Ngeleja akiri kazi aliyopewa ngumu

Huyu waziri Ngeleja naye scandal kibao!... habari zake nzito sana huko alikotokea yaani hata nashindwa la kusema!...
Hii ndio sababu kubwa inayonipa wasiwasi kubwa na uwezo wa JK kuongoza - hawa WATU WAKE!

Kwa hiyo mkuu bado unaamini kwamba yeye ni tofauti na hao watu wake? Kwa maoni yangu nafikiri yeye ni worse kuliko hao aliowateua!
 
huo ushauri ulikusudiwa uwe public amshauri rais na watendaje nn cha kufanya ?


mbona mna kimuhe muhe nyie


Kwa nini huo ushauri usiwe public? Wanataka kuficha nini tena? Sisi ndio wenye kumiliki hizo rasilimali na pia ndio tuliolalalamika kwamba rasilimali zetu hazitunufaishi Watanzania na ndiyo sababu kubwa ya JK kuunda tume hiyo. Hivyo tuna kila sababu ya kufahamishwa kwamba ni ushauri gani uliotolewa na Ngeleja ili tuamue kama tunafikiana na ushauri huo au la
 
Kitila Mkumbo,
Mkuu unayosema kweli kabisa lakini yanibidi kukiri kwamba huwa nashindwa kumweka Kikwete ktk kundi hili kwa sababu sina tetesi mbaya kuhusu yeye zinazohusiana na CHUKUA CHAKO MAPEMA isipokuwa tu huo mradi wa bomba la mafuta kwenda Mwanza ambao sidhani kama tayari wale Waarabu wameisha pewa. Fununu zinasema Kikwete ana fungu lake ktk mradi huo akimtumia mke wa pili!....hata hili sina uhakika nalo.

Kisha kwa jinsi Kikwete anavyojilinda na mavazi yake ya siku hizi kuvaa bullet proof na kadhalika linanipa shida sana, Kikwete yule aliyekuwa akipita mitaani hadi Kariakoo na kufahamu mengi ya mitaani sii huyu tena....Ana woga fulani ndio maana haishi kwenda nje! Inaonyesha wazi kama vile ni mtu aliyelishwa limbwata na kuwa zuzu badala ya kuwa mshiriki mkubwa wa Ufisadi. Hii inanipa shida sana kusema he is worse than hao anaowachagua kwa sababu hao wote wana akili zao timamu na wanafahamu wanayoyafanya...
Kwa mfano nikimtazama Mahita na yale yote aliyoyafanya alitakiwa awe jela, kutoa mfano kwa viongozi wetu lakini yupo huru na anatisha bado. Kutokuwepo kwake jela hakuwezi kunipa imani kuwa Kikwete pia alishiriki ktk Ujambazi nchini isipokuwa kayafumbia macho kwa msemo wa kiswahili kuwa yaliyopita sii ndwele!..Haya cha ajabu basi, yule alokuwa mkuu wa Polisi Moshi baada ya Mahita kutoka huko alikabidhiwa zana zote na anajulikana kwa machafu yake lakini huyu yupo bado ktk system!... na anatisha vile vile!..
Hapa mkuu nashindwa kabisa yaani nimechoka lakini sidhani kama Kikwete ni fisadi isipokuwa MWOGA!
 
ukiona mtu anasifia mvua imemnyea! kwa hivyo huo woga wa jk siyo bure una sababu zake nazo ni kwa anaogopa kuilaumu mvua iliyomnyea
 
Pengine nami ningependa kuwa rais, ila nikifikiria jinsi ya kupata baraza la mawziri nachookaaaa!!!!

Sioni pale bungeni, kama unaweza kupata watu safi japo kumi!!!! wengi wana harufu ya ufisadi!!!!
 
Mkandara,

'Yaliyopita si ndwele tugange yajayo' ni msemo ambao ulikuwa maarufu na valid katika mwaka 47 lakini 2008 msemo huo umepitwa na wakati. Mara nyingi yaliyopita yanaashiria yajayo...:) Just thinking aloud
 
Sikuwahi kuwa na imani na JK maana kachaguliwa kuwa rais bila ya kuwa na record .Si wakati huo hata sasa na ndiyo maana simwamini hata waziri wake mmoja maana ni lazima ni wale wanao nukia harufu ya JK .JK ni mnafiki hili mlijue .Ushahidi ni jinsi alivyo mchezea Chenge na hata Lowasa.Alijua issue nzima ya Chenge na SFO lakini bado akampa uwaziri .Mnafiki na mnaweza kusema si mla mulungula lakini akawa anawatumia watu wake kufanya mambo .JK haaminiki maana hata Urais aliuchukua ili kutimiza ahai ya kuwa Rais na si kuinua Tanzania .
 
Huyu nae uvivu tu au yalioandikwa humo hayaendani na yeye alivyokuwa inataka iwe!kweli hii nji hii tumekwisha!ila tukaze belt hii vita na mafisadi lazima tuvishinde!we will never walk alone!Solidarity forever!
 
Huyu waziri Ngeleja naye scandal kibao!... habari zake nzito sana huko alikotokea yaani hata nashindwa la kusema!...
Hii ndio sababu kubwa inayonipa wasiwasi kubwa na uwezo wa JK kuongoza - hawa WATU WAKE!

Waziri Ngeleja ni mtendaji mzuri sana japo hana uzoefu mkubwa katika utendaji wa kisiasa.lakini kubwa nalotaka kuliweka bayana historia ya Ngeleja inaanzia PWC na hatimaye Vodacom ambako aliwahi kufanya kazi.Kutokana na taaluma yake ya uanasheria na kazi alizokuwa anazifanya katika makampuni hayo hakuna habari nzito inayoweza kumhusu labda kama habari nzito inahusu mambo yake binafsi nje ya kazi ambayo binafsi nafikiri haziwezi kuwa habari nzito.Scandal yoyote ya Ngeleja inaweza kuhusishwa pengine na ukaribu alionao na RA (Mb-Igunga) kwasababu ni mmoja wa waliofanikisha safari yake ya kisiasa vinginevyo nafikiri tumjudge huyu kijana kuanzia pale alipopewa jukumu la kuwa naibu waziri na hatimaye waziri katika wizara ya nishati na madini.
 
Ngeleja amepoteza sifa za uwaziri

Tahariri
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ni mmoja wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa Mkoa wa Mwanza, walioitwa kukiongezea nguvu chama hicho katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Busanda, wilayani Geita.

Ngeleja katika kutimiza kazi hiyo aliyopewa na chama chake, pamoja na mambo mengine, amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini, akitoa kauli zifuatazo;

Mosi, jana baada ya kukimbiwa na wachimbaji wadogowadogo wa madini aliokuwa anawashawishi kumchagua mgombea wa CCM, alinukuliwa akiwaambia wachimbaji hao kwamba atawanyima vibali vya uchimbaji madini.

Pili, siku chache nyuma, akihutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro, aliwaambia wananchi hao kwamba, mgombea ubunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Finias Magessa, hawezi kuwaletea umeme wa jua kwa sababu yeye (Ngeleja) kwa nafasi yake kama Waziri wa Nishati na Madini, ndiye anayetoa kibali.

Kwetu sisi wa Tanzania Daima Jumatano, kauli hizi za Ngeleja, zina tafsiri kuu zifuatazo;

Mosi, ni kauli za vitisho dhidi ya wananchi walioonyesha dalili za wazi za kutokubaliana na yeye pamoja na chama chake katika kampeni hizo.

Pili, ni kielelezo cha matumizi mabaya ya madaraka yake ya uwaziri (abuse of power). Ukweli ni kwamba hakupaswa kutumia cheo chake kuwatishia wachimbaji hao, kwamba atawanyima vibali vya uchimbaji, eti kwa sababu wamekataa kumuunga mkono yeye na chama chake.

Tatu, tunaelewa kuwa Ngeleja ni mwanachama wa chama cha siasa na hata uwaziri wake ni matokeo ya kuwa mbunge kupitia CCM, lakini sawa na ilivyo kwa viongozi wote wa kiserikali, anapaswa kutumikia wananchi wote bila kujali wanaunga mkono chama chake au la.

Nne, tunalazimika kuamini kuwa Ngeleja si waziri wa Watanzania wote, bali ni wa CCM, na kwa mantiki hii, dhamira yake ni kusimamia maliasili ya nishati na madini ya nchi hii, kwa maslahi ya wale tu wanaokiunga mkono chama chake. Huo si uongozi bora.

Tano, kauli yake kwamba Magessa akiwa mbunge hawezi kuleta umeme wa jua, kwa sababu yeye ndiye anayetoa vibali, haina tafsiri nyingine zaidi ya kuuuleza umma kuwa Magessa akiwa mbunge, yeye atatumia madaraka yake ya uwaziri kuzuia mradi wa umeme wa jua jimboni humo, kwa sababu tu atakayekuwa anatekeleza mradi huo ni mbunge wa CHADEMA.

Sita, kwa tafsiri sahihi zaidi, Ngeleja atakuwa tayari kukwamisha maendeleo ya umeme wa jua ili wananchi wa Busanda waendelee kuwa gizani, awakomoe na kuwakomesha kwa sababu watakuwa wamechagua mbunge kutoka CHADEMA.

Kwa sababu hizo tulizoorodhesha hapo juu, tunaamini kuwa Ngeleja hawezi kutumikia wananchi wote kwa uaminifu. Tunachokiona kwake ni kwamba, anaiona CCM kuwa bora zaidi kuliko taifa la Tanzania.

Kwa kauli zake hizo, ni wazi kwamba atakapoona CCM inaangamia, yeye atakuwa tayari kuwaangamiza Watanzania (kwa kuwanyima vibali), ili tu chama chake kipone. Waziri kama huyu hatufai Watanzania.

Aidha, Ngeleja amedhihirisha kuwa ni dikteta, hana busara, ustahamilivu, utashi na ukomavu wa kisiasa, amepoteza sifa zote za msingi za uwaziri, hivyo ni wakati muafaka kwa Rais Jakaya Kikwete kuonyesha busara na hekima kwa kumwondoa mara moja kutoka kwenye wadhifa huo.

Tunaamini kuwa Rais Kikwete hatawaangusha Watanzania.
 
Kwa hiyo alienda pale kama waziri au mwanachama wa CCM? kazi sana kutofautisha hivi vitu hasa kwenye nchi hii ya chama kimoja, nadhani is high time for political parties to find a way of pressurising these leaders kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa, otherwise Chadema wakishinda mwakani , CCM watalalamika the same mwaka 2013! wakati waziri mkuu Zito akienda kufanya kampeni ya mtu wa chama chake! jamani Ngeleja nani wakati JK naye anafanya haya haya kila siku?
 
amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini, akitoa kauli ...
Amenukuliwa na vyombo mbalimbali, chombo gani, kasema nini? Weka maneno ya Ngeleja hapa tuyaone.

Maana si tunajadili kauli tata ya kiongozi. Niwekee kauli hiyo niione basi, halafu tutajadili. Press tunayo...
 
Amenukuliwa na vyombo mbalimbali, chombo gani, kasema nini? Weka maneno ya Ngeleja hapa tuyaone.

Maana si tunajadili kauli tata ya kiongozi. Niwekee kauli hiyo niione basi, halafu tutajadili. Press tunayo...

Dilunga,
Hii ni editorial. Na editor anayo haki ya kusummarize aliyosema Ngeleja bila kuweka quotes. Ingekuwa ni direct reporting ningekuwa upande wako.
 
Dilunga,
Hii ni editorial. Na editor anayo haki ya kusummarize aliyosema Ngeleja bila kuweka quotes. Ingekuwa ni direct reporting ningekuwa upande wako.

Okay Jasusi, ingekuwa direct reporting ungekuwa upande wangu, poa, kumbe kwenye issue ya Lukuvi tulikuwa tunashikana mashati bure tu ndugu yangu? Ukweli unaujua kwamba they'd to quote. Duuu, noma kweli hizo bro.
 
Dilunga,
Hii hapa ripoti na quotes za Ngeleja. Amua mwenyewe:

Kwa mara ya kwanza tangu alipowasili katika kampeni hizo kukiongezea nguvu chama chake, jana Ngeleja alijikuta katika wakati mgumu baada ya kukimbiwa na wachimbaji wadogo wadogo katika mkutano wa ndani wa chama hicho uliokuwa ukifanyika katika mgodi wa dhahabu wa Lwamgasa.

Hatua ya Ngeleja kukimbiwa na wachimbaji hao ilitokana na kauli yake kuwa, kama watashindwa kuichagua CCM watanyag'anywa leseni na kufutiwa usajili wa vitalu vyao.

Katika mkutano huo ambao ulifanyika katika Shule ya Msingi Mwenge, Ngeleja alisema CCM ndiyo yenye wezo wa kuchukua hatua zozote zinazostahili kuwaendeleza wachimbaji, wakiwamo wa migodi mikubwa kama vile Mererani, North Mara na Geita Gold Mine.

"Napenda kuwaambia ndugu zangu, leo nimewaita hapa kutaka kuwaambia kwamba, tuna kazi moja tu ya kuhakikisha mnachagua CCM katika uchaguzi ujao, sasa nawaambia kama hamtafanya hivyo, tutahakikisha tunawanyang'anya leseni kwani CCM ndiyo yenye serikali," alisema Ngeleja.

Alisema wachimbaji wadogo wadogo wamekuwa na tabia ya kupinga sera za CCM eti kwa madai kuwa imekuwa ikiwakandamiza, jambo ambalo halina ukweli wowote.

Katika hali inayoonekana kuwa vitisho, Ngeleja alisema kama CCM itashindwa kwenye uchaguzi huo, wachimbaji hao watashukiwa kwa nguvu zote na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuona kama kweli wanalipa kodi ya serikali.

"Moja ya mkakati ambao tumeandaa ni kwamba kama CCM haitashinda, TRA itakuja hapa kwa ajili ya kuhakiki kama kweli mnalipa kodi ya mapato, ikiwa ni kinyume chake mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya serikali," alisema Ngeleja.

Kauli hiyo ilionekana kuwaudhi wachimbaji hao ambao walianza kuondoka mmoja mmoja ndani ya ukumbi na kumwacha Ngeleja na viongozi wa CCM aliokuwa ameambatana nao kwenye kikao hicho.


Baadhi ya wachimbaji hao waliiambia Tanzania Daima Jumatano kuwa, huo ni unyanyasaji mkubwa na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali.
 
Back
Top Bottom