Fred Katulanda
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 374
- 509
Wafanyakazi zaidi ya 200 waliokuwa wameajiriwa kwenye kampuni ya new habari(2006) limited inayomiliki magazeti ya Mtanzania na mengine wameiomba Serikali imshinikize mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz kuwalipa fedha zao ambazo ni mafao yao.
Msemaji wa wafanyakazi hao, Arodia Peter amesema wanaomba taarifa zao zimfikie Rais Samia baada ya mwajiri wao ya New Habari inayomilikiwa na Rostam Aziz chini ya afisa mtendaji mkuu, Hussein Bashe ambae sasa ni waziri wa kilimo kwa kushindwa kuwapelekea mafao yao kwenye mifuko ya hifadhi ya kijamii.
Msemaji amedai Rostam Aziz kupitia kwa mtendaji mkuu, Hussein Bashe waliwaondoa kazini Mei 31, 2019 bila kuwalipa stahiki za mafao kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na iliyokuwa PPF kwa mujibu wa sheria.
Pia wamedai mwajiri wao aliwaondoa kazini kwa lazima wafanyakazi wake bila kutangaza kwa umma pia sababu za kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.
Lakini pamoja na hatua ya kuwaondoa hawajawalipa mafao kama ambavyo walikuwa wamewaahidi.
=====
UPDATES: 05 Februari 2022
======
Baada ya Masaa 24 Toka Wanaodai Mafao kuongea na Wanahabari, Hatimaye Wafanyakazi Wamekiri kwamba Rostam Aziz kawalipa Mafao yao.
Wakati akosoma taarifa kwa vyombo vya Habari, Arodia Peter amesema kwamba juzi baada ya kuongea na vyombo vya habari, Rostam Aziz aliwaita kwa kikao cha dharura. Rostam alisema alikuwa hana habari kama anadaiwa, hivyo muda huo huo akafanya Malipo yote waliyokuwa wakidai ikiwemo Mafao kwenye mifuko ya Jamii.
Wafanyakazi wa New Habari ambayo inamiliki Magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba na The African, Walikuwa wanazungushwa kulipwa mafao yao kwa miaka Mitatu baada ya kuachishwa kazi.
Pia, soma: Rostam Aziz akubali yaishe, atoa hundi za malipo ya waliokuwa wafanyakazi wa New Habari (2006)