Masikini_Jeuri
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 6,829
- 1,296
Mama mmoja mkazi wa Nkuhungu hapa mjini Dodoma, jana amelia kwa masikitiko makubwa na kutoamini baada ya kumkuta mpwawe wa umri wa miaka 4 akiwa kaumizwa vibaya kwa kupigwa na kuchomwa na pasi mgongoni na shangazi yake mdogo (Binamu yake huyu mama). Shangazi mkubwa aligundua hilo baada ya kupita siku 3 tangu mpwa atendewe ukatili huo! (Tunalo la kujifunza hapa wazazi na walezi)!
Mtoto huyo amabaye amefiwa na Baba (Kaka yake na huyu mama) alichukuliwa kuletwa kutunzwa na shangazi yake hapa Dodoma na wakati huo huo huyu Mama alikuwa anaishai na binamu yake (Shangazi mdogo) amabaye ndiye amekuwa akiwasaidia kazi za pale nyumbani kama dada wa kazi.
Kwa mujibu wa maelezo ya mtoto ni kwamba amekuwa akifanyiwa vitendo vingi sana vya kunyanyaswa na kuteswa na tukio hili ni baada ya kujinyea! Shangazi mdogo kwa hasira alimshushia kipigo mtotto huyo na hiyo haikutosha alimwamuru avue nguo na kisha alimchoma na pasi ya umeme mgongoni ! Ili kuficha maovu haya alimtishia kuwa atamwadhibu zaidi akija kumsema kwa shangazi mkubwa na pili alimvisha pull over kila wakati shangazi mkubwa akiwepo; Piga picha ya mateso aliyovumilia mtoto huyo kwa siku 3!
Kilichosababisha kugundulika jana ni baada ya shangazi mkubwa kuchelewa kuelekea mihangaikoni alipitia chumbani kwa mpwawe na kugundua kuwa amekojoa kitandani. ndipo alipomwamsha na kumkuta akiwa na nguo nzito mwilini na zikiwa zimelowana. Hivyoa limvua nguo zote na ndipo alipokutana na jambo la kusikitisha........!
Alichokifanya shangazi mubwa ni kumsafirisha huyo binamu yake arudi kwao! Nampa pongezi kwa moyo wake wa kusamehe lakini pia sidhani kama ni hatua sahihi! Anasema anahisi kuwa endapo angechukua hatua ya kisheria ni wazi huyu binamuye angefungwa na hilo huenda lingepelekea kugombana nandugu zake ambao ni wazazi wa huyu Binti (Binamu). na pili kwa ukatili huo anaogopa kuwa baada ya kutoka huyu mtu anaweza kuja kumdhuru hata kwa kumuua.
Wana JF hasa sie wazazi na walezi naomba kwa pamoja kwa nafasi zetu tuwaombee wanetu! Tuombe ulizi wa Mungu kwa wanetu! Pili tuwaombee hawa wanaotusaidia kulea wanetu!
Mungu aingilie kati!:amen: