa.

Samahani, nilikuwa najibu swali gani?

Asante kwa darasa
 
Babuuuuu!! Kumbe siku moja moja huwa hulewi.
Kabla sijamuoa huyu mama matesha wangu nilikuwa na mpenzi wangu niliyekuwa nampenda sana. Ki ukweli tulipendana sana. Na tuliachana bila kujua kimetokea nini. Niliumia sana, nilitaabika sana. Sikuwa nahitaji kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine awaye yote. Nilitamani kuwa padre.

Mpaka alipotokea huyu rafiki yake nu huyo mpenzi wangu wa zamani. Alikuwa ananionea huruma sana, alikuwa ananifariji na kunipa moyo. (Tulipoachana na mpenzi wangu, mpenzi wangu huyo alitokomea kubeba mabox na mpaka leo hajarudi -RIP kama ameshakufa). Huyu rafiki yake ndio huyu mama matesha wangu.

Nadiriki kusema nashukuru niliachana na mpenzi wangu yule wa zamani kwa kuwa huyu mke wangu wa sasa ndio ulikuwa mpango wa Mungu awe mke wangu. She is beautiful, loving and caring. Sitajuta kuonana naye (sijawahi kujuta miaka yote 15 ya kufahamiana toka urafiki, upenzi, uchumba mpaka ndoa.

Hivi thread inasemaje?? Oooh Yes.... Mimi na mke wangu Tunapendana sana. Ndani ya ndoa yetu tunapendana. Period!!!
(Am sore leo sina hangover ya kutosha)
 
Back
Top Bottom