Nchimbi: Viongozi wa CHADEMA watahojiwa juu ya kutishiwa kwao kuuwawa.

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Akiongea leo na TBC1 waziri wa mambo ya ndani Dr. Nchimbi amesema;
Shutuma walizo zitoa viongozi wa chadema kuhusu kutishiwa kuuwawa ni nzito sana. Amesema japo chadema hawajawapa tarifa serikalini, lakini yeye kwa niaba ya serikali hilo swala litafanyiwa kazi kwani ni wajibu wa serikali kulinda wananchi wake. Na tayari ameshaagiza wote walio toa shutuma hizo wahojiwe.

Usikose kuangalia kipindi cha mahojiano kati ya dr.Nchimbi na Tbc1 ifikapo saa tano kamili usiku huu.
Ni hayo tu.
 
Serikali makini ina wajibu wa kulinda watu wake....toeni taarifa mkihojiwa ili kulinda usalama wenu na ingekuwa ajabu sana kama serikali ingepuuza hilo
 
Ni aina nyingine ya usanii, mbona Dr. Mwakyembe alito ushahidi hawakumhoji licha ya kwamba ilukuwa na ukweli kwa 90%????

Nalo hilo watataka kujisafisha!!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nawasihi sana Dk Slaa, Mnyika na Lema mkienda kuhojiwa msikubali kutumia vipaza na vinasa sauti vya Nchimbi au Maji ya kunywa mtakayopewa. Wanamtindo wa kuweka hewa ya sumu kwenye vipaza sauti kama walivyomfanya Horace Kolimba.

TUMBIRI (PhD, University of HULL - United Kingdom),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Sina imani, kwani taarifa nyingi zimetolewa lakini hakuna hatua zilizochukuliwa zaidi ya kuzima tuhuma hizo. Na hasa wanapotuhumiwa polisi na TISS.
 
Ngoja niangalie! Hivi hili likipindi la saa 5 kwa faida ya nani? Tuvuje jasho kutwa halafu mijitu itucheleweshe kulala. Kuna picha za 18+ ??
 
Mbona mzee Six kasema saana, Mwakyembe nae mpaka alitoa data na majina mtawahoji lini ? nyambaf...
 
wasipuuzie, chadema kumesheen wasomi! naamini awawez kukupuka kama weng wazaniavyo!...haya mambo yapo!
 
Dr Mwakyembe aliojiwa lini mbona sijasikia au ndo hizo double standard za serikali dhaifu
 
Kwa hili la nchimbi na serikali nasema hivi, " Ni rahisi jua kuchomoza upande wa magharibi na kuzama upande wa mashariki kuliko Serikali ya magamba kulitendea kazi suala hili kwa ukweli na uwazi". Hiyo ni danganya toto ya serikali. Watakuja na matokeo yanayosema: "Tumebaini kwamba ni uzushi tu na hakuna ukweli wowote". Hili ndilo litakalokuwa jibu la uchunguzi wao. Hivi inawezekana hata siku moja shetani akafanya jitihada za kutafuta tiba ya dhambi ili kuhakikisha inatokomezwa ulimwenguni? Kama kweli shetani anaweza kufanya hivyo basi hata CCM wanaweza kushughulikia matatizo na shida za wapinzani kwa moyo.
 
Nawasihi sana Dk Slaa, Mnyika na Lema mkienda kuhojiwa msikubali kutumia vipaza na vinasa sauti vya Nchimbi au Maji ya kunywa mtakayopewa. Wanamtindo wa kuweka hewa ya sumu kwenye vipaza sauti kama walivyomfanya Horace Kolimba.

TUMBIRI (PhD, University of HULL - United Kingdom),

tumbiri@jamiiforums.com


Kweli tumbiri
 
POLICE wamekosa uhalali kama chombo cha kuhakiksha usalama wa raia na mali zake kwani mwahusishwa na vifo vingi vya raia wasiokuwa na hatia, Wameshindwa kumhoji CHENGE kwenye wizi wa fedha za RADAR, Walikana kushuhudia wizi wa kura mpendazoe, wameshindwa kuzuia madawa ya kulevya n.k... POLICE ni sehemu ya GREEN GUARD yenye maslahi mapana kwa chama cha Ma-CRIMINALS CCM...
 
Nimesikiliza na kuona Taarifa ya waziri wa mambo ya ndani ya Nchi (Ndg.Emmanuel Nchimbi) jii ya Tuhuma za Serikali kuwa na mbinu za kuwaangamiza viongozi wa CHADEMA. Kabla hata hajafanya Uchunguzi anakazana kurudia maneno mara mbili tatu kudai kuwa Viongozi wa CHADEMA ni wazushi na Wanatafuta Umaarufu!... So sad!.. Hivi kama hajafanya uchunguzi,hajawahoji walioongea anapata wapi ujasiri wa kudai kuwa ati WANATAFUTA UMAARUFU?.. Hii ni aibu,ujinga na udhaifu wa hali ya juu!..
 
Back
Top Bottom