African Believer
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 436
- 425
- Thread starter
- #81
Ni kweli kabisa kile kinachoonekana kwenye video clip ni matokeo ya mchakato unaoanzia mbali, na hilo hutokana na ukosefu wa maadili kwa wanafunzi na ukosefu wa busara kwa mtoa adhabu (kutoa adhabu akiwa na hasira)
Kabla hamjafika huko kwenye kumsimamisha masomo, lazima kuna mahali mlianzana na huyo mwanafunzi. Fikiria umemkuta mwanafunzi na kosa linalostahili achapwe viboko, unamwambia nyoosha mkono nikuchape, anakwambia mwalimu mi hunichapi. Unaona isiwe tabu, unamwambia tangulia ofisini, ukidhani labda kule kwa kuwa mpo walimu wengi ataogopa na utamchapa kirahisi, nako ukifika anakudishia vilevile. Mwalimu anapanic, na kuanza kumchapa dogo randomly, dogo anakamata fimbo na kuivunja. Sasa hapo ndio ile mitama , mateke na mangumi unayoiona kwenye video za kurekodiwa inapoanzaga. Mwalimu tayari anajazba, dogo nae ni nunda by nature, hahahahahaa yajayo lazima mfumbe macho kwakweli.