Hiyo 50400 ukienda polyclinic hela ya kumuona specialist, vipimo kama viwili na dawa imeisha...haina ukubwa wowote mkuu.


Kwa kifupi hiyo NHIF mostly inajiendesha kwa hasara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kimsingi kabima kanasaidia sana, ila tu wajidhatiti kwenye mifumo yao ya uendeshaji waepuke kudanganywa na watoa huduma pamoja na wateja wao
 
Samia unahujumiwa na watendaji wako . shtuka
Mzilankende Chap Angemtimua Kazi Huyo NHIF
Nakumbuka Mwijage Aliambiwa Mfute Kazi DG Brela
Akagoma, Jiwe Akasema Ikifika Saa Kumi Bado
Nakufuta Wewe Waziri
 
NHIF kumejaa watu wenye primitive thinking!
Tanzania sijui tuna shida gani, Yaani watu hata wangesoma vipi lakini wanakuwa wajinga wajinga tu!
Yaani nikate Bima ya afya bado nipangiwe mambo ya Kijinga jinga ya kufuata.
Mimi nadhani hawajui hata maana ya Bima ya afya.
Watendaji wa huo mfuko wanachojua wao ni kutumbua fedha za mfuko baaasi!
 
Baada ya wananchi kupigia kelele mabadiliko ya mfuko wa bima ya afya, hatimaye NHIF wamesitisha mabadiliko hayo.

Hii ndio nguvu ya mitandao ya kijamii

==============

Pamoja na hivyo kumetolewa taarifa mbili ambazo ni wazi zina onesha wahusika hawakujipanga, taarifa ya kwanza imetolewa na NHIF wenyewe wakionesha kuwa walikuwa na utaratibu mpya, lakini baadaye wameona umeleta utata wameufuta.

Dakika 20 baadaye taarifa ikatolewa na Wizara ya Afya kuwa wamesitisha utaratibu huo mpya, ikumbukwe kuwa awali hakuna taasisi yoyote kati ya hizo mbili iliyojitokeza kuzungumzia kuhusu utaratibu mpya.

Inamaanisha kuwa baada ya presha kuwa

NHIF inaweka limitation ya matibabu ya wanachama na wategemezi wao.
Kama ni hivyo nini maana ya BIMA YA AFYA?
Hii inamaana kuwa mtu akiumwa zaidi ya mara tatu kwa mwezi lazima awe na akiba ya fedha ya matibabu na ya baadhi ya vipimo.
( Kukata mshahara wa mtu, hawasemi kama mtu asipotumia bima kwa mwaka au zaidi watapunguza makato). Watu wamekatwa BIMA zaidi ya miaka mitano bila kutumia HUDUMA( halafu anakuja kuumwa serious mna mpa limitation ya matibabu, "this is unfair".)
 
Kama wanataka kuthibiti basi isiwe lazima kwa watumishi wa umma kujiunga na mfuko. Huwezi kulazimisha watu kujiunga na mfuko halafu unakuja na masharti magumu.
Monopoly haijawahi kuchochea quality improvement wala competition kwenye huduma. NHIF alitakiwa kuwa mtoa huduma kama zinavyofanya health facilities za serikali ila yaonekana NHIF amekuwa mfanyabiashara tena asiye na ushindani kwani ana wateja(watumishi wa umma) hawana kimbilio na hii inawapa NHIF jeuri na kutokujali wateja. Serikali itaisaidia sana NHIF itakaporuhusu watumishi wa umma kuchagua kampuni ya bima ya afya anayopendelea; NHIF watajifunza na watajali wateja na huenda baadaye wakawa wazuri zaidi. Kwao kwa sasa mteja sio mfalme bali ni kidampa tu. Naunga mkono hoja.
 
Hiyo 50400 ukienda polyclinic hela ya kumuona specialist, vipimo kama viwili na dawa imeisha...haina ukubwa wowote mkuu.


Kwa kifupi hiyo NHIF mostly inajiendesha kwa hasara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inajiendesha kwa hasara sababu imekumbatia watu.
Mfanyakazi hata kama analipwa 370 kwa mwezi atatibiwa sawa na yule wa 3mil kwa mwezi wakati wanatofautiana makato
 
Tulishasema hapa kuwa yale maamuzi yalikua ni layman solution.

Eti mgonjwa anapangiwa idadi ya siku za kuumwa kwa mwezi 😂
 
Back
Top Bottom