AY 5225
JF-Expert Member
- Jul 16, 2023
- 484
- 1,135
Heshima yenu wakuu.
Kuteleza na kuanguka kisha kuinuka tena na kusonga mbele ni shule nzuri sana ya vitendo ambayo humfanya mwanadamu kuwa na mbinu thabiti za kutatua changamoto zake za hapa na pale katika maisha. Wazungu wanasema, "mistakes are the best lessons".
Nawakaribisha kwenye uzi huu mje mtiririshe vitu ambavyo ulifanya miaka kadhaa iliyopita na unatamani usingefanya ama ungevifanya tofauti ili vitumike kama somo kwa wengine.
Binafsi mwezi huu umetimiza mwaka mmoja toka nihitimu shahada yangu ya kwanza na kitu ninachotamani ningefanya tofauti ndani ya huo mwaka mmoja uliopita toka nihitimu chuo ni kutokua mtu anaejifungia ndani na kuangalia series siku nzima kila siku.
Kipindi hicho chote nilikua niki'apply nafasi za kazi mbalimbali bila mafanikio na ilikua kila nikihudhuria interviews narudi ghetto nikiwa nimekata tamaa sana kwani mategemeo yalipitiza uhalisia wa mambo.
Baada ya kujiunga na JF na kupata busara za waliotangulia, hivi sasa nimekua mtu wa kujichanganya kutafuta mishe za hapa na pale na tabia ya kushinda ndani bila mpango imekoma.
Hata hivyo sijilaumu sana kwani ni rahisi sana kubadili uelekeo ila ni ngumu sana kubadilisha imani. Mtu aliekaa darasani kwa miaka 16 kwa imani ya kwamba akimaliza atapata kazi fulani, sio rahisi kumbadilisha imani kwa muda wa miezi kadhaa kwamba ajiajiri na hata kupata huo mtaji wenye ni changamoto.
Ushauri wangu kwa waliyo chini yangu; USIKAE NDANI MKUU. USIKAE NDANI MKUU. USIKAE NDANI MKUU. TOKA NENDA POPOTE TU UNAPOWEZA KUANZIA.