Nchimbi: Viongozi wa CHADEMA watahojiwa juu ya kutishiwa kwao kuuwawa.

Mtu kama huyu, kiongozi mkubwa anaongelea suala serious hivyo kiutani utani, yaani anafikia hata hatua ya kucheka wakati anaongelea ishu kama hii, ni nani asiyejua polisi ni watu wao wa karibu sana sana, maovu mangapi polisi wa Bongo wanayatenda kwa watu wasio na hatia kweli, wamezoea kupeleka umbea umbea na taarifa kwa hao hao wahalifu wanaowanyanyasa wasio na hatia, wananchi watadeal nao vizuri this time
 
Nchimbi hana moral authority ya kuwahoji viongozi wa Chadema, achilia mbali kufanya utafiti juu ya kutekwa na kupigwa kwa Dr. Ulimboka. Taaluma yake ya ujasusi haitumii vizuri na ni mtu mwenye kupenda kulipiza kisasi.
 
Kesha maliza uchunguzi sijui anamwagiza nani Kasema huyu mzee ( Nadhani Dr Slaa) kila siku anasema nitishiwa kukuuawa hata wananchi watampuza watasema ni kiongozi wa aina gani
Hawa Chadema wanataka kutisha wananchi wanachonganisha wananchi na jeshi la polisi ( Kamaliza uchunguzi hapo)
Hawa viongozi wa Chadema wafuate utaratibu wa sheria waende kwenye vituo vya polisi wakaripoti huko
Sikujua Nchimbi anadharau kiasi hiki anaadress hawa viongozi wa Chadema kama wahaini hawana uzalendo eti Marekani huwa wanaelewana democratis an republican kuna mambo wana simamia kama nchi
najiuliza jee CCM ya nchimbi inasimamia hayo au yenyewe inajiona ina hati miliki ya kutawala milele
Anasema Chadema wanawatia hofu wananchi kuhusu jeshi la polisi kwa wananchi hawajui kuwa jeshi la polisi na usalama wa taifa ni matawi ya CCM
 
Usoni nakuchekea,Moyoni nimeshakupangia watu kukupeleka Mwabe,km likibumburuka nitaunda tume yangu ya uchunguzi, kisha nitasafiri kwenda kuonana na kupiga picha na 50 cent nikirudi nitawaagiza mahakama watoe hukumu yao halafu vyombo vya habari haswa TBC itawatangazia.halafu mtafunga midomo yenu
 
Mtu kama huyu, kiongozi mkubwa anaongelea suala serious hivyo kiutani utani, yaani anafikia hata hatua ya kucheka wakati anaongelea ishu kama hii, ni nani asiyejua polisi ni watu wao wa karibu sana sana, maovu mangapi polisi wa Bongo wanayatenda kwa watu wasio na hatia kweli, wamezoea kupeleka umbea umbea na taarifa kwa hao hao wahalifu wanaowanyanyasa wasio na hatia, wananchi watadeal nao vizuri this time
Ulitaka aongee huku analia na wakatia ana address majungu ya watu wazima.....hahahaha na unaposema kuwa polisi wanatenda mabaya je na mazuri ya polisi hakuna?
 
Nimesikiliza na kuona Taarifa ya waziri wa mambo ya ndani ya Nchi (Ndg.Emmanuel Nchimbi) jii ya Tuhuma za Serikali kuwa na mbinu za kuwaangamiza viongozi wa CHADEMA. Kabla hata hajafanya Uchunguzi anakazana kurudia maneno mara mbili tatu kudai kuwa Viongozi wa CHADEMA ni wazushi na Wanatafuta Umaarufu!... So sad!.. Hivi kama hajafanya uchunguzi,hajawahoji walioongea anapata wapi ujasiri wa kudai kuwa ati WANATAFUTA UMAARUFU?.. Hii ni aibu,ujinga na udhaifu wa hali ya juu!..

Yap kasema wanatafuta umaarufu kwa kuwa hawataki kutoa ripoti polisi wanakimbilia vyombo vya habari ili kuchafua hali ya hewa ya nchi.
 
Ulitaka aongee huku analia na wakatia ana address majungu ya watu wazima.....hahahaha na unaposema kuwa polisi wanatenda mabaya je na mazuri ya polisi hakuna?
Inaonyesha unamfahamu sana,hivi siku ile ya mazishi ya Saitoti ilikuaje mbona alikua anatetemeka sana?
 
Hata wakipewa viti wasikae, waende na viti vyao, wasije wakakalia sindano za sumu, wawe na maji yao, wawekewe tape recorder kwa mbali kiasi, wasitumie vipaza sauti vya huko, kama vipi, now waanze kutembea na vipaza sauti vyao kila mahali, hadi Bungeni, wasitumie vile vya Bungeni, wawe na vya kwao binafsi wanavyoviweka just kwenye mabegi yao, kama wakiamua tu kwenda polisi, though hawana msaada wowote kiukweli kwa watu wasio wa chama tawala, chumba watakachokuwemo wahakikishe kiwe na madirisha makubwa ya kutosha, wasije wakajitoa mhanga kufa nao kwa kutumia gesi ya sumu, wawe na bodyguards wa kutosha kwenye misongamano kiasi na mikubwa ya watu, hata wanapokuwa njiani, bodyguards wanaowaamini kwa kiasi kikubwa, wasije wakachomwa sindano za sumu, kwenye misongamano ya watu wengi, hao washenzi, wanaweza kufanya uhalifu wao maeneo kama hayo, hata kama wataenda kwa hao polisi, pia wawe makini sana, bodyguards wa kutosha kupambana na lolote wakati nje Wananchi watazunguka hiyo ofisi ya polisi kinoma, ukitokea ujinga polisi watajuuuta!
Nawasihi sana Dk Slaa, Mnyika na Lema mkienda kuhojiwa msikubali kutumia vipaza na vinasa sauti vya Nchimbi au Maji ya kunywa mtakayopewa. Wanamtindo wa kuweka hewa ya sumu kwenye vipaza sauti kama walivyomfanya Horace Kolimba.

TUMBIRI (PhD, University of HULL - United Kingdom),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Unatakiwa uwe serious, sio unacheka, viongozi wa Bongo mko sawasawa kweli?!, vitu kuhusiana na usalama wa raia, unacheka, cheka ukitekenyana na Mkeo nyumbani, haoni hata aibu mtu mzima kama yeye, labda alitaka watu wamshushie kichapo pale au some few bullets zakumchangamsha kwanza, unapoongea vitu , tuhuma kuhusu watu wako usijichekeshechekeshe kama uiko na kimada wako, kuwa serious, serious, usiwatie watu hasira zaidi, wakati ya Chacha Wangwe waliyaona, juzi Ulimboka, hivi alimwona yule aliyekuwa anatangaza matokeo Kenya kipindi kile ilipokuja kutokea vurugu kubwa alivyokimbia mule kwenye mkutano, alinusurika kusalauliwa, yaani angepigwa mpaka angepagawa, msicheze na Wananchi, kuna siku mtashangaa!
Ulitaka aongee huku analia na wakatia ana address majungu ya watu wazima.....hahahaha na unaposema kuwa polisi wanatenda mabaya je na mazuri ya polisi hakuna?
 
Chakufurahisha ni kwamba "mission" ya wauaji ime "backfire". sasa wanajiosha nyang'au wakubwa. Message send!

Mkuu hii inanikumbusha teja mmoja alikuwa na tabia ya kupitia viatu nje ya mlango wangu, sasa kuna siku ile natoka nje nakutana nae uso kwa uso ananyemelea viatu na kwa kuwa hakuna njia ya kupita akajifanya amepotea nyumba na kumuulizia mtu ambaye wala simfahamu. Nilipombana sana akakiri kuwa ni yeye ambaye huwa anachukua viatu mlangoni ila ni kwa ajili ya njaa na kuniahidi kuwa atahakikisha hakuna kibaka mwingine anachukua viatu pale. Tokea siku hiyo tukawa marafiki nikimkuta njia nampatia buku au jero na hakuna tena wizi uliofanyika.

Kawaida Mhalifu ukiishamjua huishia kujibalaguza kwani hujua kuwa chochote kikifanyika utamfuata yeye. Huu mpango haramu umebumbuluka na mahojiano hayo yatalenga si kuwahakikishia ulinzi bali kummbaini aliwapatia habari hizi za Operation haramu. Kinachonisikitisha ni wataalam wa usalama kukubali kutumiwa katika mbinu ambazo ni unprofessional na wanasiasa waroho wa madaraka.

Serikali hii imekosa legitimacy na haiaminiki tena na wananchi. Leo hii watu wanaiamini CDM zaidi ya serikali ambayo imekuwa ikitunga uwongo wa kitoto kufunika mambo. Watu hawajali credibility ya taasisi bali wapo kimasilahi zaidi.
 
Akiongea leo na tbc1 waziri wa mambo ya ndani dr.Nchimbi amesema;
Shutuma walizo zitoa viongozi wa chadema kuhusu kutishiwa kuuwawa ni nzito sana. Amesema japo chadema hawajawapa tarifa serikalini, lakini yeye kwa niaba ya serikali hilo swala litafanyiwa kazi kwani ni wajibu wa serikali kulinda wananchi wake. Na tayari ameshaagiza wote walio toa shutuma hizo wahojiwe.
Usikose kuangalia kipindi cha mahojiano kati ya dr.Nchimbi na Tbc1 ifikapo saa tano kamili usiku huu.
Ni hayo tu.

Kwani Mwenzie na Ocampo yule atakuwepo??:flame:
 
Akiongea leo na tbc1 waziri wa mambo ya ndani dr.Nchimbi amesema;
Shutuma walizo zitoa viongozi wa chadema kuhusu kutishiwa kuuwawa ni nzito sana. Amesema japo chadema hawajawapa tarifa serikalini, lakini yeye kwa niaba ya serikali hilo swala litafanyiwa kazi kwani ni wajibu wa serikali kulinda wananchi wake. Na tayari ameshaagiza wote walio toa shutuma hizo wahojiwe.
Usikose kuangalia kipindi cha mahojiano kati ya dr.Nchimbi na Tbc1 ifikapo saa tano kamili usiku huu.
Ni hayo tu.

Mwanzoni aliongea vizuri aliposema ni jukumu la serikali kutoa ulinzi kwa raia wote wa Tanzania. Kumbe hii ilikuwa geresha tu, somewhere in the middle akaanza kuonesha bias yake - kwamba wanajitafutia umaarufu kwa kujenga hofu kwa wananchi. Yaani, ameshajua kuwa hawatishiwi kuuawa. Sasa huko kuhojiwa anakosema kunatokana na nini?
 
Ni aina nyingine ya usanii, mbona Dr. Mwakyembe alito ushahidi hawakumhoji licha ya kwamba ilukuwa na ukweli kwa 90%????

Nalo hilo watataka kujisafisha!!!!

Ahsante sana Mkuu. Sitta naye aliwahi kutamka hadharani kwamba anapata simu toka kwa watu ambao hawafahamu wakitishia uhai wake. Mbona magamba kwa kupitia wizara ya ndani hawakumhoji!? Viongozi wa CHADEMA wasikubali kabisa kuhojiwa na hili genge la wauaji.

Hali ni tete, Spika Sitta aomba ulinzi

By Mwandishi wetu

31st July 2009

Amuomba Waziri Mkuu rasmi

Asema alionao sasa hautoshi
Kisa, vita ya wabaya wake

Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ameomba serikali kumuongezea ulinzi kutokana na vita kali inayoendeshwa na wabaya wake. Akizungumza baada ya kutoa uamuzi wa suala la Mbunge wa Mcheweni (CUF), Shoka Khamis Juma, alisema anahitaji ulinzi zaidi kutokana na kundi la maadui wake kujipanga na kutunga kashfa dhidi yake na kuziweka kwenye mtandao halafu huchukuliwa na magazeti ambayo alidai limeyanunua na kuzifanya habari.

"Wanatunga, wakishatunga wanaweka kwenye internet halafu magazeti yao yanaichukua hiyo kuwa ni habari. Ni mambo ya ajabu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, mimi naomba ulinzi zaidi. Hii vita ni kubwa sana sasa. Ulinzi mnaonipa ni dhahiri hautoshi," alisema Sitta na kuongeza:

"Kama watu wanaweza wakafikia kufanya uhuni namna hii ndani ya nchi na kutumia fedha nyingi sana wala sisemi zile fedha wanazopeleka jimboni. Nazo zile wanasaidia kupunguza umaskini Urambo wala hawatashinda."

Sitta alisema maadui zake wamechagua magazeti manne, ambayo alitaja mawili (si Nipashe) na kwamba, wanaotunga kashfa hizo sio watumishi wa Bunge bali kundi ambalo limekaa Dar es Salaam.
Alisema maadui zake wamekuwa wakitumia fedha nyingi zingine zikipelekwa kwenye jimbo lake kuhakikisha anashindwa ubunge, lakini alilikatisha tamaa kundi hilo kwamba wananchi wanajua anachofanya na atashinda.

"Wananchi wa Urambo wanaelewa ninachokifanya kwa hiyo waendelee kupokea hiyo neema inayotujia ya mapikipiki na nini. Lakini tutashinda uchaguzi na Mungu akiniweka hai nitaendelea kuwa Spika katika kipindi kijacho cha miaka mitano," alisema Sitta.

Sitta alitoa mfano wa baadhi ya magazeti ya jana ambayo yameripoti kuwa anakula njama za kuchoma ofisi za Bunge ili kuficha ushahidi wa matumizi yake na kwamba, alisema habari hizoi ni upuuzi.

"Leo gazeti moja ambalo linatumiwa na watu ambao hawanipendi kabisa eti linasema Spika ameingia njama za kuchoma Ofisi za Bunge ili afiche ushahidi wa matumizi yake," alisema Sitta na kuongeza:

"Kama kweli ningehitaji kuficha ushahidi wa matumizi, nani ataninyima file la Bunge hapa? Si naliondoa file tu. Eti niingie njama nikae na watu hebu nifikirieni mtu mzima kama mimi nikae nafanya mkutano wa njama."

Kuhusu uamuzi wake dhidi ya Shoka, Sitta alimtaka mbunge huyo kufuta kauli aliyotoa bungeni Juni 12, mwaka huu kwamba mwitikio mdogo wa kupiga kura kwenye chaguzi ndogo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinanunua shahada za wapiga kura.

Sitta alisema Shoka aliwasilisha magazeti kama vielelezo vya ushahidi wake wa kauli aliyotoa bungeni.

Alisema mbunge huyo hakuthibitisha madai hayo kwa kiwango kinachohitajika na Kanuni ya 63 (6) na kwamba, licha ya magazeti kukubalika kuwa chanzo rasmi cha habari ambazo mbunge anaweza kuzungumzia bungeni, uamuzi wa Spika hauwezi kufanyika kwa kutegemea magazeti peke yake.
"Waheshimiwa wabunge, uamuzi wa Spika.

Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa madai ya Mheshimiwa Shoka, bado ni tuhuma (allegations) tu, kama yalivyo malalamiko mengine yanayowasilishwa na vyama vya siasa juu ya ukiukaji taratibu za uchaguzi na ambayo bado hayajawahi kuthibitishwa na mahakama," alisema.

Hii ni mara ya kwanza kwa Sitta kutangaza hadharani kwamba maisha yake yako hatarini na kuomba ulinzi wa ziara kwa Waziri Mkuu. Hatua hiyo inathibitisha ongezeko la mchezo mchafu dhidi ya kundi linalopigana na ufisadi, huku mafisadi wakitaka wapambanaji wote kusalimu amri.




SOURCE: NIPASHE



 
Serikali makini ina wajibu wa kulinda watu wake....toeni taarifa mkihojiwa ili kulinda usalama wenu na ingekuwa ajabu sana kama serikali ingepuuza hilo

Hivi serikali ni nini? Wiki iliyopita nilipita baa fulani inaitwa Makuti (iko barabara ya lami inakata kulia (branches to the right) mara tu baada ya Makaburi ya Kanisa Katoliki Chang'ombe kati ya mataa ya Chang'ombe na kabla hujafika Jengo la Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke/kabla ya kufika Uwanja wa Taifa, Mandela Road). Niliona nipoze koo kwanza.

Nilikaa kwenye meza peke yangu na kisha walikuja watu wawili na walitaka kukaa meza ya jirani ambapo kulikuwa na jamaa wawili. Kisha hao jamaa (waliokuwa wamekaa) wakamwambia jamaa aliyetaka kukaa kwenye kiti kimojawapo kuwa kuna mtu ametoka kidogo atarudi.

Hivyo, wakaja kukaa kwenye meza nilipokuwa nimekaa. Basi yule bwana akaanza kuwatukana wale wawili waliokuwa wamekaa na wao wakawa wanashangaa kulikoni. Mmoja wao akauliza huku akiniangalia, "eti ndugu yangu tumekosa nini, kusema kuna mtu atakuja kukaa hapa au?"

Huyu jamaa akazidi kuwatukana akidai kama hawamjui anaweza "kuwamaliza sasa hivi." Kisha akawauliza: "mnataka nikachukue cha moto kwenye gari?" Mwenzake akawa anampoza "poti achana nao". Alitaka kunisemesha mimi nikaa kimya sikumjibu. Maana sikutaka anigeukie hata mimi. Kisha mke wake, ambaye alikuwa akisubiri kwenye gari akamwita na yeye akamfuata.

Mimi nikamwuliza yule mwingine aliyebaki kwenye meza nilipokuwa nimekaa. Kwa nini "poti wako ana'behave hivyo'?" Yule bwana akasema: "Huyu bwana ni traffic police. Si unaona bado amevaa suruali nyeupe? Ni inspector yuko pale Central. Alikuwa kikosi cha Defender na akaua na kisha akatolewa huko. Ni hatari sana. Kama angekuwa na silaha hapa angewalipua hao aliobishana nao."

Aliposema hivi niliogopa kwa kudhani alienda kuchukua silaha. Yule poti wake aliniambia "anapiga sana judo". Niliogopa sana na hasa kusikia mlinzi wa raia na mali zao anakuwa pia threat kwa maisha yao for no good reason. Ukiona dalili kama hizi ujue tumekwisha!
 
Nchimbi hana moral right ya kuchunguza,kuhoji wala kusemea maswala ya haya.. otherwise anapaswa kuelezea vifo vilivyotokea kama cha
  1. Salome Mbatia
  2. Ipyana Malecela
  3. Amina Chifupa
  4. Ulimboka etc
ndipo aje awahoji viongozi wa Chadema. Afteral hiyo ni trick ya kujua sources za information za Chama and i hope wamemshtukia tayari
 
Mkuu hii inanikumbusha teja mmoja alikuwa na tabia ya kupitia viatu nje ya mlango wangu, sasa kuna siku ile natoka nje nakutana nae uso kwa uso ananyemelea viatu na kwa kuwa hakuna njia ya kupita akajifanya amepotea nyumba na kumuulizia mtu ambaye wala simfahamu. Nilipombana sana akakiri kuwa ni yeye ambaye huwa anachukua viatu mlangoni ila ni kwa ajili ya njaa na kuniahidi kuwa atahakikisha hakuna kibaka mwingine anachukua viatu pale. Tokea siku hiyo tukawa marafiki nikimkuta njia nampatia buku au jero na hakuna tena wizi uliofanyika.

Kawaida Mhalifu ukiishamjua huishia kujibalaguza kwani hujua kuwa chochote kikifanyika utamfuata yeye. Huu mpango haramu umebumbuluka na mahojiano hayo yatalenga si kuwahakikishia ulinzi bali kummbaini aliwapatia habari hizi za Operation haramu. Kinachonisikitisha ni wataalam wa usalama kukubali kutumiwa katika mbinu ambazo ni unprofessional na wanasiasa waroho wa madaraka.

Serikali hii imekosa legitimacy na haiaminiki tena na wananchi. Leo hii watu wanaiamini CDM zaidi ya serikali ambayo imekuwa ikitunga uwongo wa kitoto kufunika mambo. Watu hawajali credibility ya taasisi bali wapo kimasilahi zaidi.

Chadema kwa stori za kujiliwaza hawajambo.
 
Back
Top Bottom