Huo mkutano wa Arusha ulikuwa na viongozi wengi tu na wamekuja na ndege zao. Kwanini hii ndege ya vigogo wa Ivory Cost izuiliwe na sio hizo zingine?
Kwani ameshazuia ndege ngapi toka kumekucha leo? Na kwanini ni ndege hiyo tu aizuie? Tafakari Mjomba, Unaweza kukuta kuna Kiboko au Mamba hai wa Baba Riz ameshapakiwa ndani ya hiyo ndege. Hataki kufa Ki-Maige huyo.
Mkuu huenda jamaa anafanya kazi yake. Labda ndege imekiuka masharti na inabidi wenye ndege wafuate taratibu fulani ndio waondoke. Naona unamshutumu kuwa ana kiburi; si anafanya kazi yake? Hiyo ni Arusha mkuu isije ikawa ndege ina simba ama kori bastard kesho mkaja kumuuliza kama alivyoulizwa Maige.
Labda ina twiga ndani
Hiyo ni hukumu ya jumla siyo nzuri sana. Sidhani kama ni vyema kuwa na chuki na kundi la watu kwa jinsi hiyo. Hiyo husababisha dhambi ya ubaguzi kama alivyowahi kuiita Baba wa Taifa, huwa haiishi kinyume chake huendelea kukua kama kansa katika mawazo ya binadamu. Ni nyema sana kujitahidi kuji-control. Epuka sana generalization za namna hii katika jamii.Wanapenda shortcut, na wao ndio waliojazana Kilimanjaro Airport, kila idara.
Mbona umemuhukumu bila hata ya wewe kujua sakata zima.Inaonekana sorce yako ya habari ni kutoka upande mmoja. Hapo KIA kuna uchafu unafanyika kila kukicha ,kuna ndege za Cargo kubwa mno zinatua hapo na kuondoka nishazishudia mara mbili wakati nime-land hapo na zote mbili ni za falme za kiarabu,sasa sijui kuna biashara gani na hao waarabu ili hali twajua waarabu ni wazoefu wa biashara ya pembe za ndovu tokea enzi hizo.Mengi yatajulikana Baba riz akiachia ngazi.Mpaka naondoka eneo la tukio ndege hiyo ilikuwa bado haijaruhusiwa kuruka baada ya msimamizi wa uwanaja huo kutia ngumu,haikujulikana maramoja sababu ni nini ila baada ya kumhoji alisema hajui ni kampuni gani inayo husika na ndege hiyo hivyo hawezi kuiruhusu kuruka.hata baada ya msaidizi wa katibu wa raisa kupiga simu uwanjani hapo kutaka kujua sababu ya ndege hiyo kuzuiliwa kuruka bado msimamizi huyo wa uwanja aligoma katakata kuongeanae hata alipo ambiwa ni ndege iliyokuwa na wageni wa raisi msimamizi huyo hakuwa tayari kuongea na msaidizi huyo wa katibu.kwa mwonekano msimamizi huyo wa uwanja anaonekana kuwa na kiburi sana na mtu asiye jali ila inaonekana ni mwendelezo wa kukomoana.
Chanzo ni mimi mwenyewe toka ngurudoto na uwanja wa ndege wa kilimanjaro kia
nikipata habari zaidi nitawaletea.
Ukiuke wewe mfanyakazi kutenda kazi zako huko airport uwasingizie CCM? kweli kuna watu na viatu.
Wewe cha kandambili. Kwi kwi kwi teh teh teh
Labda ina twiga ndani
Hiyo ni hukumu ya jumla siyo nzuri sana. Sidhani kama ni vyema kuwa na chuki na kundi la watu kwa jinsi hiyo. Hiyo husababisha dhambi ya ubaguzi kama alivyowahi kuiita Baba wa Taifa, huwa haiishi kinyume chake huendelea kukua kama kansa katika mawazo ya binadamu. Ni nyema sana kujitahidi kuji-control. Epuka sana generalization za namna hii katika jamii.
Acheni utoto.. Hoja hapa ni kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za kazi zinavyotaka au ku-by pass/overlook sheria na taratibu hizo za kazi pindi vikitumwa vimemo toka Ikulu..? Yuko sahihi kucimamia maamuzi yake kama taratibu hazikufuatwa..? Kwangu mie ninaona yuko sawa kama amezuia kwa kuwa kuna taratibu hazikufuatwa..
Aliyetoka kwenye mada ni wewe in the first place!Angekuwa hana dhambi ya ubaguzi kusingekuwa na 87/13. Turudi kwenye mada.