Ndanda kossovo atimuliwa nchini

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895

*WAPIGWA PA, WAPO CHINI YA ULINZI ARUSHA KESHO KUSAFIRISHWA KWENDA CONGO.

MWANAMUZIKI mahiri wa miondoko ya dansi aliyepata kujizolea sika kem kem nchini wakati akiwa na bendi ya FM miaka ya nyuma kabla ya kujiengua na kuunda kundi lake lililojulikana kwa jina la Stono Musica, Ndanda Cosovo ‘Kichaa’ amekamatwa masaa machache jijini Arusha pamoja na wanamuziki wa bendi yake mpya.

Akizungumza kwa njia ya simu, Ndanda Cosovo, alisema kuwa amekamatwa yeye pamoja na wanamuziki wake wote na kuwekwa chini ya ulinzi ambapo kwa sasa wanasubiri kupelekwa Rumande hadi kesho watakaposafirishwa kurudi kwao Kongo.

Aidha Ndada alisema kuwa ameshangazwa na uongozi wa Uhamiaji kukagua vibali vyake vya kuishi nchini na kumwambia kuwa vibali hivyo ni ‘Feki’ hali ya kuwa alikata na kulipia vibali hivyo jijini Dar es Salaam.

“Mimi nashangaa sana kama Mkurugenzi wa Uhamiaji anaweza kupokea pesa na kisha akatoa vibari Feki, hii si sawa kwani mimi nilikuwa nikiishi Tanzania kwa uhalali na kufuata taratibu zote na ndiyo maana nikawa nikifanya kazi zangu bila kificho, leo nakamatwa nakuambiwa vibari vyangu ni feki kwa kweli nimesikitika sana,

Napenda kuwaageni marafiki zangu wote mbaki salama kwani tuliishi kwa amani na kusaidiana kama ndugu leo hii naambiwa nimevunja sheria mbona hawajaniambia hivyo tangu nilipokuwa nikiwalipa pesa za vibari??” alimaliza kwa kuhoji Cosovo. Mia
 
Hao ndio wanaofanya maisha yazidi kuwa magumu. Afadhali wamemuondoa kudadadadeki
 
Hao ndio wanaofanya maisha yazidi kuwa magumu. Afadhali wamemuondoa kudadadadeki

WaTZ wenzenu walioko nje wakifanyiwa hivo hizo nchi mnaita wabaguzi, kumbe na nyie wabaguzi ehe! Kama hakuwa na vibali sawa ila kama wanampa alafu wanamzunguka hapo si sawa.
 
WaTZ wenzenu walioko nje wakifanyiwa hivo hizo nchi mnaita wabaguzi, kumbe na nyie wabaguzi ehe! Kama hakuwa na vibali sawa ila kama wanampa alafu wanamzunguka hapo si sawa.

Rudi kwenu kwani lazima na wewe uishi Tanganyika? Njaa tu ndio inayokusumbua kwani kwenu hamna chakula mpaka mkimbilie tanganyika
 
waambie wakuruhusu uende na mkeo chitoto: miariko tutakupa na tutakulipa US dollar:
 
mnh mbona siku nyingi anafukuzwa mara anarudishwa....................BASHE sijui watampeleka wapy
 
Sio hao wacongo tu, kuna wasomali tele wanaishi bila vibali, wahindi na waarabu ndo wa kumwaga, agghhhhhhr hii nchi hii!
 
sasa wanaanza kulia ooh..nuhu..ooh! nuhu tufungulie safina..Mimi sina uwezo..hapa piga ua...funguo anayo Mungu baba...
MIA
 
wangeanza na wahindi wanaoinyonya nchi yetu hata kujenga nyumba hawataki wanaishia kukaa kwenye nhc wakongo wamewaonea ni ndugu zetu hao
yani hawa wahindi ni watu wa ajabu sana! Yani pesa yote wanapata inarudi kwao hata kujenya nyumba ya chumba kimoja hawataki!
 
kila binadamu ana roho mbaya

Jela jela kubaya. Dawa yao malipo yawe yanafanyika kwa Cheque ndio utakuwa mwisho wa rushwa Idara ya uhamiaji
 
kila binadamu ana roho mbaya

Jela jela kubaya. Dawa yao malipo yawe yanafanyika kwa Cheque ndio utakuwa mwisho wa rushwa Idara ya uhamiaji

kivipi, kwani hizo cheque nazo si ni hela tu, unaenda kuzibadili maisha yanaendelea kama kawa
 
Bora hata wahidi wanasaidi kuendeleza mzinguko wa hela.wa congo ni wanaongeza mzunguko wa maradhi
 
Back
Top Bottom