Ndesamburo kusafirisha wananchi bure kwenda Loliondo

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,988
4,507
MAMIA ya wakazi wa mji wa Moshi wamejitokeza kwenye ofisi ya Mbunge wa jimbo hilo, Philemon Ndesamburo (CHADEMA) kujiorodhesha majina kwa ajili ya safari ya kuelekea kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, katika Kijiji cha Samunge, Loliondo anayetoa dawa ya kutibu magonjwa sugu.

Wananchi hao wamejitokeza baada ya mbunge huyo kuamua kutoa usafiri wa bure wa kuwapeleka na kuwarudisha wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa sugu ambayo tiba yake hutolewa na ‘Babu' baada ya kuona wananchi wengi wanahitaji kwenda ila wanakwamishwa na fedha za nauli ambazo zimefikia kiasi cha shilingi 150,000.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana huku nje kukiwa na misururu mirefu ya wananchi wanaojiorodhesha, Ndesamburo alisema kuwa watawapeleka wananchi hao kwa awamu ambapo kwa kuanzia leo (Jumanne) jumla ya watu 73 wataondoka majira ya saa kumi jioni kuelekea Loliondo na wakirudi wataondoka wengine.
 
anajua kula na kipofu
real people like Ndesa will always live in our heart even though his life is over, live long Ndesamburo. The so call tycoons need to copy from this Mzee he is a true MZALENDO. May God Almight grant you more days on planet earth, aika mmeku!
 
Back
Top Bottom