Ni kosa gani hutalisahau katika mahusiano yako?

Kosa kubwa sana nilifanya kugombana na mwanamke niliyempa mimba kwa sababu nilimtokea rafiki yake muarabu...

Siku akili iliponirudi nikasafiri kwenda kwake kuomba msamaha ila kabla sijafanikisha zoezi nikagundua ana bwana mwingine wakati bado ana mimba yangu!!!

Nilikasirika hadi nikaanza kuona mauzauza. Ili kutuliza akili yangu nilienda chuo fulani nikatafuta wanawake wakajaa kwenye kitoroli changu nikaenda nao club. Kulipokucha ndio nikagundua nilidraw hela benki hadi kiwango cha mwisho kwa siku na hapo hata hela ya mafuta inabidi niende benki tena
 
Sitosahau siku nilimpa namba ya simu mtoto wa kidosi akanipigia akanikosa kumrejeshea akapokea mama yake daah mpaka leo inaniuma manake toto liliingia kilaini na alikuwa mzuri hatari. Sijui kahamia wapi hata vitaa simuoni tena.
 
sitasahau nilipoambiwa sikupendi na kuachwa hapo nikaambiwa kwanza huna faida yoyote kisa Pesa sina Aisee.
 
Sitasahau siku niliyoaibishwa mbele ya wakwe kwamba nina nini cha kuwatisha kisa nimemsomesha mwanao aje tusaidiane maisha na baada ya kupata ajira akanipiga teke,nashukuru now niko poa na nilienae.
Daah kweli unamachungu naona tungo tata tuuu.
 
Kosa ambalo sitolisahau

Ni siku demu wangu aliniambia wazazi wake wamesafiri kwenda kumsalimia bibi yake anaumwa kijijini.

Nikaenda kulala kwao maana tulikua majiran na kwao wote walikua shuleni kwahiyo alibaki peke yake.

Ebwana hata sa6 usiku haikufika wazazi hawa hapa. Mgonjwa wamempeleka hospitali na shangazi yake ilibisi aje alale na demu wangu.

Nlilala uvunguni mpaka sa10 asubui,na lile barid la mbeya acheni tu alafu baada ya mwezi tu nagundua kuna fala kamtundika mimba.

Hahaha hahaha aiseeee
 
Kosa kubwa nililofanya na kuharibu mustakabari wangu, ni kuanza kunywa pombe baada ya kuvurugwa na mpenzi. Nimekuwa mlevi sana najitahidi kuacha maisha yaendelee lakini sio rahisi.
 
Kumpa thamani kubwa kupitiliza niliyedhani angekuwa mke wangu, mwisho wa siku nikapigiwa simu ananiambia better tuachane kwan hana mapenzi na mimi tena. Haitokaa ijirudie tena, NEVER
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom