NECTA inatunga na kusahihisha mitihani na hatimaye kutangaza matokeo ya mitihani. Haihusiki na ufundishaji - sasa kitakuwa kihoja Mkurugenzi wa NECTA kuwajibishwa kutokana na maafa haya!!!! Waziri anaweza kuwajibishwa au kuwajibika (kisiasa) mwenyewe kwa vile yeye ndio kichwa cha sekta yote ya elimu nchini. Lakini hata hivyo lo lote linawezekana bongoland, itself another wonder of the world.
Uko sahihi kimantiki, lakini kisiasa (kichama) sio.Nikiiamini taarifa ya mleta uzi kuwa Dr. Ndalichako aliombwa achakachue akakataa, kisha nikirejea alivyonukuliwa kwenye gazeti la Mwanachi la 19 Feb 13, baadhi ya wanafunzi waliandika namba zao tu kwenye karatasi za majibu akatolea mfano wa mtihani wa biolojia, na kuwa wao NECTA walifanya jitihada za kupiga simu kwa Walimu wa wanafunzi hao na kuambiwa kuwa wanafunzi walifanya hivyo kwa KUWA HAWANA WALIMU WA MASOMO HAYO! Kama nikweli, natarajia kabisa hiki kipengele kimtie matatizoni.NECTA inatunga na kusahihisha mitihani na hatimaye kutangaza matokeo ya mitihani. Haihusiki na ufundishaji - sasa kitakuwa kihoja Mkurugenzi wa NECTA kuwajibishwa kutokana na maafa haya!!!! Waziri anaweza kuwajibishwa au kuwajibika (kisiasa) mwenyewe kwa vile yeye ndio kichwa cha sekta yote ya elimu nchini. Lakini hata hivyo lo lote linawezekana bongoland, itself another wonder of the world.
kwa aliyokuwa anaongea waziri wa elimu katika kipindi cha tuongee asubuhi siku ya jnne,anaetakiwa kujiuzulu ni waziri mwenyewe maana anaonyesha kwamba kufeli kwa watoto hilo sio jambo la kutishaHabari zilizoenea miongoni mwa wafanyakazi wa NECTA na wizara ya Elimu tangu jana jumatano zinasema wakati wowote kuanzia sasa Katibu Mtendaji wa baraza la Mitihani - Dr. JOYCE NDALICHAKO atang'olewa katika nafasi yake!....
kumjenga
Anaondolewa ili kisiasa DR. Shukuru Kawambwa, kufuatia matokeo mabaya ya kidato cha nne!... Haya ni matokeo mabaya ya kihistoria katika nchi ya Tanzania... hayajawahi kutokea na pengine hayatatokea tena siku za usoni.Hizi ni TAKWIMU ZA UKWELI!.....
- DIV ONE 1,641
- TWO 6,453
- THREE 15,421
- FOUR 103,327
- ZERO 240,903! SAFI SANA WALIMU!
Hofu kubwa imekuwa kelele nyingi za chini chini na wazi wazi Zinazomtaka Dr. Kawambwa ajiuzulu. Matukio ya uchomaji moto kanisa na mauaji ya padre Mushi yamepunguza kidogo presha na shutuma za matokeo.
Hofu pia inachangiwa na moto uliowashwa na Mbatia na kuungwa mkono na wapinzani wote kuhusu kuporomoka kwa ubora wa elimu na ukosefu wa mitaala. Kwa mujibu wa wafanyakazi hao hoja hii pia ilichangia ucheleweshaji wa kutangaza matokeo!...
Dr. Ndalichako pia analaumiwa kuwa aliwajibu vibaya wanasiasa walipomtaka ACHAKACHUE matokeo ILI KUFICHA aibu hii!.. Yeye aliwajibu kavukavu kuwa YEYE HAJUI NA TENA HAWEZI KUCHAKACHUA!.. Bifu hili liliendelea mpaka utangazaji wenyewe ukawa mikononi mwa waziri Kawambwa na msaidizi wake MULUGO!. KATIBU MTENDAJI - Ndalichako hakung'ara kama ilivyozoeleka wakati wa kutangaza matokeo.
MATOKEO HAYA Yamekuwa yakishambuliwa kupitia njia mbalimbali zikiwemo simu za mkononi na hii ni moja ya sms hizo:
ELIMU JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU!!!! WALIMU SAFIIIIIIIIIII!!! WATANZANIA HASA WENYE TAALUMA YA UALIMU NA WENYE MAPENZI MEMA NA NCHII!
TUNATUMIA FULSA HII KUWAPONGEZA WALIMU WA SEKONDARI KWA MATOKEO MAZUR YA KIDATO CHA NNE AMBAYO HAYAJAWAH KUTOKEA TOKA BARAZA LA MITIHAN LIUNDWE NCHINI!
WALIMU WAMEONESHA FADHILA KWA SERIKAL YA CCM KWA MAMBO MEMA ILIYOWATENDEA! HII MTAALA WA WAZIR KAWAMBWA NA MULUGO UMETOA MATOKEO HAYA:
DIV ONE 1,641 TWO 6,453 THREE 15,421 FOUR 103,327 ZERO 240,903! SAFI SANA WALIMU!
MTAALA BORA ELIMU BORA YA CCM! UNALIPA UNAVYOLIPWA! HEKOHEKO WALIMU!
kitu cha kwanza ili tufanikiwe na chochote katika nchi hii ni kuitoa ccm madarakani kwanzaPamoja na reforms zoote tunazotaka kufanya, malezi na.makuzi yasisahaulike. Tunao ndugu, hata kama sio watoto wetu ambao wamefanya huu mtihani. Kuna aliepata division 3 na hakulala kwa kilio na masononeko. Kuna aliepata 4 na anakenua meno ukimuuliza matokeo. Lakini tofauti unaiona kwenye malezi ya wazazi wao.
Sichoki kuwaza wazazi wangu binafsi, ningewarudia na division 4 ama 0 (sheria ilikuwa hata 2 haikubaliki!), ingekuwaje. Watoto wakifeli na hata wasione soni juu ya hilo, kuna maswali zaidi ya kujiuliza!
Hivi hii badilishabadilisha silabasi kila kukichwa imefanywa na Ndalichako au Kawambwa??? Mbona hawaangalii walipojikwaa wanaangalia walipodondokea? Tutafika kweli jamani kwa mwendo huu?