Ni kosa gani hutalisahau katika mahusiano yako?

Siku mpenzi niliyekuwa nampenda sana alinimwaga mbele ya boyfriend wake mpya, ajabu rafiki yake ambaye alikuwa mzuri kuliko yeye akanibembeleza tukaanza mahusiano naye!!!

Nilifurahia mahusiano ya huyu rafiki yake kuliko yake coz huyu kumbe alijua nahitaji nini!!
 
Kosa kubwa ambalo siwezi kulisahau ni jinsi nilivyotumia nguvu,akili,na rasilimali nyingi kukimbizana na turu turu mtaani huku nikiwa na kengeza kuona upendo wa kweli kwa My Muiseke Nyamughe!
cc afande Mentor mzee wa Chelsea
Lakini si ulifanikisha mengi pia kaka..Au level ya maisha ul8okuwa nayo zamani na saivi ni 1 na 5 nini..
 
Kosa ambalo sitolisahau

Ni siku demu wangu aliniambia wazazi wake wamesafiri kwenda kumsalimia bibi yake anaumwa kijijini.

Nikaenda kulala kwao maana tulikua majiran na kwao wote walikua shuleni kwahiyo alibaki peke yake.

Ebwana hata sa6 usiku haikufika wazazi hawa hapa. Mgonjwa wamempeleka hospitali na shangazi yake ilibisi aje alale na demu wangu.

Nlilala uvunguni mpaka sa10 asubui,na lile barid la mbeya acheni tu alafu baada ya mwezi tu nagundua kuna fala kamtundika mimba.
 
Lakini si ulifanikisha mengi pia kaka..Au level ya maisha ul8okuwa nayo zamani na saivi ni 1 na 5 nini..

Ndugu gharama za kuwekeza kwa wapenzi usiokuwa na fungamano nao ni kubwa kuliko uwekezaji kwenye bomba la kusafirishia gesi kutoka Ziwa Albert Uganda hadi bandari ya Tanga! Ukiisha kuja kumpata uliyepangiwa ndipo utagundua uko nyuma kama plate number ya semi trailer
 
Kosa ambalo sitolisahau

Ni siku demu wangu aliniambia wazazi wake wamesafiri kwenda kumsalimia bibi yake anaumwa kijijini.

Nikaenda kulala kwao maana tulikua majiran na kwao wote walikua shuleni kwahiyo alibaki peke yake.

Ebwana hata sa6 usiku haikufika wazazi hawa hapa. Mgonjwa wamempeleka hospitali na shangazi yake ilibisi aje alale na demu wangu.

Nlilala uvunguni mpaka sa10 asubui,na lile barid la mbeya acheni tu alafu baada ya mwezi tu nagundua kuna fala kamtundika mimba.
Pole sana mkuu
 
Siku alipochukua ela kwenye wallet yangu akaenda kumnunulia mwanamke mwengine zawadi .tena aliniuliza hivi wanawake .wanapenda zawadi Gani nikamtajia kwa mbwembwe zote kumbe anaenda kununuliwa mwengine.

hahahaha huku ukisubiri baada utapewa surprise kuna watu wanautani mbaya
 
Sitasahau enzi hizo naanza anza kazi kuna kasichana mtaani nilikapenda nikawa nakaita love of my life. Yani kalinisababisha nikamwacha mchumba wangu. Kalinikamua hela hadi familia ikatishia kunitenga ila mi siambiwi sickii (Imagine tulikuwa tumepanga kumnunulia kitu mama nikazingua kuwa sina hela wakati nimempa 500k/- ya shopping huyo msichana). Hata mke wangu (wakati huo rafiki tu) nikamwambia usinizingue we kwanza mtoto wa mama maisha ya kupambana huwezi! hapo alijaribu kunishauri kuwa nnakoenda siko.
Siku tumelala akapitiwa na ucngizi na aliweka simu kwenye charger na huwa ckuruhusiwa kuishika coz of password. Cku hiyo anadownload cjui nini simu ilikuwa wazi. Nikakuta pic zake za uchi kwene gallery. Naangalia msg za whatsapp kawatumia watu wawili na ni 20mins ago, yani mi niko bafuni ye anajipiga akiwa na kanga ile ile alotoka nayo bafuni na kutuma. Mbaya zaidi ana wanaume wengine zaidi ya wa3 , I couldn't keep on scrolling yani. Nikazima simu ikaendelea kucharge. Kesho yake nikaamka saa 11 nikaenda kwa mama kumuomba msamaha. Akati narudi nikakuta demu kasharudi kwao nilichukua vitu vyake vyote(Ilikuwa come to stay type) nikampelekea nikamwambia nasafiri. Hadi leo hatujagombana wala nini (Niliogopa kutukana mamba kabla ya kuvuka mto. Nikiassume naweza kumpiga chini akanikashifu kuwa kwanza ckua chaguo lake) na hajui kwanini tuliachana(actually i was hoping naweza kuja kumsamehe lakini moyo wangu haukumrudia tena).
 
Hahah hii kufatilia mke wako iko siku utajikuta we ndo mchepuko ukapewa na kipondo cha ukweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom