Ndoa Matatani

idorome

Member
Apr 19, 2012
28
7
Nimatumaini yangu hamjambo wote humu ndani na naheshimu sana busara zenu,mimi nimeoa na nina watoto 2, ndoa yangu imeingia doa na iko mashakani kuvunjika, kuna mwanaume nilikuta ujumbe wake kwenye simu ya mke wangu na nahisi wana mahusiano na inapelekea mke wangu kutaka tutengane, je kuna uwezekano nikienda TIGO kupata mwenendo wa mawasiliano kati ya watu hawa wawili ili niwe na uhakika na mbaya wangu, naombeni mawazo kwani nipo mbali na ofisi za hawa wandugu
 
anasema hanipendi tena na amenizidi kipato hatuwezi kuishi kwa yeye kuleta mapato makubwa home

naomba nitambae na maeneo niliyoya-bold
1- hanipendi tena...kwanini?..umebadilika nini?
2- amenizidi kipato...wewe ulikuwa wapi akakuzidi kipato?..kipato chake kinatokana na ajira au mapato binafsi?..nini chanzo chake cha mapato binafsi?..nini chanzo cha mapato yake rasmi na ni kiasi gani?
3-kwa yeye kuleta mapato makubwa home...kwanini yeye alete mapato makubwa home?...mapato yako yanaenda wapi?..hujui jukumu la kulea na kulinda familia kwa mila za kiafrika ni la baba?...kwanini unaishi na mkeo kwa kipato kilicho-nje ya uwezo wako?

4- je ni mkeo wa ndoa na muna watoto?..wangapi?..ndoa ina umri gani?

nipe majibu ya maswali haya ili nikupe ushauri sahihi..maana hapa najaribu kusoma maisha yenu ya ndoa na nini hasa ni chanzo cha matatizo.
 
yeye ameajiriwa na ana kipato cha kila mwezi mimi nimejiajiri na kipato sio kikubwa sana kama unavyojua bishara ndogondogo, naomba kujuzwa kama nikienda TIGO watanipa mwenendo wa mawasiliano yao? naomba nijuze hilo mkuu
naomba nitambae na maeneo niliyoya-bold
1- hanipendi tena...kwanini?..umebadilika nini?
2- amenizidi kipato...wewe ulikuwa wapi akakuzidi kipato?..kipato chake kinatokana na ajira au mapato binafsi?..nini chanzo chake cha mapato binafsi?..nini chanzo cha mapato yake rasmi na ni kiasi gani?
3-kwa yeye kuleta mapato makubwa home...kwanini yeye alete mapato makubwa home?...mapato yako yanaenda wapi?..hujui jukumu la kulea na kulinda familia kwa mila za kiafrika ni la baba?...kwanini unaishi na mkeo kwa kipato kilicho-nje ya uwezo wako?

4- je ni mkeo wa ndoa na muna watoto?..wangapi?..ndoa ina umri gani?

nipe majibu ya maswali haya ili nikupe ushauri sahihi..maana hapa najaribu kusoma maisha yenu ya ndoa na nini hasa ni chanzo cha matatizo.
 
Kaka, mfano umeenda wamekupa kweli hayo mawasiliano (kitu ambacho sidhani kama wanaweza); halafu nini?
Ingekuwa wewe ndio unataka muachane na unatafuta ushahidi hapo sawa, lakini ni yeye ndio anataka muachane.

Mimi nakushauri, tulia kaa naye mzungumze ukiwa umetulia; washirikishe wazee wamshauri kuhusu watoto n.k. kama ni mke kweli atakusikia na mtasameheana; lakini kama ni kicheche, mwachie aende.
 
tumeshakaa amekomaa kuachana, vipi kama nikienda na barua ya kutoka polisi watanipa?

yeye ameajiriwa na ana kipato cha kila mwezi mimi nimejiajiri na kipato sio kikubwa sana kama unavyojua bishara ndogondogo, naomba kujuzwa kama nikienda tigo watanipa mwenendo wa mawasiliano yao? Naomba nijuze hilo mkuu

mkuu hujanijibu maswali yangu yote..naona unahofia sana kipato au unadhani kipato ndio kinamuweka mkeo nyumbani?...ndoa ni zaidi ya kipato...

pili naona unakomaa kwenda tigo..ukifika unaanzaje kuuliza?..eti ohh naomba mawasiliano ya simu namba hii unaulizwa wewe polisi utasemaje?..unaulizwa upewe ya kazi gani...ohh ananit$%%ombea mke wangu...punguza jazba...

Nisaidie imani yako ya kidini nikupe pia mafunzo kuhusu fumanizi sio unakurupuka tuu dogo. Pia jibu maswali yangu ya awali upewe ushauri sahihi...umenielewa dogo??
 
tumeshakaa amekomaa kuachana, vipi kama nikienda na barua ya kutoka polisi watanipa?

mbona unaonekana unaogopa kuachana nae??..unanitia wasiwasi...yani ufumanie sms wewe kisha uogope kumuach???...au wewe mariooo umeolewa unahofia life itakaba mtaani???...

Acha uoga kama anataka kusepa na basha wake mpe go ahead....kamata shorty mwingine life goez on...kwani akifa na wewe utakufa au ndio utataka ukamuulize mungu kwanini amemjukua mkeo??
 
Mkuu ushaidi muimu kuwa nao ata kama mtaendelea kuishi pamoja itakusaidia for further reference.

note: Naona mkae chini mzungumze labda munaweza kupa solution nzuri
 
One thing i know for sure.
Mwanamke akisema inatosha tambua kuwa hakuna tiba hapo.
Kubali matokeo na anza maisha mapya.
OTIS
 
ni kweli mkuu ila sasa namna ya kuupata ndio matatani
Mkuu ushaidi muimu kuwa nao ata kama mtaendelea kuishi pamoja itakusaidia for further reference.

note: Naona mkae chini mzungumze labda munaweza kupa solution nzuri
 
chukua chako mapeja labda BOSS wake anamega kisela...............lakini pole
 
mkuu mi naona ukipata hayo mawasilianao utakata tamaa na waweza chukua hatua mamabazo sio sahihi.
mi nakushauri ongea na mkeo ili uone kama anaweza badili msimamo wake, akiendelea kushikilia msimamo wake mi nafikiri mwache aende zake akuache ujipange kwa maisha mapya.
Ila kama ww ni muumini omba mungu atakufungulia njia.
 
Sidhani kama watakupa kwasababu wewe sio mwenye simu, na wale wanawajibika kwa wateja wao tu. Halafu ukishajua itakusaidia nini, yeye keshaweka bayani kuwa hakutaki tena na ameshakupa sababu zake. Binafsi sioni sababu ya kung'ang'ania hiyo ndio ikiwa ameshakupa kinagaubaga.

Wewe bora utambae zako, fanya mikakati na jinsi ya kuwalea hao watoto.
 
ni kweli mkuu ila sasa namna ya kuupata ndio matatani

nenda kwenye kampuni ya mtandao anao tumi utapata data.

Mind u: Nivema ukumbuke taree ya hiyo msg, no. yake uyo mkeo, no. ya ya mmewe wa nje, zote uwende nazo uatawinne tu. pole mkuu.
 
nashukuru kwa ushauri wako MadameX na vipi kama ukitoa cha juu

Back
Top Bottom