Huyu bwana ni msanii, na zaidi ya hapo anaamini watanzania walio wengi hawatunzi kumbukumbu yaahadi za viongozi wao; kutokana na hayoNgelenja ni mwepezi kusema lolote ili mradi siku ipite.
Hii ngoma Ngereja sijui huyu mkwele kaiokota wapi ? Migao kibao, mafuta bei juu, umeme bei juu, yote haya ndani ya wizara yake ila yeye anacheka tu haoni kama ni tatizo!
Ngoja tu na hizo dhihaka zake miguu isije ikaota matende.
Maana kwa mgomo wa Wafanyakazi Tanzania hapo ni kwamba watu bila shaka watakua wanatetea usallama na uhakika wa kula ya watoto hapo na ndiyo maana napata hofu sana mimi.
Ogopa sana ugomvi wa kukupambanisha na mtu anayepigania KULA YAKE.
Huyu Mgaya aache kuwachanganya wafanyakazi. Toka aabandon ule mgomo wa May mimi sina imani naye tena. Actually, wafanyakazi ilibidi wamtoe watafute kiongozi bora zaidi ya huyu jamaa. Mgaya ni muoga na hawezi kuandaa kitu kama hicho. Anabeep tu!!