TEC ni taasisi ya kidini ambayo watu wake ni Watanzania; msimamo wao ni msimamo wa wananchi wengi

neno ni upanga

Senior Member
Jun 28, 2022
189
725
Habari za asubuhi wakuu,

Juzi kati, Maaskofu wa Kikatoliki Tanzania wametoa msimamo wao kuhusiana na bandari, lakini jambo la ajabu kuna watu wameibuka kuwashambulia kwa kuwapinga na cha ajabu wengine ni viongozi wa dini ya Kikristo!

Mimi ni Mkristo, tena Mpentekoste, mwalimu wa neno la Mungu na mwinjilisti ninayehubiri neno la Mungu kama lilivyo. Walichokifanya TEC ni kibiblia na yeyote anayepinga msimamo wao akapimwe akili kwa sababu zifuatazo:

1. TEC ni taasisi ya kidini ambayo watu wake au waumini wake ni Watanzania, hivyo msimamo wao ni ndio msimamo wa wananchi tulio wengi.

2. Lusekelo anasema TEC inapinga serikali, mwambie akasome historia ya akina Daniel kwenye Biblia, Eliya, Elisha, Samweli, walivyopingana na serikali waziwazi kwa mambo ya hovyo. Kuwa kiongozi wa dini maana yake ni kusimamia kweli, sio kujikomba kwa serikali. Pale serikali inapokosea, wanapaswa kuambiwa ukweli, pale wanapofanya sahihi wanapaswa kupongezwa pia. Nimuulize Lusekelo, mbona hao viongozi wa dini wanavyopongeza serikali, husemi kuwa wanaingilia serikali? Ni kwenye kupinga ndio useme wanaingilia serikali? Lusekelo anapaswa kujua kuwa serikali au mamalaka zote duniani, watu wake wana dini, hivyo huwezi kubeza maoni ya viongozi wa dini. Vinginevyo hao viongozi wa serikali wawe ni sio watu, ni mashetani.

3. TEC wamechambua waraka kwa kifungu kwa kifungu, hao wanaowapinga nao waje na waraka wao, tuuone na watupe majibu yao kuhusiana na maswali tunayohitaji majibu kuhusiana na mkataba wa DP World.

4. Watanzania wengi tulishaelewa ukweli ni upi, hivyo unapokuja kutetea suala la bandari, tunakuona wewe kama chawa tu, mchumikaji tumbo, mwizi, jambazi, nk.

5. Mnasema viongozi wa dini wasichanganye siasa na dini. Gwajima yupo chama gani? Anapokuwa jukwaani mbona kila uchwao anaongea siasa? Mbona mnapopongezwa hamsemi kuwa hiyo ni siasa? Tuache unafiki!
Msitulazimishe bhana mkataba wa bandari hatuutaki iwe usiku au iwe mchana! Hatuwataki tu! Hao DP World, wakatafute kwingine.
 
Wanaoupinga huo waraka ni walewale waliokuwa wanaupigia chapuo toka mwanzo, wakiongozwa na chawa na ma waziri bongolala kama akina Napesi nk.

Hakuna mwenye akili timamu ambaye amesikika anaupinga huu waraka.
 
20230821_133253.jpg
Huyu hapa mvamia ubwabwa
 
Back
Top Bottom