Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,445
Jamani dada wa watu yamemkuta maswala ya bill za pombezi na msosi anatupiwa yeye na Boy friend wake alipe au washare cost.
Hii ya cost sharing wadau mnaionaje wale wa vyangu vyetu na chako ni chako mtakuwa upande upi?
Kulekule kwa Dinahicious wa Bongoradio.Mwaka huu ulipoanza nilipata mchumba ambaye wakati tunakutana mimi nilikuwa nimeajiriwa na yeye akiwa bado so unakuta tulipokuwa tunatoka out I had to share cost with him ili asijione ni mzigo kwake. Mchumba kwangu namwona ni mtu wa ajabu maana anaweza akaniita sehemu na kuagiza vitu na bill inapokuja ananirushia mpira mwanzo nilidhani kwa sababu hana kazi but now amepata kazi lakini bado anafanya the same.
Kama juzi tulitoka na rafiki zake bill ilipokuja akalipa chakula na kunirushia mpira bill ya vinywaji, kisa alijua siku hiyo nimepata pesa Ofisini. Kwa shingo upande nikatoa ma kulipia vinywaji. Aunt hii sio mara ya kwanza there are time nilifiwa na ilinibidi kusafiri kwenda nyumbani (Kijijini) wakati msiba umetokwa ilikuwa kama 3 days before birthday yake.
Niliporudi kama 2 dayz baada ya siku yake huyu Mchumba akawa ananikumbushia zawadi yake bila hata huruma kwamba nilitumia pesa kusafiri kwenye msiba tena wala yeye hakunipa hata shilingi kwa ajili ya safari.
Jamani eti hii ni kawaida au huyu wangu kazidi?
Hii ya cost sharing wadau mnaionaje wale wa vyangu vyetu na chako ni chako mtakuwa upande upi?