Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Cha kuchekesha hapa ni kwamba hakuna anayesema serikali moja ndio suluhisho. Watu wamerogwa nini? Kama Zanzibar ni nchi na ina gharama zake, kwa nini Tanganyika isiwe nchi.

Tanganyika kukosa serikali, haina uhuru na ndio maana rasilimali zake zinaporwa hovyo, mfano madini asilimia 3%.

Mawaziri wa Tanganyika ni mawaziri wa jamhuri ya muungano?

Mambo yasiyo ya Muungano ya Tanganyika, yanawahusu nini wabunge wa Zanzibari?

Napata taabu sana kuelewa msimamo wa ajabu usio na ligic. Kwani ni sisi tu ndio tuna muungano duniani, Whta about USA, UK nakadhalika. Tusiwe dependent mind, eti kwa sababu fulani, kwa sifa zake binafi akauza uhuru wa Tanganyika

Mjadala wa katiba bila swala la Tanganyika ni Mzaha tu.:noidea:
 
Ujio wa tanganyika hauepukiki, tujiandae kusherehekea uhuru wa Tanganyika kutoka mikononi mwa CCM.

Twaweza kukubali kuungana na kuwa nchi moja tu, la sivyo nchi mbili serikali tatu?
Piga ua naelewa nchi moja haiwezekani mu aana wazenji hawatapenda iwe hivyo.

Then kwa kuwa wanaopendelea muungano watakomaa, serikali tatu haipukiki.
Hapo ndipo ninapoiona Tanganyika yangu ikipata uhuru kutoka midomoni mwa Mabeberu.
 
Mtikila ana idea nzuri tatizo lake hawezi kukaa na wenzake,aelewe kwamba tusipochukuliana madhaifu yetu hatutafika pale tunataka:a s 39::a s 39::a s 39::a s 39::a s 39::a s 39:
 
Tungepata kundi kubwa la watanganyika wenye msimamo kama wako, wa Rev. Mtikila, wa G-55 na mimi na madai ya wazanzibari ya kupotea kwa mbia mwenza wa muungano basi kazi ingekuwa rahisi kuufahamisha umma wa Tanganyika.

Lakini kila nikifuatilia mijadala humu JF linalohusu kuirejesha Tanganyika ndani ya Muungano basi...list ya "influencial contibutors" kuanzia Mwanakijiji, Nguruvi3, JokaKuu, mkandara ,Miss judith wanasema hawataki hata kuisikia Tanganyika ikitajwa...Kasumba ya Mwalimu ya Tanzania ni nchi moja imewaingia vizuri na wanasahau kuwa Tanganyika na zanzibar zimeunganisha baadhi ya mambo tu. na kila sehemu kubakisha mambo mengi ya kila upande kuyashughulikia yenyewe...sasa vipi utabakisha mambo ya Tanganyika bila ya serikali na taasisi zake?

Wengine wanasema itakuwa ni kuitiA GHARAMA Tanganyika aka Tanzania bara.. hivi kuna kitu ambacho hakina gharama? Hasa kama kina manufaa? Na kama hakina manufaa/faida kwa nini tuwe nacho?, tuendelee kuking'ang'ania? Na hata kuzuia kisijadiliwe au kukosolewa?

Unajua, mimi hujiuliza kama Muungano wetu tungeu-model katika mfumo kama wa EAC basi hizi nchi nyengine zingekuja kujiunga nasi badala ya kuanzisha EAC mpya na kweli Muungano wetu ungekuwa wa kupigiwa mfano duniani. Lakini miaka 47 imepita sasa na hakuna nchi nyengine iliyotamani kuyeyuka ndani ya Muungano kama ambavyo Tanganyika imeyeyuka na kwa Sasa juhudi tunazofanya kuiyeyusha Zanzibar kwa kuelekea serikali moja.

Kuna watu wanapenda kusema Muungano wetu is unique...mimi sioni hii uniqueness isipokuwa naona utapeli tu na mazingaombwe au changa la macho. sijui itatuchukua tena miaka 47 kujua kuwa tunakawilisha na kujiongezea matatizo badala ya kuwa na ujasiri na kukabiliana na uhalisia wa siasa za kimuungano wa nchi huru!!???


Hivi kwa mfumo huu, Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya, Congo NK wataingia katika muungano. Tuafikiria nini, kama sio kudanganyana tu. Hapa naona kuna ajenda ya siri.:tape:
 
Ukichunguza kwa makini kile kinachoitwa JMTZ utaona tu ndiyo serikali ya tanganyika.Jaribu tu kufikiri kama rais wa jamhuri akitaka ikulu yake iwe zanzibar kama wazanzibar hawataona kuwa wamevamiwa au wamekuwa na marais wawili.Kimsingi rais wa jamhuri akienda zanzibar anachukuliwa kama mgeni hivyo mambo yote yanayofanywa na serikali ya muungano wazazibari wanayaona ni ya tanganyika.
Bahati mbaya mtanganyika haruhusiwi kuwa rais wa zanzibar ila mzanzibar anaruhusiwa kuwa rais wa tanganyika(JAMHURI YA MUUNGANO).
Wao wanaleta wawakilishi wao dodoma lakini sisi hatupeleki wetu kwenye baraza la wawakilishi.
Muungano wetu ni fumbo ni bora ama tuunde shirikisho au wazanzibari wajikane tuanzishe nchi moja na serikali moja tu.
 
Nimelisema hili miaka mingi. Nimerudia rudia mara nyingi hata katika forum hii. Nimelichangia star tv kwenye vile vipindi vya mjadala!
Bila Tanganyika tunazungumzia katiba ipi? Kama hakuna Tanganyika katiba tunayofikiri kuunda ni batili. Lazima kuwe na Tanganyika na Zanzibar kisha tuzungumzie katiba na tuzungumzie muungano. Asante kwa kuliona hili pia muanzisha thread. Tanganyika ni ya lazimaaaaaaaaaa.
 
Usidharau watu simply kwa kuwa wana mtizamo tofauti na wa kwako! Washabiki wa u-Tanganyika bahati mbaya sana haelezi faida zitakazopatikana mara baada ya kuanzisha Serikali tatu! Je, ufisadi utatoweka? Je, umaskini utaondoka? Je, vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 5 vitapungua? Kama hakuna majibu, basi sioni haja ya hiyo Serikali ya Tanganika ambayo nahisi itaongeza matatizo badala ya kupunguza!
Kwa bahati mbaya una uvivu wa kusoma na hata hapa Jf tumeeleza sana sababu ya utanganyika, lakini kama alivyosema mchangiaji mmoja kwamba sijui mna uji vichwani? pitia michango yote hapa jf soma na utajua kwamba watetezi wa utanganyika wanazo sababu, acha kutandia treni kwa mbele bana!
 
Sijui ni mimi tu nina kichwa cha panzi?! Maana sielewi kabisa... Kwa nini hata hapa hajitokezi mtu aje na faida za wazi kabisa?! Kwamba muungano kwa Tanganyika una faida 1,2,3,4, nk,nk. Siku zote tunaambiwa ni mzuri tuuenzi, faida za huu muungano kwa watanganyika hazisemwi! Ni siri ya nani hii? Kwa uelewa wangu mdogo kwa mambo haya, nadhani ingekuwa faida kwa wananchi kama tungeenzi Azimio la Arusha kuliko huu muungano wa ajabu.. Msinipige mawe tafadhali!!!
 
Naunga mkono hoja.

Hata kwa mahitaji ya kisheria, kama mshirika wa Z'bar ni mfu (Tanganyika) sasa huyo Z'bar mwenza wake ni nani muda huu? Ni sheria gani duniani inayoendeleza mahusiano ya aliye hai na mfu? Ikiwa Mke na Mume tu kifo huwatenga sembuse nchi!

In my terms it's a political Masturbation.
 
Nonda,'
Umesahau kunijumuisha na mimi katika hilo kundi. Tanganyika tayari imo ndani ya Tanzania sasa mnataka Tanganyika tofauti ya nini? Rais wa Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania ni rais wa Tanganyika vile vile, sasa mnataka muwe na marais wawili? Hivi mkishapata rais wa Tanganyika, huyu rais wa Jamhuri ya Mwungano atakuwa na kazi gani? Atakuwa ceremonial tu kama rais wa Israel? Tanganyika imo ndani ya Tanzania, na mara nyingi nikisafiri kutoka Dar kwenda makwetu najisikia nimo ndani ya Tanganyika.
Kwa maana hiyo Wazanzibar wapo sahihi wanaposema wanatawaliwa na Tanganyika?.
 
Ni kitu cha ajabu sana kuwa na nchi moja yenye mambo yanayofanana na mithili ya kinyonga.

Mawaziri wa Tanganyika wanaitwa mawaziri wa jamhuri ya muungano, tunawaudhi wazanzibari

Mambo ya Tanganyika (yaani yasio ya muungano) yanapelekwa kwenye bunge la Tanzania, na wabunge wa zanzibar hawatoki nje wakati wa maamuzi.

Baraza la mawaziri linapozungumzia mambo ya Tanganyika, sijui kama mawaziri wasiohusika wanatoka nje.
Jimbo moja zanzibari lina wabunge wawili, Tanganyika mmoja.

Hii ni mifano tu ambayo inalilia Serikali ya Tanganyika, na bunge lake:help:

Ukiniambia nizungunzie mabadiliko ya katiba bila kuzungumzia muungano unanidanganya.

hapo Vipi wana JF:noidea:

Huu ndio wakati wake hasa wakuifufua Tanganyika yetu waliyo ipa sumu lakini haijafa!HAKUNA TANGANYIKA HAI BILA KATIBA REKEBISHI
 
Hii ichi inaongozwa na watu wenye akili za kuku ni shida sana kuwaeleza haya wakakuelewa. Mazoea yamewalevya!

Unamaana wa wa zidumu fikra za fulani. Lakini mimi ninauhakika kama muungana hautaangaliwa vizuri wakati wa kurekebisha katiba basi utaja vunjika tu. :frusty: Kwa sasa kinachoendelea ni mchezo wa kuigiza. Either Tanganyika au serikali moja:amen:
 
Ndugu, nichukue nafasi hi adhimu kuchukua maoni yenu juu ya muungano wetu. Hoja ya kujadili hapa inaitaji tutoe maelezo ya Tanganyika tuitakayo endapo Muungano umevunjika! Swali jingine linakutaka uchangie umuhim wakuwa na Tanganyika!
 
Ndugu, nichukue nafasi hi adhimu kuchukua maoni yenu juu ya muungano wetu. Hoja ya kujadili hapa inaitaji tutoe maelezo ya Tanganyika tuitakayo endapo Muungano umevunjika! Swali jingine linakutaka uchangie umuhim wakuwa na Tanganyika!

Je, unazungumzia Tanganyika ipi, ya Mjerumani iliyojumuisha Rwana na Burundi au ya Mwingereza ambayo haikujumuisha nchi hizo! Ukitaka turudi nyuma turudi pale ambapo wakoloni walikuta tupo, yaani tawala za kichifu na kitemi, right?
 
Nazungumzia tanganyika iliyotupa uhuru na hifadhi kwetu km raia, ile ambayo ilichanganywa na zanzibar tukapata tanzania!
 
Jamani twaitaji maoni yenu juu ya tanganyika yetu. Je iko wap sehemu ya tanganyika ktk muungano wa tanzania?
 
Je, unazungumzia Tanganyika ipi, ya Mjerumani iliyojumuisha Rwana na Burundi au ya Mwingereza ambayo haikujumuisha nchi hizo! Ukitaka turudi nyuma turudi pale ambapo wakoloni walikuta tupo, yaani tawala za kichifu na kitemi, right?
Kwani wewe ulitokea tanganyika ipi ? Ya pemba unguja,au tanga au mombasa kenya ? Inamana hujui mipaka ya tanganyika#? WACHA KUJITOA FAHAMU ZA AKILI. Tanganyika ipo na mipaka yake,burundi pia ina mipaka yake,na uganda wacha ujinga .
 
Jamani twaitaji maoni yenu juu ya tanganyika yetu. Je iko wap sehemu ya tanganyika ktk muungano wa tanzania?
Tanganyika ipo ndio hiyo hiyo muitaro tanzania bara,kwani tanzania ni ipi ? ZANZIBAR ina mipaka yake juzi tu ilishawatambulisha mipaka,sasa iliyobaki ndio tanganyika/tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom