Mbunge Gambo fikisha kilio cha ujenzi wa barabara ya kwenda kwa nabii Geordavie

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Arusha

Mke wa Nabii Mkuu Mh GeorDavie, Mchungaji Anna Davie ameiomba Serikali kutengeneza barabara ya kuelekea nyumbani kwake iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha kwani Mtumishi wa Mungu Nabii Mkuu GeoDavie ambayo kwa muda mrefu imekuwa na changamoto ya kupitika hasa kipindi cha mvua.

Akizungumza katika ibada ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Nabii Mkuu Dokta GeorDavie Mchungaji Anna Davie amemuomba Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo kupeleka kilio hicho kwa Mh Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzanai Mh Rais Samia Suluhu Hassan kutambua changamoto hiyo ya barabara ya kwenda kwa Nabii Mkuu GeorDavie ambayo kwa muda mrefu ameiomba serikali kufanyia marekebisho lakini mpaka sasa hakuna kilicho fanyiwa kazi.

Awali Mke wa Nabii Mkuu alimuomba Mbunge wa Arusha Mjini Gambo kufikisha maombi hayo kwa Rais Samia au bungeni kwa lengo la kufanyiwa utekelezaji wa haraka zaidi kwani barabara hiyo hutumika na wananchi kujipatia vipato na wengi wao ni wakulima pamoja na wafugaji.

"Naomba sana Mh mbunge fikisha maombi yangu kwa Mh Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan amjengee baba barabara ya kufika kwake ambayo inatumika na wananchi ambao ni wakulima na wafugaji na wanategemea kusafirisha mifugo yao kupeleka minadani pamoja na kusafirisha mazao yao" Alisema Mchungaji Anna Davie .

Mara baada Maombi hayo Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo alisema amepokea na kufanyia kazi na mara baada ya muda mchache alimjibu mke wa Nabii kuwa atalifanyia kazi mara baada ya kuwasiliana na wataalamu.

Hata hivyo Mbunge wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo alimshukuru Nabii Mkuu Mh Dokta GeorDavie kwa kutumia utajiri wake kusaidia jamii ya chini pamoja na wafanya biashara wa soko la Samunge pamoja na kutoa mitaji kwa kina mama na vijana wa kitanzania ambao kwa asilimia kubwa amegusa na kuwabadilisha katika maisha yao.

Gambo amesema kuwa, toka wafanya biashara wa Samunge wapewe zaidi ya shilingi Millioni Mia moja kwa wafanya biashara wa Samunge wamekuwa na mafanikio makubwa katika biashara zao na uongozi wa somo kwa sasa wameanza ujenzi wa uzio wa soko pamoja na kuweka mageti ya kuingilia sokoni hapo lakini yote hayo ni kutokana na Nabii Mkuu Mh GeorDavie kuwasaidia wafanya biashara hao.
View attachment 2598750
20230423_165749.jpg
View attachment 2598749
 
Kama Sadaka hazi toshi basi mtumishi aombe nayo lami itokeze si wana sema ukiwa na imani chochote utakacho kina fanyika vipi mtumishi hana imani
 
Mheshimiwa Mbunge nasi wa barabara ya Kijenge Mwanama Engutoto utusaidie, ile lami inayoishia pale Mwanama ije hadi Engutoto..wapigakura wako tunateseka..

Pia hiyo lami inayoishia kwa Matajiri wa Kijenge PPF ijengwe hadi huku Moshono karibu na Club D..hii itasaidia kutufikisha kirahic hapo Kituo cha Afya, Moshono
 
Nabii mkuu wa mchongo inakuwaje anakubali kuishi kwenye mazingira mabovu ya miundo mbinu?
Kwanini asijitolee kujenga hiyo barabara yeye mwenyewe kwa kuwa anazo pesa za kugawa ovyo?
 
Nabii Mkuu wa mchongo ana mbwembwe kibao za kujionyesha kuwa ana pesa na mamlaka ya kuamuru chochote lakini kiuhalisia ni maskini wa kawaida mnoo anaishi kwa kuwakamua waumini wake na ujanja ujanja wa kuwahonga watu ili wampe promo.
 
Back
Top Bottom