Ndama Mtoto wa Ng'ombe!

MmasaiHalisi

Senior Member
Jan 15, 2009
192
23
Wafanyabiashara wa magari Dar mbaroni kwa kunyatia albino

* Yumo Kizaizai na Ndama 'mtoto wa ng'ombe'

Na Mwandishi Wetu


WAFANYABIASHARA maarufu wa magari jijini Dar es Salaam, akiwemo Ali Juma (40) maarufu kama 'Kizaizai' wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutaka kumteka mtoto albino.

Mbali na Kizaizai, ambaye huimbwa katika nyimbo kadhaa za muziki wa dansi na bendi mbalimbali nchini, mwingine anayeshikiliwa kuhusiana na tuhuma hizo ni Ndama Shaaban (36) maarufu kama 'Ndama Mtoto wa Ng'ombe'.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Evarist Mangala, aliliambia Uhuru jana na kuwataja watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kuwa ni Kulwa Herman (3, Suleiman Mohammed (34).

Wengine ambao walikamatwa siku hiyo ya tukio ni Thobias Mgayi (21), anayejishughulisha na upambaji katika kumbi za starehe, Juma Ndaigwa (26) mfanyabiashara mkazi wa Magomeni Mapipa na Edgar Elias (21) ambaye anadaiwa ndiye aliyekuwa mwenyeji wa watuhumiwa Mgayi na Anthony waliokamatwa siku hiyo ya tukio.

Kulingana na Mangala, tukio hilo lilitokea Novemba 27, mwaka huu, saa 11.00 jioni, eneo la Kipawa, Manispaa ya Ilala, nyumbani kwao, Irene Stanslaus (10) ambaye ni albino. Kizaizai na Ndama walitajwa na watuhumiwa waliokamatwa awali.

Akielezea suala hilo, Mangala alisema siku ya tukio, vijana hao walionekana wakizungukazunguka katika eneo hilo na ndipo , walipotiliwa shaka na wakazi wa eneo hilo kwamba walikuwa wakitaka kumkamata mtoto huyo Irene.

Mapema, akitoa taarifa za tukio hilo la kukamatwa Mgayi, Elias na Anthony, alisema watuhumiwa hao walimwita mtoto huyo kwa nia ya kumtorosha, ili kufanikisha masuala ya kishirikina.

Akimnukuu mama wa mtoto huyo, Evodia Stanslaus (34), Kamanda Mangala alisema baada ya Irene kushtuka, alikimbilia ndani na kumueleza mama yake kuhusiana na watu hao.

Mangala alisema baada ya Evodia kupata taarifa hizo, alitoka nje na kuhoji kulikoni, ndipo watuhumiwa walipodai wanataka kununua simu za mkononi, lakini alipotoa simu yake ili awauzie walishindwa kuinunua.

Alisema kitendo hicho kilimshtua na hivyo kuamua kupiga 'yowe', lililovuta watu wengi kabla ya polisi kujitokeza na kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.

Kwa mujibu Mangala, watuhumiwa walipohojiwa walikiri kuhusika na matukio manne ya mauaji ya maalbino nchini.

Akifafanua, matukio hayo ni la mkoani Morogoro mwaka 2005 na Coco Beach, Oysterbay Dar es Salaam, mwaka 2006. Watuhumiwa hao pia walikiri kuhusika na tukio la mauaji ya albino lililotokea eneo la Tandale kwa Mtogole, mwaka 2006. Pia, walikiri kuhusika na tukio ambalo halikufanikiwa, lililotokea eneo la Kigamboni, mwaka 2006.

Watuhumiwa pia waliwataja watu wanaodaiwa kushirikiana nao kuwa ni Ndama, Kizaizai, Mohammed na Herman ambao nao walitiwa mbaroni baadaye ambapo wanaendelea kuhojiwa na polisi.

Hivi kesi hii iliishia wapi?
 
Jamaa waliletewa Ndama na Kizaizai wakashindwa kuwatambua. Hivyo Ndama na Kizaizai waliachiwa,wale jamaa bado wanasota.
 
Asante Mponjoli kwa update, si ndio maana Burn akasema hizi zilikuwa Beef za watoto wa Mujini! By the way Yo Yo kibongo bongo! wote Ndama mtoto wa ng'ombe na Kizaizai ni celebrities si huwa watatajwa sana kwenye bendi za muziki hasa zile za jamaa zetu wa DRC na siku hizi hata T-respect na Twanga, na tusubiri kuwasikia Extra Bongo. Hivi Fikiri Madinda yuko wapi?
 
Asante Mponjoli kwa update, si ndio maana Burn akasema hizi zilikuwa Beef za watoto wa Mujini! By the way Yo Yo kibongo bongo! wote Ndama mtoto wa ng'ombe na Kizaizai ni celebrities si huwa watatajwa sana kwenye bendi za muziki hasa zile za jamaa zetu wa DRC na siku hizi hata T-respect na Twanga, na tusubiri kuwasikia Extra Bongo. Hivi Fikiri Madinda yuko wapi?

Huyo Fikiri Madinda anafanya kazi pale Wizara ya Kilimo (maeneo ya TAZARA).
 
Sio Shemeji ila ninataarifa kutakuwa na shughuli ya kuvunja na Mundu... na nimeshaandaa koo kwa ajili ya vitu bariiiidi... pale Karimjee...
 
Ilikuwa ni beef na kamanda mmoja wa polisi alitokea Arusha ,........aliuziwa Prado lika haribika engine baada ya mwezi akadai arudishiwe pesa yake...aahhh wapi bwana,...hapo ndipo beef lilipozuka...ila walionewa tu...huku na huku ziliwatoka kama 10m
 
Ilikuwa ni beef na kamanda mmoja wa polisi alitokea Arusha ,........aliuziwa Prado lika haribika engine baada ya mwezi akadai arudishiwe pesa yake...aahhh wapi bwana,...hapo ndipo beef lilipozuka...ila walionewa tu...huku na huku ziliwatoka kama 10m

Sasa watu wangapi hufungwa kwa kesi za ksingiziwa?. Mijizi na mifisadi iko nje inakula raha.
 
Back
Top Bottom