Ndugu yangu anataka kuomba mkopo elimu ya juu but mzazi mmoja ana ulemavu aanzie wapi ili apate fomu ya kujaza kuhusu mzazi mwenye ulemavu?

cute nee

Member
Jul 13, 2019
42
40
Habari zenu,

Nina binamu yangu kafaulu anataka kuomba mkopo bodi ya elimu ya juu lakini kuna mzazi wake mmoja ana ulemavu wa masikio(kiziwi) katika fomu ya mikopo anatakiwa kujaza taarifa za mzazi mwenye ulemavu ambapo ameshauriwa kwenda hospital ili kupata uthibitisho.

Tatizo lipo hapa kipindi cha nyuma 2019 mzazi wake alikuwa anafanya matibabu ya masikio katika hospitali binafsi na anathibitisho na vipimo wa taarifa za ulemavu wake wameenda hospital ya manispaa wanamwambia aanze mwanzo kabisa wa matibabu yani aonane na daktari wa masikio kwa uthibitishokitu ambacho kinakuwa ngumu sababu gharama zinaanza upya(kwa sasa hana bima) je ile karatasi ya mwanzo ya hospital private haiwezi thibitisha?

Je, akienda kwa daktari wa kawaida na karatasi ya uthibitisho ya hospital ya private je hawezi thibitisha?

Na je uthibitisho wa hospitali ya manispaa kwenye fomu ya mikopo inakubaliwa au mpaka wa wilaya na mkoa tu?
 
Waende Hospital ya serikali na hizo documents za prvt wawaelezee wanaweza saidiwa na jambo lisiwe na ugumu sana
 
Asante sana
Hapana ,mimi nilimfanyia mtu application mwaka jana utaratibu uko hivi;

Pale pale wakati unaapply kuna sehemu unaulizwa kama kuna Mzazi mmoja mlemavu ukiweka Yes fomu wanatoa wenyewe kisha unaipakua na kuitoa ikiwa hardcopy kisha unaipeleka kwa mganga mkuu wa wilaya ,mkoa au daktari wa ulemavu husika ili kuthibitisha na kupiga mihuri na kutoa maelezo kisha unaiscan na kuiupload kwenye mfumo wako wa online wa mkopo.
 
Hapo nimekuelewa asante
 
Back
Top Bottom