Ni kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo yapo taratibu sana?

kevin strootman

JF-Expert Member
Nov 26, 2017
1,077
1,728
Nimekaa sana Kigamboni na nimetembea sehem nyingi, sehemu kubwa ya Kigamboni ni mapori tuu, miundombinu mibovu sana, barabara za lami ni chache mno, hakujajengeka sijui kwanini watu hawajengi Kwa Kasi.

Ukitoka Mji Mwemba mpaka Pemba mnazi Kuna sehemu lami inaishia, Kimbiji ya miaka 10 iliopita na ya Leo hakuna tofauti, huko Buyuni Sasa kama mkoani, njoo Mwasonga hapo kati ni mapori tu na barabara mbovu, ukitokea kiwanda cha Nyati cement kupitia mwasonga-kibada barabara ni mbovu balaa, mvua zikinyesha hapapitiki, kuna sehemu kuna mashamba ya mpunga kunajaa maji balaa hakuna nyumba ni nyasi tuu na mapori unaweza ukasema sio Dar.

Nashangaa sana juzi nmetoka Chanika nikataka kupotea, kumbe Chanika kumekuwa mjini kabisa, nashangaa sana kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo hamna au kwakuwa wilaya mpya ndio maana inakua ya mwisho Kwa maendeleo Kwa hizi wilaya 5 za Dar??
 
Nimekaa sana kigamboni na nmetembea sehem nyingi, sehemu kubwa ya kigamboni ni mapori tuu, miundombinu mibovu sana, barabara za lami ni chache mno, hakujajengeka sijui kwanini watu hawajengi Kwa Kasi.

Ukitoka mjimwemba mpaka Pemba mnazi Kuna sehemu lami inaishia, kimbiji ya miaka 10 iliopita na ya Leo hakuna tofauti, huko buyuni Sasa kama mkoani, njoo mwasonga hapo kati ni mapori tu na barabara mbovu, ukitokea kiwanda cha Nyati cement kupitia mwasonga-kibada barabara ni mbovu balaa, mvua zikinyesha hapapitiki, Kuna sehemu Kuna mashamba ya mpunga kunajaa maji balaa hakuna nyumba ni nyasi tuu na mapori unaweza ukasema sio dar.

nashangaa sana juzi nmetoka chanika nikataka kupotea, kumbe chanika kumekua mjini kabisa, nashangaa sana kwanini wilaya ya kigamboni maendeleo hamna au kwakua wilaya mpya ndio maana inakua ya mwisho Kwa maendeleo Kwa hizi wilaya 5 za dar??
KIGAMBONI HAKUNA VIONGOZI WA KUILETEA MAENDELEO
SIO DC MBUNGE WALA MKURUGENZI WAPO WAPO TU KILA SIKU SAFARI ZA KWENDA POSTA huwezi kuwaona wanatembelea Mitaa kata kuwasikiliza Wananchi Kero zao Barabara zote vumbi na mashimo mvua zikinyesha Mabwana kuna Mji mpya umepimwa nyuma ya Chuo cha Mkorea jirani na Kisota barabara hazina mifereji Madhimo utadhani mahanadi Kidi za Viwanja Mkurugenzi kachukua huduma hapeleki
MANISPAA ya Kigamboni inahitaji MABADILIKO MAKUBWA ya VIONGOZI
 
Huku hatuna viongozi..siku makonda alivo shindwa kula za maoni ccm niliumia sana maana yule mbunge anaonekana kipindi cha uchaguzi akimaliza hapo sahauni kumuona
Kweli kabisa jamaa Ngeshinda angefanya mapinduzi, hii wilaya Iko nyuma sana, Yani wilaya ya ilala Kuna sehemu zilikua hovyo Sana sasahv ni bonge moja ya mji aisee
 
KIGAMBONI HAKUNA VIONGOZI WA KUILETEA MAENDELEO
SIO DC MBUNGE WALA MKURUGENZI WAPO WAPO TU KILA SIKU SAFARI ZA KWENDA POSTA huwezi kuwaona wanatembelea Mitaa kata kuwasikiliza Wananchi Kero zao Barabara zote vumbi na mashimo mvua zikinyesha Mabwana kuna Mji mpya umepimwa nyuma ya Chuo cha Mkorea jirani na Kisota barabara hazina mifereji Madhimo utadhani mahanadi Kidi za Viwanja Mkurugenzi kachukua huduma hapeleki
MANISPAA ya Kigamboni inahitaji MABADILIKO MAKUBWA ya VIONGOZI
Mabarabara mengi ni mabovu sana
 
Ukitaka ukae sehemu ambayo inakuwa haraka. Nenda sehemu ambapo watu wa kipato cha kati na maskini wanajenga.

Kigamboni viwanja vingi na maeneo vinamilikiwa na watu matajiri ambao hawana shida ya nyumba za kuishi.

Unakuta mtu ana nyumba Mbezi beach ila amenunua kiwanja Kigamboni.

Huyo mtu hawezi kujenga leo wala kesho.

Hao ndio wanachelewesha mji kukua.

Tofauti na maeneo kama Chanika maana wanaonunua viwanja ni watu wenye shida ya nyumba za kuishi. Hivyo wanajenga fasta mji unajaa
 
Chanika imeendelea sana, majuzi nilimtembelea Rafiki yangu aliejenga huko mtazamo wangu juu ya Chanika ulibadilika, Kigamboni maendeleo yake hayakwepeki siku za usoni, nadhani kuchelewa kwake kuna manufaa pia ya kufanya planning ya mji, Ile Hype ya watu kukimbilia kujenga eneo moja inafanya mpangilio wa mji uwe Mbovu mfano halisi ni Goba.
 
Kuna kivule na msongola pia.. pameendelea sana na bado lami haijafika

Ikitokea pakapigwa lami patapanda value sana
Mkandarasi yupo site kwa barabara ya Msongola-Mbande ili kukamilisha njia yote itokayo Chanika-Mvuti-Kitonga-Msongola-Mbande-Chamazi- Mbagala.
Kwa speed yake hii njia Lami itawahi kukamilika.

Kimbembe ni barabara ya Msongola-Kivule-Kitunda kutokea banana ndio sijui lini Mungu atawakumbuka.

Ila hiyo miji inajengwa kwa Kasi ya kimbunga halafu kimya kimya bila kelele.
 
Mkandarasi yupo site kwa barabara ya Msongola-Mbande ili kukamilisha njia yote itokayo Chanika-Mvuti-Kitonga-Msongola-Mbande-Chamazi- Mbagala.
Kwa speed yake hii njia Lami itawahi kukamilika.

Kimbembe ni barabara ya Msongola-Kivule-Kitunda kutokea banana ndio sijui lini Mungu atawakumbuka.

Ila hiyo miji inajengwa kwa Kasi ya kinbunga halafu kimya kimya bila kelele.

Mimi mwaka 2022 nilitaka nunua kiwanja Kigamboni kwa ajili ya kujenga bar mbeleni.

Afisa ardhi ndio akanipa siri. Kwamba Kigamboni inachelewa kukua sababu viwanja vingi ni vya matajiri ambao hawana shida ya kujenga leo. Akaniambia kama nataka kiwanja cha kujenga bar nenda miji mipya inayojaa kwa kasi kama Goba, Chanika, Kivule ama Magole. Ni Miji inayokuwa kwa kasi

Ndipo nikaenda nunua kiwanja Kivule fremu 10.

Kiwanja nilinunua milion 5 mwaka 2022 ila mwaka jana kuna mtu amefika milioni 9 anakitaka. Na hapo hata lami bado haijawekwa..

Nimemkatalia sababu lengo langu ni bar ya kisasa. Bado nasubiri lami.
 
Kwani maendeleo ni nini?
Why mnataka Dar yote iwe kama Sinza? Hayo mapori yanapitisha hewa na kuleta nature ..iwabariki...

Kwani mji mzima ukiwa umejaa nyumba na lami na mabar kila hatua 2 ndo maendeleo?.....

Kabla hatujasema maendeleo lazima tujiulize maendeleo ndo yapi kwanza?
Au kukiwa na foleni hadi usiku ndo maendeleo?
 
Mimi mwaka 2022 nilitaka nunua kiwanja kigamboni kwa ajili ya kujenga bar mbeleni.

Afisa ardhi ndio akanipa siri. Kwamba kigamboni inachelewa kukua sababu viwanja vingi ni vya matajiri ambao hawana shida ya kujenga leo. Akaniambia kama nataka kiwanja cha kujenga bar nenda kivule ama magole. Mji unakuwa kwa kasi

Ndipo nikaenda nunua kiwanja kivule fremu 10.

Kiwanja nilinunua milion 5 mwaka 2022 ila mwaka jana kuna mtu amefika milioni 9 anakitaka. Na hapo hata lami bado haijawekwa..

Nimemkatalia sababu lengo langu ni bar ya kisasa. Bado nasubiri lami
Nafikiri Swala la Lami litafuatia baada ya barabara ya Msongola Mbande kukamilika.

Si unajua wananchi wa Kitunda Kivule wasivyo na dogo.

Una wazo kama langu ila Mkuu mbona bar unaweza kuanza ujenzi Lami itakukuta kati kati ya project yako
 
Mimi mwaka 2022 nilitaka nunua kiwanja kigamboni kwa ajili ya kujenga bar mbeleni.

Afisa ardhi ndio akanipa siri. Kwamba kigamboni inachelewa kukua sababu viwanja vingi ni vya matajiri ambao hawana shida ya kujenga leo. Akaniambia kama nataka kiwanja cha kujenga bar nenda kivule ama magole. Mji unakuwa kwa kasi

Ndipo nikaenda nunua kiwanja kivule fremu 10.

Kiwanja nilinunua milion 5 mwaka 2022 ila mwaka jana kuna mtu amefika milioni 9 anakitaka. Na hapo hata lami bado haijawekwa..

Nimemkatalia sababu lengo langu ni bar ya kisasa. Bado nasubiri lami
Originally Kigamboni ni mji wa wastaafu wasiotaka kelele za ma bar kama ya Sinza na misomgomano na mafoleni...baada ya daraja kujengwa ndo baadhi ya watu wanataka Kigamboni iwe kama Sinza...wakati wenyeji siku zote hawataki hizo kelele...

Ukivuka Tu Kigamboni...inakuwa hakuna foleni wala makelele...Saa tatu Tu mji uko kiimya.....
 
Back
Top Bottom