Ndege iliyokuwa na ujumbe toka Ivory Coast yazuiwa kuondoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA)

Hao ni wageni wa Rais na kama umesoma vizuri mada yeye kauliza kutaka kujuwa tatizo ni nini. Hivi wewe mgeni wako akizuiliwa kusafiri hutotaka kujuwa sababu? kweli kuna watu na viatu.

Huo mkutano wa Arusha ulikuwa na viongozi wengi tu na wamekuja na ndege zao. Kwanini hii ndege ya vigogo wa Ivory Cost izuiliwe na sio hizo zingine?
 
huyo jamaa anapaswa kuvikwa medani ...yaani ujumbe wa rais ndo nini?yaani kama hawajafuata sheria washuke waendelee kupiga koka wasubiri mkuu wa uwanja atoe go ahead

Halafu hawa wanatumia jina la rais wengine ndo wezi wakubwa. Wanaweza kuwa wanavusha nyara za serikali
 
Anataka sheria na kanuni zifatwe? au anazuia wakati sheria na kanuni zote zimefatwa? Sidhani kama atakuwa na kiburi bila kulindwa na sheria na kanuni, kuna vitu haviko sawa.

Hata kama anafuata sheria,huyo nadhani ccm itamtoa kafara kupitia waziri wake mhusika.Mimi pia nipo kwenye viwanja vya ndege naona taratibu zinavyokiukwa na bado watu hao wanaruhusiwa kuondoka.Kama watumishi wote wangekuwa wana komaa kufuata sheria kila siku mngesikia habari hizo.Ila wafanykazi wengine wanakubali yaishe na amri hizi hutoka kwa watu wa ccm yaani serikali yake.Kule kupigiwa simu tu hata kama sheria zimekiukwa mwingine tayari angekuwa ameshakubali yaishe.Nchi hii haina utawala wa sheria wala kuheshimu.Nimeshuhudia mwenyewe viongozi wa ccm wakitoa amri ya mukuu wa uwanja kupandisha bendera ya ccm wakati wa maadhimisho ya sherehe za ccm.Hapo utasema nini.Meneja mwoga anakubali yaishe ili tu kulinda kibarua chake.Nina uhakika huyo siku zake zinahesabika na huu ndio utawala wa ccm,ni hovyo.Nina ushahidi wa hili.
 
Hata yule dogo mfupi naye anatumia vibaya sana jina la rais anatakiwa apewe shuluba ajue urais sio cheo cha familia wala kujuana juana
 
Hakuna cha AJABU hapo mkuu kwani misafara kama hii ya viongozi wa juu ndio inayotumika kusafirisha MEGENDO na hata MADAWA ya kulevya

Usimseme vibaya anafanya kazi yake
 
Nadhani huu uwanja unaendeshwa na kampuni ya nje, na sio Watanzania. Nina uhakika kwamba kuna taratibu hazijafuatwa ndio maana amegoma, na anastahili pongezi. Kumbuka miaka michache iliyopita Kenya Airways walilazimisha kuruka kutoka uwanja wa ndege nchini Cameroon wakati wa mvua kubwa, japo walikataliwa. Matokeo ndege ile ilianguka baada ya dakika tano za kuwa hewani, abiria wote wakafa.

yeah mkuu..KQ ilianguka Doulla Cameroon.msimamizi yupo fresh kwa kukataa kufanya kazi kwa shinikizo la mkubwa
 
Watumishi wa Umma wote wajifunze kutoka kwa huyo Meneja wa uwanja, epuka kufanya kazi kwa simu na vimemo, omba uandikiwe maelekezo na ushauri kulingana na utalaam wako ili mambo yakienda vibaya, TAKUKURU wasianzie kwako.
 
Dah hapo kuna changamoto kubwa sana,,,,,tunaweza kuhisi huenda hata ile ndege ya wanyama watu waliona ila wakapigiwa SIMU....
 
Huo mkutano wa Arusha ulikuwa na viongozi wengi tu na wamekuja na ndege zao. Kwanini hii ndege ya vigogo wa Ivory Cost izuiliwe na sio hizo zingine?

Soma post zangu za mwanzo, nimesema, huyo aliyeizuwia ni lazima ana sababu muhimu za kisheria na kanuni na si kiburi chake kama mleta mada alivyoandika. Tusibishane kwa kitu ambacho hatujapata habari kamili, ngoja tuendelee kusikia kwa waliopo huko. Au unasemaje?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Huo mkutano wa Arusha ulikuwa na viongozi wengi tu na wamekuja na ndege zao. Kwanini hii ndege ya vigogo wa Ivory Cost izuiliwe na sio hizo zingine?

nadhani ina nyara za serikali bcoz asubuhi NILIMUONA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI AKIPANDA NA KUSHUKA NJIA YA ARUSHA MOSHI
 
Hata kama anafuata sheria,huyo nadhani ccm itamtoa kafara kupitia waziri wake mhusika.Mimi pia nipo kwenye viwanja vya ndege naona taratibu zinavyokiukwa na bado watu hao wanaruhusiwa kuondoka.Kama watumishi wote wangekuwa wana komaa kufuata sheria kila siku mngesikia habari hizo.Ila wafanykazi wengine wanakubali yaishe na amri hizi hutoka kwa watu wa ccm yaani serikali yake.Kule kupigiwa simu tu hata kama sheria zimekiukwa mwingine tayari angekuwa ameshakubali yaishe.Nchi hii haina utawala wa sheria wala kuheshimu.Nimeshuhudia mwenyewe viongozi wa ccm wakitoa amri ya mukuu wa uwanja kupandisha bendera ya ccm wakati wa maadhimisho ya sherehe za ccm.Hapo utasema nini.Meneja mwoga anakubali yaishe ili tu kulinda kibarua chake.Nina uhakika huyo siku zake zinahesabika na huu ndio utawala wa ccm,ni hovyo.Nina ushahidi wa hili.

Ukiuke wewe mfanyakazi kutenda kazi zako huko airport uwasingizie CCM? kweli kuna watu na viatu.
 
Inavyoonekana kuna mambo hayako sawa. Na hata kama ni msafara wa nani haijalishi, swala ni taratibu zote zifuatwe, utumishi wa kuzingatia sheria na taratibu ni wa kupongezwa.Ila hapa, tutataka maelezo ya ziada, kwann walizuiwa?
Mamlaka husika lazima hapa muutafute ukweli na muueleze umma wa Watanzania, we dont wanna here 'confidential due to diplomatic worries'.
 
Nilikuwa nafikiri ni mtu mwenye busara.

Basi huyo mfanyakazi aliyoruhusu inabidi ashitakiwe, kama hafati sheria na anafata maagizo ya simu, huyo hafai hata tone, itakuwa ni mchagga tu huyo, ndio wanapenda shortcut.

U Al Haj wake unahusu nini? kweli kuna watu na viatu.
Mkuu Zomba mbona unaonekana kama unatoa povu kinywani, sasa uchagga na hii hoja vinakuja je humu?? Wewe ni mmoja wa wanaoshinikiza watendaji kufuata matakwa ya viongozi bila kujali uvunjaji sheria na kanuni za nchi nini??
Sasa itakapofahamika kuwa kuna sababu kama za kuhujumu nchi au uvunjifu wa sheria amabvyo havihusiani na uchaga utatuambia nini hapa? Kaa sawa fuatilia kwa makini itakapobidi uwe tayari kula matamshi yako mwenyewe.
 
Simu ya msaidizi wa katibu ambaye ni msaidizi wa rais. Kama kuna mambo hayako sawa, hata mimi nisingeruhu hiyo ndege iruke. Hizi simu na vimemo ndo vinavyotafuna rasilimali za nchi yetu.

nijuavyo mimi taarifa rasmi huwa inaambatana na maandishi na wala sio kwa njia ya simu...
 
Mkuu Zomba mbona unaonekana kama unatoa povu kinywani, sasa uchagga na hii hoja vinakuja je humu?? Wewe ni mmoja wa wanaoshinikiza watendaji kufuata matakwa ya viongozi bila kujali uvunjaji sheria na kanuni za nchi nini??
Sasa itakapofahamika kuwa kuna sababu kama za kuhujumu nchi au uvunjifu wa sheria amabvyo havihusiani na uchaga utatuambia nini hapa? Kaa sawa fuatilia kwa makini itakapobidi uwe tayari kula matamshi yako mwenyewe.

Wanapenda shortcut, na wao ndio waliojazana Kilimanjaro Airport, kila idara.
 
Huyo msimamizi yuko sahihi, na watu kama yeye ndiyo wanaofukuzwa kazi kwa kuwa wakweli,kunauzembe hapo,hatuwezi kufanya kazi kwa kuongea kwa simu kwani wasaidizi wa rais hawatambuliwi kwa sauti zao kwenye simu, na wewe mtoa maada hii unatia shaka kwanini unamuhukumu kwamba ana kiburi,na si mtu anayejali,,,,unatia shaka
 
Back
Top Bottom