Ni adhabu ipi iwe mbadala wa viboko kwa wanafunzi watukutu mashuleni?

Ni kweli kabisa kile kinachoonekana kwenye video clip ni matokeo ya mchakato unaoanzia mbali, na hilo hutokana na ukosefu wa maadili kwa wanafunzi na ukosefu wa busara kwa mtoa adhabu (kutoa adhabu akiwa na hasira)
Kabla hamjafika huko kwenye kumsimamisha masomo, lazima kuna mahali mlianzana na huyo mwanafunzi. Fikiria umemkuta mwanafunzi na kosa linalostahili achapwe viboko, unamwambia nyoosha mkono nikuchape, anakwambia mwalimu mi hunichapi. Unaona isiwe tabu, unamwambia tangulia ofisini, ukidhani labda kule kwa kuwa mpo walimu wengi ataogopa na utamchapa kirahisi, nako ukifika anakudishia vilevile. Mwalimu anapanic, na kuanza kumchapa dogo randomly, dogo anakamata fimbo na kuivunja. Sasa hapo ndio ile mitama , mateke na mangumi unayoiona kwenye video za kurekodiwa inapoanzaga. Mwalimu tayari anajazba, dogo nae ni nunda by nature, hahahahahaa yajayo lazima mfumbe macho kwakweli.
 
Na unajua kuna umri fulani hata mzazi unaona aibu kumpiga mwanao...
Sasa hawa walimu wanataka eti kumchapa mtoto ambaye ana nguvu zaid yao...
Wajiongeze...
Mtoto anapozidi kukua anahitaji kuheshimiwa na wazazi, walimu na jamii
Unaona aibu, lakini ushatamani kumpiga. Mpaka hapo kuna alilolifanya lililokukera. Taratibu za nyumbani kwako ni tofauti na shuleni. Kule walimu hawatoi laana, wanachapa. Mzazi kama hutaki mwanao achapwe na unajua ni nunda, plz mpeleke gereji au akashone cherehani.
 
Kwa nini mwanangu awe nunda?
Wewe una mtoto nunda?
Usiwabatize watoto majina mabaya...ni kuwapa laana
 
Sidhani kama kupiga ni suluhu
Ifike mahali kama ni wadogo sana hata kuangalia ukuta kwa nusu saa ni adhabu kubwa kwa mtoto kwani anakosa raha kabisa
Kwa wenye makamo ni kuwatoa darasani
Na kuandika au kumuita mzazi na kumwambia

Shule nyingi waalimu hawawajui hata wazazi achilia mbali hata kuandika barua tu
Mtoto anafundishwa kwani kila kitu ni kipya kwake
Utamaduni wetu ni mfumo mzuri sana wa kuheshimu wakubwa lakini isiwe kuwaogopa

Sent from my SM using Tapatalk
 
Shule za dini zinafaulisha na watoto wanakuwa na maadili mema sababu,hawacheki na kima,mtoto akijifanya kaenda kukua hapo shule anarudishwa nyumbani akamfate mzazi wake,aje afokewe badala yake.akirudia tena kosa nao wanamkataa mtoto wako,tena kwa unoko na ada unarudishiwa.

Jaman wazazi/walezi wangu walikuwa wanoko,sijawahi kuchekewa mimi kwenye maslahi mapana ya ustawi wa tabia yangu.nashukulu leo hii mimi si kijana wa ajabu ajabu,ili kuunga mkono juhudi za wazazi wangu namimi nitakuwa mnoko kwa kizazi changu chote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Comment inafurahisha aiseeee hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wanajukwaa, kama kichwa cha habari kinavyojieleza mimi kama mdau wa elimu ya Tanzania ningependa kupata ushauri kutoka kwenu kuhusiana na adhabu wanazopewa wanafunzi wanaokutikana na makosa mbalimbali mashuleni.

Hoja yangu imetokana na madhila ambayo yamewapata baadhi ya wanafunzi ambao kwa nyakati tofauti wameangukia kwenye vipigo vikali kutoka kwa wale waliopewa dhamana ya kuwasimamia na kuwafunza (walimu) jambo lililopelekea baadhi yao kupata maumivu makali na hata kuaga dunia.

Kwa sababu ya matokeo ya adhabu za walimu kwa wanafunzi wao, wadau mbalimbali wamekua wakishauri kuwa adhabu ya viboko mashuleni iondolewe. Jambo ambalo kwa mzazi yoyote aliyeona baadhi ya vipande vya video za walimu wakitoa adhabu kali kwa wanafunzi wao watakubaliana na hilo moja kwa moja.

Swali la kujiuliza hapa, je ni kwanini shuleni kuna adhabu? Jibu la moja kwa moja hapa ni kuwa adhabu hutolewa tu pale ambapo mwanafunzi ameenda kinyume na utaratibu ambapo kwa mujibu wa sheria inampasa aadhibiwe.

Kama ni hivyo basi mtoto huadhibiwa kwa sababu amekiuka utaratibu, na adhabu kuu na kongwe ni kuchapwa viboko au kupewa zoezi gumu, na jamii ya sasa haikubaliani na yote hayo. Ni nini basi kifanyike ili kuboresha nidhamu ya wanafunzia watukutu na wasiofuata utaratibu uliowekwa?

Kwa kuwa utukutu na kutokufuata utaratibu vimekuwepo enzi na enzi, na zama zote, hayo yalitafutiwa ufumbuzi wa namna mbalimbali. Ningeomba wanajukwaa kwa ujumla wetu tupate kulijadili hili na kupendekeza njia mpya za kukabiliana na watukutu pasipo kugusa miili yao kwa viboko, makofi, push up ama mateke.

Karibuni wana jukwaa tujadiliane.
I. Tujifunze kutumia Time management kama adhabu kwa vijana wanaochipukia (adolescence)
Kuhakikisha wanafanya kitu kwa muda maalum/ mchache mfano kabla ya muda wa kawaida wa masomo kuna kitu kama adhabu yake lazima awe amemaliza.

II. Kumpa adhabu ya kufanya kitu baadae chaweza kuwa hobby pia mfano kusoma kitabu na kukichambua kwa fixed time na afanye presentation ya kitabu

III. Au kama shule ina kompyuta unaona mwanafunzi ana tatizo la typing speed unampa adhabu at a fixed time awe amemaliza na kusubmit.

Makosa mengi ya vijana wa shule yanaletwa na loosing time au kuwa idle. Ukiwa idle ndio shida inapoanzia
Kuna adhabu nyingi sana zenye kujenga badala ya kujutia na kudhalilisha.
NB: police brutality ni zao la brutal actions since childhood.😔😔
 
Shukrani kwa mchango maridhawa.
 
Nashangaa watu wanaongelea maadili, mara nidhamu, sijui malezi.

Ipo hivi, huwezi kukwepa maendeleo ya sayansi na teknolojia. Badala ya kuona watoto wamekosa maadili kuwa na simu shuleni. Tuifanye hiyo kuwa fursa. Tuwafundishe namna ya kutumia simu zao kuwaongezea maarifa.
Kwani naamini lengo kubwa la mtoto kuletwa shuleni ni kupata maarifa ambayo yatakua msaada wake huko mbele kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Alafu suala la adhabu endepo mtoto ataenda kinyume na sheria za shule, ni kuwaita wazazi wake na kuongea nao. Ikishindikana baada ya wazazi kuitwa mara mbili, basi adhabu ya mwisho ni kumfukuza mtoto shule. Suala la nidhamu ni suala la wazazi. Maana mazingira tunayoishi, ndiyo yanayofanya nidhamu zetu.

Adhabu ya viboko ni utumwa. Tena utumwa ambao mimi naupinga kwa 100%
Kwenye kufundisha watoto juu ya matumizi ya simu halipo !!walimu wanafata mitaala ndio inayowaongoza!! Huwezi kwenda kinyume chake kisa tu maendeleo ya sayansi na teknolojia nooooo!!! Content inatoka kwenye mitaala ya elimu ndg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nahisi tusilaumu tu adhabu ambazo watoto wanazopewa bila kupendekeza adhabu mbadala na yenye manufaa.

Kwanza kumbuka mwalimu ni mlezi kama alivyo mzazi. Na hakuna mlezi ama mzazi yeyote atakayependa kuona mtoto akionyesha tabia isiyofaa na akamuacha pasipo kumkemea. Sisi kama wanajamii tusijikite kuwalaumu walimu bali tupendekeze njia bora ya kukabiliana na tabia zisizokubalika.

Huyo mkuu wa mkoa wa Tanga ambaye mimi sijamsikia kapendekeza njia mbadala? Au kajisemea tu kwa kuwa ana mamlaka na mdomo wa kusema.
MKUU naona watu hili suala wanalitumia kisiasa sana lakini madhara yake ni makubwa!!! Watu wanaongea tu hovyo na hii ni kwassbabu watu hawaijui taaluma hii na changamoto zake!!! Mtu anaongea utafikiri yeye alijifundsha!!! Yani kwamba Mwl anaonekana hafai kwa wakati fulani daaa tabu kweli kweli

Lakn kiujumla watoto tunawajua goja wabanwe walimu ambao lawama nyng zinawaelemea na wanataka kutumika kisiasa lakn tuelewe kwamba wanaopotea na Kuharibika ni watoto

Nakuwa nawaza tu fuuuuuuuuuuulani angepewa kufundsha au kukaa na hawa watoto Week moja tu angesema

Ila walimu kikubwa kiboko ni adhabu ya mwsho kikubwa watoto hawa tujenge mazoea ya kukaa nao,, kushauri na hata kuwa ambia pale wanapokosea nje na adhabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Adhabu ya watu kama hao ni kuwaachia dunia iwafunze tu wasisumbue wanaotaka kusoma, warudi nyumbani wacheze na wazazi wao
 
MKUU naona watu hili suala wanalitumia kisiasa sana lakini madhara yake ni makubwa!!! Watu wanaongea tu hovyo na hii ni kwassbabu watu hawaijui taaluma hii na changamoto zake!!! Mtu anaongea utafikiri yeye alijifundsha!!! Yani kwamba Mwl anaonekana hafai kwa wakati fulani daaa tabu kweli kweli

Lakn kiujumla watoto tunawajua goja wabanwe walimu ambao lawama nyng zinawaelemea na wanataka kutumika kisiasa lakn tuelewe kwamba wanaopotea na Kuharibika ni watoto

Nakuwa nawaza tu fuuuuuuuuuuulani angepewa kufundsha au kukaa na hawa watoto Week moja tu angesema

Ila walimu kikubwa kiboko ni adhabu ya mwsho kikubwa watoto hawa tujenge mazoea ya kukaa nao,, kushauri na hata kuwa ambia pale wanapokosea nje na adhabu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa ndugu, kwani hao wanaolijadili hili jambo kimzaha wangepewa fursa ya kukaa na hao watoto kwa wiki moja tu hakika wangekonda.

Halafu jambo jingine utundu wa watoto unatokana na mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa mfano, huku DSM maeneo ya Uswahilini kwetu utamkuta mzazi anamtukana matusi makubwa na ya nguoni kwa mtoto bila kujali umri huku akimtendea kwa ukatili. Mtoto huyo huyo aliyekuzwa kibazazi pasipo nidhamu hata chembe anapoenda shuleni huwa hana utii wowote. Hivyo walimu ambao ni walezi wenza hujikuta wakiwa na wakati mgumu kulikabili hilo.

Hebu fikiri kuhusu mwalimu wa kidato cha tano ambaye amemweleza mwanafunzi achukue adhabu fulani, mwanafunzi akakataa na kuanza kumshambulia kwa ngumi mwalimu, je mwalimu kama mhanga achukue hatua gani?

Kuna mambo mengi ya kujadili kwa kina kama jamii na kuyapatia ufumbuzi wa kina pasipo kumtupia lawama mtu ama kundi moja.

Mwalimu hufanya kazi kubwa lakini amekuwa hathaminiwi wala hatetewi kwa jambo lolote; kwanza hufanya kazi katika mazingira magumu, malipo kidogo, pasipo marupurupu hata chembe.
 
Kutengenezwe Magereza ya shule, mwanafunzi akikosea hasa kosa la utoro na ukosefu wa nidham awekwe humo kwa kifungo cha wiki hadi mwezi kurekebishwa, vijana kibao wako mtaani wapewe training ya kutoa adhabu ya watukutu hawa

'HOW MUCH IS TOO MUCH?'
 
Ni kweli kabisa ndugu, kwani hao wanaolijadili hili jambo kimzaha wangepewa fursa ya kukaa na hao watoto kwa wiki moja tu hakika wangekonda.

Halafu jambo jingine utundu wa watoto unatokana na mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa mfano, huku DSM maeneo ya Uswahilini kwetu utamkuta mzazi anamtukana matusi makubwa na ya nguoni kwa mtoto bila kujali umri huku akimtendea kwa ukatili. Mtoto huyo huyo aliyekuzwa kibazazi pasipo nidhamu hata chembe anapoenda shuleni huwa hana utii wowote. Hivyo walimu ambao ni walezi wenza hujikuta wakiwa na wakati mgumu kulikabili hilo.

Hebu fikiri kuhusu mwalimu wa kidato cha tano ambaye amemweleza mwanafunzi achukue adhabu fulani, mwanafunzi akakataa na kuanza kumshambulia kwa ngumi mwalimu, je mwalimu kama mhanga achukue hatua gani?

Kuna mambo mengi ya kujadili kwa kina kama jamii na kuyapatia ufumbuzi wa kina pasipo kumtupia lawama mtu ama kundi moja.

Mwalimu hufanya kazi kubwa lakini amekuwa hathaminiwi wala hatetewi kwa jambo lolote; kwanza hufanya kazi katika mazingira magumu, malipo kidogo, pasipo marupurupu hata chembe.
Dah!!! Hakika umeongea hoja ya msingi sana!!! Kuna vitu nmejifunza hakika umenena!!

Kikubwa ni muda utasema wacha walimu wetu leo wabebeshwe lawama hizi ila matokeo yake tutayaona!!!!

MWL huyu huyu ambaye kama ulivyosema mazingira ya kazi ni magumu ukijumlisha na watoto wenyewe kwann aonekane ndo mwenye makosa!???

Hivi tunaolalamika sana japo siseme viboko vtumike je tumelelewa mazingira yepi majumbani kwetu???

Ukichunguza hata hawa viongozi wanaoongea kwa ujumla hili suala walichapwa viboko teena VIBOKO acha vya hivi lakn kasahau??? OK sawa tuwalaumu lakn tuelewe kisaikolojia hawa walimu ku-popularize madhaifu yao tena ktk media kuna madhara makubwa sana but nisieleweke natetea hapa ila

1 mazingira wanayofanyia kazi jumlisha na hii ishu inawafanya wote wawe ktk kundi moja na kwa maana hyo wataonekana dhaifu sana ktk jamii na matokeo yake wanakuwa inferior. Matokeo yake tutayaona hapa

2 Hawa tukiendelea kuwaponda ktk ujumla tunawafanya waseme acha yaende hvyo hvyo maana yake wanaweza kujitoa ktk malezi ya wanfnz ipasavyo matokeo tutayaona

3 Kuhusu matamko ambayo yanakuwa kama adhabu sizani kama walimu ambao ni wahusika wanalipokea ktk miktadha lengwa yaani inawapain kwamba adhabu wamei feel sina hakika koz wao wanaweza kujitengenezea mazingira ambayo yataleta uhasama kati ya serikali, watoto na hata jamii jamn hapa watoto watakuwa wamewaharibu kabsa ,,,kuna watoto ni vichwa maji hivyo kwao hii wataitumia kama siraha kumbe wanaangamia na wazazi mmeshangilia ..shauri yenu
Kama ulivyoshauri kinachotakiwa n meza ya pamoja na kuangalia suluhisho la kudumu na isieleweke kwamba kundi moja ndo lilaumiwa kumbukeni makuzi ya mwanafunz yapo ktk makundi yasiyopungua matatu,, walimu,, jamii,, na wazazi wenyewe sasa tutoe mentality hyo na bnafs nashauri wajaribu kutumia vkao vyao na maofsa elimu kuwaonya wale wanaokiuka sheria na kutoa adhabu kama tajwa itasaidia

Asante mkuu ukweli nmejifunza ktk maoni yako thank you sana!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimesoma seminary. Hakuna fimbo wala adhabu ya aina yoyote lakini nidhamu ni ya hali ya juu. Timetable inafuatwa bila shuruti hupotezi hata sekunde moja.

Kama ni muda wa sala upo chapel kwa wakati, muda wa masifu, compreto, muda wa kazi, muda wa michezo. Kila kitu lazima ushiriki on time.

Tulikuwa na handbooks, hizo ndio zilikua muamuzi wako kwamba ubaki kwenu mwisho wa semester au urudi shule. Hizo handbook zina mambo kibao lakini zina sehemu ya discipline, siku ukifanya kosa tu sijui hujashiriki michezo, ume dodge chapel, huja chakula, hujashiriki usafi, umechelewa kula au chapel.

Basi inachukuliwa handbook linaandikwa kosa na tarehe unapewa kitabu chako unasepa kama hakijatokea kitu. Ukivurunda tena kama kawaida msaafu unajazwa unaondoka zako.

Mwisho wa semester kuna mchujo sasa, wa academic performance na discipline. Lazima vi balance, yani mzani usiegemee upande mmoja.

Hapo lazima discipline na performance viwe sawa. Ukiwa hata umepata wastani wa A lakini handbook imechafuka kidogo tu basi ni kwaheri. Ukiwa handbook iko safiii lakini wastani C basi kwaheri.

Unakuta tunaanza skuli watu 60+ ila kumaliza hatufiki 30. So mimi naona haya mambo ya viboko ni ujinga tu. Kuna njia rahisi sana za kudeal na hawa watoto

Nakubaliana kabisa na wewe kuhusu utaratibu wa baadhi ya shule za seminari, ambazo hazitoi adhabu ya viboko lakini wakawa na adhabu mbadala lengo likiwa ni lile lile la kumfanya mtoto akue katika maadili mema.

Kwangu mimi pia nimebahatika kusoma seminari lakini pale kwetu viboko vilikuwepo na recta wetu hakuwa na mchezo katika hilo hata kidogo.

Kitu kingine ni lazima uangalie aina ya watoto wanaochaguliwa kusomea kwenye shule za seminari na wale wanaosoma katika shule za kawaida za serikali. Kumbuka lengo kubwa la seminari hasa za Kikatoliki ni kuwaandaa mapadri hivyo humchagua mwanafunzi kwa kufuata vigezo vingi sana, kama vile; historia ya maadili ya familia anakotoka, ushiriki wa wazazi katika ibada, utii wa mtoto katika familia na jamii kwa ujumla, ushiriki wake katika mashirika ya kidini kama vile virafra, mt. Aloice etc. Sasa utaweza kuona utofauti kati ya seminari na shule nyingine za serikali.

Hapo vile vile umesema seminari mnaweza mkaanza 60 mkamaliza 30 sasa wewe unafikiri hao 30 wanaofukuzwa huenda wapi. Hao huenda kuendelea na elimu kwenye shule za serikali/za kawaida. Kumbuka jamii ina jukumu la kuhakikisha kila mtoto anapata elimu inayofaa bila kujali tofauti za kipato, kirangi, kidini, kikabila na kiutimilifu. Suluhisho hapa sio kumfukuza mwanafunzi bali ni kutafuta njia ya kuboresha maadili yake na kumfanya aendelee na elimu ambayo ni haki yake ya msingi.

Tulete mapendekezo ya namna tutakavyotatua tatatizo la ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya wanafunzi pasipo kutajataja seminari ambazo si mfano mzuri wa kulea watoto mchanganyiko.
 
Back
Top Bottom