New Habari (2006) Ltd imefulia... Nani alaumiwe?

Media House hii itaendelea kupumulia kwa mashine ICU hadi lini? habari zilizopatikana kutpoka hapo zinasema mmiliki, "anayesadikiwa" kuwa ni RA, hataki kutoa hata senti moja kusaidia kulipa mishahara kwani kuna ukata wa hali ya juu.

Wafanyakazi hawajalipwa miezi miwili sasa (Feb na Mar) na yote hii ni tangu mdosi Bobby ashike u-CEO na Muhingo kuwa Mhariri Mkuu (Managing Editor). Bobby ni customer mkuu wa ma-casino ya Dar, na Muhingo ni mlamba viatu mkuu wa RA, na ambaye yeye, Balile na Manyerere kazi yao kuu ni kumsafisha huyo muajiri wao. Katika hali hii kuna biashara hapo?
 
TRA wanacheza shere tu, hawana ubavu kuitia kufuli kwa sababu RA kaiweka serikali mfukoni. RA ana vimemo vya vigogo wa CCm waliochukua hela za Kagoda kufanyia kampeni za 2005.
 
Wafanyakazi wengi wanamlilia yule mama mchapakazi, Rosemary Mwakitwange aliyekuwa CEO kabla ya Bobby. mishahara ilikuwa tarehe 26 na aliwahi kuwatangazia kuwa endapo tarehe 26 ATM hazitemi basi apewe gtaarifa mara moja na siku hiyo atabwaga manyanga. Kwa karibu miaka miwili hilo halikutokea.
 
iyeela! iyeela! ccm nambari wani, hizi habari zinanifurahisha sana, huwa namtakia rostam kila baya kasoro afya yake, akishindwa kuendesha hii media yake, itakuwa nafuu kubwa kwa watanzania kwa kuwa hakutakuwepo tena na magazeti ya bla bla mtaani. huenda ana ukata baada ya mrija wa richmond na epa kukatika
 
iyeela! iyeela! ccm nambari wani, hizi habari zinanifurahisha sana, huwa namtakia rostam kila baya kasoro afya yake, akishindwa kuendesha hii media yake, itakuwa nafuu kubwa kwa watanzania kwa kuwa hakutakuwepo tena na magazeti ya bla bla mtaani. huenda ana ukata baada ya mrija wa richmond na epa kukatika
.
Mwakimbi, usifurahie kufa kwa magazeti ya Mtanzania kwa sababu tuu ya chuki dhidi ya RA, hebu fikiria na maisha ya 100+ employees ambao hapo ndio tegemeo lao, fikiria readership yao ambayo itakosa something of value no matter how little. Ukiwa ni msomaji mzuri wa magazeti, lazima utakubaliana na mimi, ukiondoa ukibaraka wao, kujikomba ama kuendekeza njaa, Muhingo, Manyerere na Balile, ni wanataaluma mahiri waliojikita kwenye kujikita kuwasafishia njia mafisadi. Pia wako waandishi makala wengi ambao wanayatumia magazeti hayo kama reaching out medium and have nothing to do with RA.

Nashauri tuwe more pro- active, tufike mahali tukubaliane kutokubaliana, to manage divesity yetu kwenye kumeza kidonge kitamu tunachokipenda na kulazimika kumeza kichungu ambacho hatukipendi lakini ndio dawa yenyewe, naombea magazeti ya Mtanzania yadumu, kama ninavyoliombea gazeti la Uhuru lidumu pamoja na U CCM wake, sambamba na gazeti la Tanzania Daima, pamoja na Uchadema wake, ndivyo hivyo lidumu Mtanzania na utetezi wa mafisadi, na IPP-Media na vita dhidi ya ufisadi.

Kwa mtu anayebobea kwenye total impartiality, samaki yoyote ni samaki, kama papa ni samaki na nyangumi ni samaki, wote samaki, hivyo papa akiwa ni fisadi, na nyangumi naye fisadi, wote ni mafisadi, labda dagaa tuu ndio samaki lakini si fisadi.
 
iyeela! iyeela! ccm nambari wani, hizi habari zinanifurahisha sana, huwa namtakia rostam kila baya kasoro afya yake, akishindwa kuendesha hii media yake, itakuwa nafuu kubwa kwa watanzania kwa kuwa hakutakuwepo tena na magazeti ya bla bla mtaani. huenda ana ukata baada ya mrija wa richmond na epa kukatika
mimi na wewe tunafikra sawa, natamani kila baya limuangukie RA
 
Biashara ya magazeti kwa Tanzania ngumu jamani. Watanzania hatusomi. RA aliyanunua magazeti haya na baadhi ya wamiliki wake (akina Salva wa Ikulu) kwa malengo maalum ambayo yalitimia. Haya sasa hayahitajiki tena. RA hafanyi kazi kwa hasara. Magazeti yake haya yatakufa tu. Mzee Mengi yeye ameyapunguza sana magazeti yake ingawa hakuna nafuu yoyote hadi sasa.
 
Hii mbona nashindwa kabisa kuielewa...huu ni mwaka wa Uchaguzi, RA ni mmoja wa Wagombe na Chama Chake kinahitaji kuungwa mkono na kupigiwa debe Magazeti yote yakiwamo ya New Habari Corp. Halafu eti mnasema TRA wanataka kuitia kufuli New Habari..??

Au kuna mlengwa mwingine hapa anatafutwa?
 
Hii mbona nashindwa kabisa kuielewa...huu ni mwaka wa Uchaguzi, RA ni mmoja wa Wagombe na Chama Chake kinahitaji kuungwa mkono na kupigiwa debe Magazeti yote yakiwamo ya New Habari Corp. Halafu eti mnasema TRA wanataka kuitia kufuli New Habari..??

Au kuna mlengwa mwingine hapa anatafutwa?

ili itakapotokea watasema... mbona na..
 
Biashara ya magazeti kwa Tanzania ngumu jamani. Watanzania hatusomi. RA aliyanunua magazeti haya na baadhi ya wamiliki wake (akina Salva wa Ikulu) kwa malengo maalum ambayo yalitimia. Haya sasa hayahitajiki tena. RA hafanyi kazi kwa hasara. Magazeti yake haya yatakufa tu. Mzee Mengi yeye ameyapunguza sana magazeti yake ingawa hakuna nafuu yoyote hadi sasa.

Malengo hayajatimia. Kufuatanana na ratiba yao, EL (swahiba wa Jk na RA) anatakiwa ashike dola 2015, na kila dalili hiyo hakuna tena. Isitoshe magazeti hayo yalishindwa kabisa kumuokoa EL from Richmond na ikabidi ayabwage manyanga midway. Aidha magazeti hayo yanaonekana kushindwa kumtetea kwa nguvu za hoja, RA kutokana na kashifa ya kagoda, kilichobakia ni ubabe tu wa vyombo husika vya serikali ya JK kutomshughulikia kikamilifu. Ni rahisi sana kuwapata waliochukua hizo hela kutoka akaunti za CRDB (zilikopelekwa kutoka BoT) kwani hatujaambiwa iwapo wakuu husika benki hiyo "ya wazalendo" (sic!) walihojiwa kwa lengo la kueleza walizilipa hizo pesa kwa akina nani.

Ni manguvu tu yanatumika kuzima suala hilo kumuokoa RA kwani kama CRDb wangekuwa wamemlipa mwingine saa hizi mtu huyo angekuwa na kesi. WaTz tunafanywa mafala sana na utawala huu.
 
Ha ha ha !!! Wameanzia kwa RA kama kiini macho!!! Kuna mahali wanalenga!!! Tusubiri kule kwa mzee wetu wa VIKOBA na mafisadi Pa pa pa pa pa pa !!!
 
Sikizeni
hiyo ni danganya toto ili media hausi nyinginezo waanze kukusanya pichu zao na kuzifutika kabatini.

Pia hii tabia ya agencies za serikali kutumia kampuni binafsi kwa kazi za umma ilhali tunalipa kodi zetu ili polisi wapate mishahara. je huu si ufisadi huu kwa sura ya kuhalalishwa kisheria??
 
Kama Kweli TRA wako serious basi kuna media house nyingi tuu zitakumbwaa na adha hii.. Vipi IPP mko sawa wasije kumchafua Mwenyekiti??????
 
Rostam amuumbua Boniface Makene

Yule mwandishi makini wa zamani ambaye aliliasi gazeti la Mwananchi na kwenda kujiunga na kundi la mafisadi sasa ameonja joto la jiwe baada ya kusimimishwa kazi takribani wiki moja sasa.

Kwa mujibu wa Muhingo Rweyimamu aliyemsimamisha kazi ni kuwa mwandishi huyo ni mkosefu wa adabu na amekuwa mara kwa mara akijifanya kuwa ana mawasiliano na Mh Rostam ambaye ndio mmiliki wa gazeti hilo.

Aidha, alisema kuwa hata Mh Rostam amebariki uamuzi huo kwa kudai kuwa Makene hawezi kuendelea kuwa kwenye gazeti hilo kwa kuwa amekuwa ni mlevi sana kwa sasa na anaandika meseji za ajabu ajabu zisizo na heshima wala staha…..

Mara kwa mara Makene alikuwa anajisahau na kudhani yeye ni sehemu ya hawa mafisadi na kujikuta akijifanya kuwapenda sana kuliko hata ambao aliwakuta na hiyo ndio zawadi aliyopewa kwa kuwa zawadi kama hio huwa wanapewa watu kama yeye wanaodhani kuwa kuna urafiki kati ya tajiri na masikini" Alisema mwandishi mmoja wa gazeti la Mtanzania anaetokea mkoa wa kigoma.

Aidha wachunguzi wa mambo wanabashiri kuwa anaefata katika utaratibu huu wa kuondolewa kazini baada ya kutumika sana na mafisadi ni Bashe na Deodatus Balile……Aidha asubuhi hii Muhingo alionekana akichekelea ofisini kwake jinsi ambavyo wameondoa tatizo moja.POLE KAKA MAKENE.
 
Labda na yeye alikuwa anataka siku za usoni apewe lawalawa kama Salva.
 
Je, urafiki wa Muhingo na Rostam nao ni wa kudumu au ni mwendelezo wa sinema za urafiki wa matajiri na masikini? Au Muhingo ni tajiri? Kwani Salva alipewa lawalawa na Rostam? Ule ukuta pale umevunjwa na nani, maana naona wamebaki uchi, ukuta wote pale mbele pwaa, pamebaki wazi kama kituo cha polisi kisichofungwa au labda lile Mercedes Benz bovu la makene ndilo liligongesha?
 
Kila mtu anapewa tunu yake kutokana na mazingira yake, Muhingo nae alikuwa ana matarajio mengi sana ya kupata vyeo hasa baada ya kutimuliwa kazi Mwananchi kwa kuedit picha ya Salim Ahmed Salim, mwenzie akapewa kuwa mwandishi wa habari wa waziri mkuu, yeye akapigwa bench, akajaribu kuomba u-DC bila mafanikio, na sasa anajituma kweli kwa Shein ili apelekwe ikulu ya Zanzibar.....

Niliwauliza watu wa usalama kwa nini Muhingo hapewi post wakanijibu fanya nae kazi uone uzima wa kichwa chake kwanza. Na kweli tangu nimekuwa nae hapa New Habari amashatangaza kutaka kuacha kazi zaidi ya mara tatu then anarudi tena....... mara anajifanya yeye ni CEO anajifanya yuko karibu na Mengi, Rostam na hata Lowassa.
 
Naona wenye hii thread mnajijua sana tu... Mwaka huu, wenyewe mtawekana uchi!!!
 
Boniface Makene namfahamu vizuri sana, tulikuwa bweni moja pale Mkwawa High School, pia tukawa wote UDSM, the guy is opportunist, ana majivuno yaliyopita mpaka, anapenda makuu, anajiona kuwa juu ya kila mtu.

Pia ana sifa nzuri, mojawapo ni kujiamini na uwezo wake mkubwa wa kujieleza. Huyu hawezi kufanya kazi na mtu yeyote awe fisadi au mtakatifu labda awe bosi wa wote.

A piece of advice, Makene (najua tupo sote hapa JF) jaribu kupunguza u-opportunist, jifunze kuishi na watu; zaidi try to stand on a right side na utumie elimu na ujuzi wako vizuri. Sorry I look too personal, but they are many guys like you, have to get this message... yamkini watasikia na kubadilika.
 
Back
Top Bottom