Nchimbi: Viongozi wa CHADEMA watahojiwa juu ya kutishiwa kwao kuuwawa.

Fikiria hili:
Hivi kama Dr Ulimboka angeshtuka dakika kadhaa kabla ya wale watekaji na watesaji hawajamkamata na akasepa, kisha akasema kuwa maisha yake yapo hatarini na kuna watu wanataka kumdhuru au kumuua, hivi mnategemea Serikali ingesemaje? Si serikali wangekanusha tu kama hili la Slaa, Mnyika na Lema na kusema kuwa ni uzushi na kuwa Dr Ulimboka anajitafutia umaarufu?


Halafu, nani maarufu kati ya Dr Slaa, Lema na Mnyika kwa upande mmoja na Nchimbi kwa upande mwingine?
Inanikumbusha yale ya Zitto na Mkullo kuhusu umaarufu...


Mwisho wa watekaji na watesaji unakaribia...

Kidnapping and Torture ni makosa ambayo yatasababisha watuhumiwa wetu wakamatwe na kupelekwa Mahakama ya Kimataifa (ICC) ya The Hague. Kama wanadai hawahusiki na hawana hatia wakajitee huko kama akina Uhuru Kenyatta na Rutto.
 
Akiongea leo na TBC1 waziri wa mambo ya ndani Dr. Nchimbi amesema;
Shutuma walizo zitoa viongozi wa chadema kuhusu kutishiwa kuuwawa ni nzito sana. Amesema japo chadema hawajawapa tarifa serikalini, lakini yeye kwa niaba ya serikali hilo swala litafanyiwa kazi kwani ni wajibu wa serikali kulinda wananchi wake. Na tayari ameshaagiza wote walio toa shutuma hizo wahojiwe.

Usikose kuangalia kipindi cha mahojiano kati ya dr.Nchimbi na Tbc1 ifikapo saa tano kamili usiku huu.
Ni hayo tu.

Kuwahoji ni kuwalinda, nadhani angesema mkakati wa kuwalinda si kuwahoji ili iweje si vitisho bado hivyo???
Dr Mwakyembe si aliwekewa sumu akiwa ofisini tena waziri sembuse mtu baki, je uchunguzi uliishia wapi mbona kimya????
 
Fikiria hili:
Hivi kama Dr Ulimboka angeshtuka dakika kadhaa kabla ya wale watekaji na watesaji hawajamkamata na akasepa, kisha akasema kuwa maisha yake yapo hatarini na kuna watu wanataka kumdhuru au kumuua, hivi mnategemea Serikali ingesemaje? Si serikali wangekanusha tu kama hili la Slaa, Mnyika na Lema na kusema kuwa ni uzushi na kuwa Dr Ulimboka anajitafutia umaarufu?


Halafu, nani maarufu kati ya Dr Slaa, Lema na Mnyika kwa upande mmoja na Nchimbi kwa upande mwingine?
Inanikumbusha yale ya Zitto na Mkullo kuhusu umaarufu...


Mwisho wa watekaji na watesaji unakaribia...

Kidnapping and Torture ni makosa ambayo yatasababisha watuhumiwa wetu wakamatwe na kupelekwa Mahakama ya Kimataifa (ICC) ya The Hague. Kama wanadai hawahusiki na hawana hatia wakajitee huko kama akina Uhuru Kenyatta na Rutto.
Nimekupata Mkuu kweli kabisa the Hague ndilo jibu la wabishi, hayo mambo hayataisha hivihivi hata mauwaji ya ARUSHA BADO NIKITENDA WILI YANATAKA MAJIBU!!!!

 
hawa watataka kuwahoji ili wajue ni kwa kiasi gani chadema wanajua. ikiwezekana wabadili namna au kujipanga upya
 
Kwa hili la nchimbi na serikali nasema hivi, " Ni rahisi jua kuchomoza upande wa magharibi na kuzama upande wa mashariki kuliko Serikali ya magamba kulitendea kazi suala hili kwa ukweli na uwazi". Hiyo ni danganya toto ya serikali. Watakuja na matokeo yanayosema: "Tumebaini kwamba ni uzushi tu na hakuna ukweli wowote". Hili ndilo litakalokuwa jibu la uchunguzi wao. Hivi inawezekana hata siku moja shetani akafanya jitihada za kutafuta tiba ya dhambi ili kuhakikisha inatokomezwa ulimwenguni? Kama kweli shetani anaweza kufanya hivyo basi hata CCM wanaweza kushughulikia matatizo na shida za wapinzani kwa moyo.
Mkuu muulize Mhe Tundu Lisu anajua alifuatilia mauwaji ya watu kule kwenye machimbo watu walifuliwa wazima wazima na magreda sasa hivi na mifupa ogopa serikali ya maghamba!!! Mhe Mrema pia alifuatilia hatimaye kimyaaa!!!!

 
kwa kweli sekikali ya magamba imeshemsha na hizi siasa zao chafu ndio zitawamaliza kabisa
 
Mkuu hii inanikumbusha teja mmoja alikuwa na tabia ya kupitia viatu nje ya mlango wangu, sasa kuna siku ile natoka nje nakutana nae uso kwa uso ananyemelea viatu na kwa kuwa hakuna njia ya kupita akajifanya amepotea nyumba na kumuulizia mtu ambaye wala simfahamu. Nilipombana sana akakiri kuwa ni yeye ambaye huwa anachukua viatu mlangoni ila ni kwa ajili ya njaa na kuniahidi kuwa atahakikisha hakuna kibaka mwingine anachukua viatu pale. Tokea siku hiyo tukawa marafiki nikimkuta njia nampatia buku au jero na hakuna tena wizi uliofanyika.

Kawaida Mhalifu ukiishamjua huishia kujibalaguza kwani hujua kuwa chochote kikifanyika utamfuata yeye. Huu mpango haramu umebumbuluka na mahojiano hayo yatalenga si kuwahakikishia ulinzi bali kummbaini aliwapatia habari hizi za Operation haramu. Kinachonisikitisha ni wataalam wa usalama kukubali kutumiwa katika mbinu ambazo ni unprofessional na wanasiasa waroho wa madaraka.

Serikali hii imekosa legitimacy na haiaminiki tena na wananchi. Leo hii watu wanaiamini CDM zaidi ya serikali ambayo imekuwa ikitunga uwongo wa kitoto kufunika mambo. Watu hawajali credibility ya taasisi bali wapo kimasilahi zaidi.
Mkuu hakuna cha mbinu kubumburuka ogopa hao watu wakizamilia watafanya kweli, mifano ni mingi tuu chunguza ndugu yangu serikali ya kuzima watu hii!!!!

 
Nchi yetu ingekuwa mbali sana kama ingekuwa na watu wanofikiri haraka na kushauri kikamilifu kama ulivyofanya. Hakika umekumbusha jambo la msingi na pia kabla ya Dr. Slaa kuhojiwa ni vyema wakampa majibu ya vile vinasa sauti vilivyokutwa chumbani kwake akiwa bado mbunge hotelini dodoma.
 
Nchimbi utabakia kuwa mwanasiasa makini katika historia ya nchi yetu ikiwa utakuwa makini na suala la Dr. Ulimboka kabla ya kudandia hili la viongozi wa chadema.
 
Amesema japo chadema hawajawapa tarifa serikalini, lakini yeye kwa niaba ya serikali hilo swala litafanyiwa kazi kwani ni wajibu wa serikali kulinda wananchi wake. Na tayari ameshaagiza wote walio toa shutuma hizo wahojiwe.
Mbona hawajatoa taarifa za kuhusu "vinasa sauti" walivyotega kwenye kitanda cha Dr Slaa kule Dodoma?
 
Hii serikali ya ajabu sana, victim(Dr. Uli) kataja hadi mtuhumiwa aliyeshiriki kumteka, ambaye alimtambuwa alipokuwa hospitali, huo ni ushahidi mkubwa sana usioweza kupuuziwa na serikali timamu, lakini hakamatwi, badala yake anawekwa kwenye kamati ya uchunguzi, chadema kuweni makini...
 
Mkuu hakuna cha mbinu kubumburuka ogopa hao watu wakizamilia watafanya kweli, mifano ni mingi tuu chunguza ndugu yangu serikali ya kuzima watu hii!!!!


Uwezo wa kufanya tunajua wanao kwani wanamiliki maghala ya silaha na kila kitu. Lakini uwezo wa kufanya kwa siri hawana. Wanaweza kuwa na silaha za kujilinda na mashambulizi ya watakaokuwa wamapata hasira lakini hawatakuwa na siraha za kuifanya mioyo ya watu hao iachana na mawazo ya kutaka haki dhidi ya wahalifu wote itendeke whether kwenye mahakama au kwa njia yoyote itakayokuwepo.

Tumeshuhudia watu wengi wakitolewa uhai, kama Imran Kombe, Kolimba, Professor Juan Mwaikusa, Mwenyekiti wa CDM USA River na wengine wengi na hakuna la maana lililofanyika kuwafikisha wahalifu kwenye mikono wa sheria. Matendo yote haya yameondoa trust ya wananchi kwenye vyombo hivi na hili ni jambo la kuhofia kwani wananchi wanapokosa imani na authorities alternative huwa ni kujichukulia sheria mkononi.

Huwezi kuwa na legitimacy ya kuongoza kama unaweka vikao vya kuua raia wema kwa kuwa tu wanatishia ustawi wako au wa chama chako cha siasa kuwa madarakani. Vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria na lango ni moja kuomba ridhaa ya kuongoza nchi. Sasa kama chama kilichopo madarakani kinaona chama kinatishia uhai wao madarakani ni sawa na uhaini unaostahili execution summary ya ki-blackmail basi chama hicho kinakuwa hakina tofauti na kikundi haramu cha kimafia chenye lengo la kulinda masilahi yake.
 
Dr. Ulimboka alivyo toa taarifa ya walio taka kumuua, alisha kamatwa nani?? Tanzania tutaingia kwenye sura nyingine.Make hatuna imani na wanao jiita Serikali. Ni wasanii wasio na akili, wanakurupuka kutoa issue bila kutumia akili. Mungu wangu hivi hii nchi itaishia wapi?? Hakuna hata kiongozi wa serikali anaye weza kutoa tamko watu wakapiga makofi.!
Mungu tunusuru na hali hii.
 
Kwani Samuel 6 alihojiwa alivyo dai wanataka kumuua? CDM msikubali, sana sana hao ndo wana deal za kuwalimboka
 
Nchi yetu ingekuwa mbali sana kama ingekuwa na watu wanofikiri haraka na kushauri kikamilifu kama ulivyofanya. Hakika umekumbusha jambo la msingi na pia kabla ya Dr. Slaa kuhojiwa ni vyema wakampa majibu ya vile vinasa sauti vilivyokutwa chumbani kwake akiwa bado mbunge hotelini dodoma.

Ni kweli vile alivyowekewa na mkewe mama Rose Kamili ili amfumanie mfumbusa
 
Hii serikali ya ajabu sana, victim(Dr. Uli) kataja hadi mtuhumiwa aliyeshiriki kumteka, ambaye alimtambuwa alipokuwa hospitali, huo ni ushahidi mkubwa sana usioweza kupuuziwa na serikali timamu, lakini hakamatwi, badala yake anawekwa kwenye kamati ya uchunguzi, chadema kuweni makini...

Ni ngumu maelezo ya ulimboka kuchukuliwa kama sahihi kwa kuwa hata dr weaske alisema alipata mtikisiko wa ubongo....na pia ukisoma Mwananchi ya jnne iliopita walisema ameanza kutambua watu huko South Afrika hii inaonyesha alikuwa anaweweseka na sio kutambua watu kama mnavyodhania.sasa huo ni ushahidi butu hata kama angemtaja mtu
 
Leo nimesoma Nchimbi anapiga kelele kwamba ameshangazwa na msimamo wa Slaa, Lema na Mwanyika kukataa kupeleka suala lao Polisi kwa madai ya kuhofia suala hilo halitafanyiwa kazi. Nadhani Nchimbi kwanza anapaswa kutuambia Polisi walifanya nini pale walipopelekewa ushahidi kama huo na Dr. Mwakyembe kabla hajakimbilia kuwalaumu kina Slaa.

Na vipi tuhuma za Mengi kuhusu mtoto wake kubambikiwa madawa na Polisi - mtuambie kwanza Polisi walizifanyiaje kazi.

La sivyo tutawaambia serikali ya CCM ndiyo inayopandikiza chuki kwa wananchi kwa jinsi inavyolifanya jeshi la Polisi liwe na double standards. Ni kweli Watanzania wengi wanachukizwa na jinsi ambavyo jeshi la Polisi linashughulika na mambo yanayowahusu wanasiasa kwa namna ambayo inaonyesha wanafanya kazi kwa influence ya chama tawala cha CCM, au kwa kujipendekeza kwa CCM. Katiba ya Tanzania anayayoitaja Nchimbi haisemi jeshi la Polisi litatoa upendeleo kwa kikundi fulani cha kisiasa au chama tawala. Kama Nchimbi anajali katiba ya Tanzania basi ifikie wakati awaambie Polisi waache kufanya kazi kwa kujipendekeza kwa CCM - kama si kweli kwamba wanakuwa influenced na viongozi wa CCM katika utendaji wao.

Labda uwe na akili ya mwendawazimu ndio hutaona upendeleo wa wazi wa jeshi la Polisi jinsi kwa jinsi wanavyoshughulika na masuala yanayohusu CCM.
 
Hawa watu yahani wanatapatapa tu, wakisikia tuhuma ziko kwa wapinzani haraharaka sana wanatuma polisi wenyewe wala. ngoja siku nao watakuwa wapinzani
 
Back
Top Bottom