Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Kwa asili kila jambo lina chanzo chake na uboreshaji wa chanzo waweza kuimarisha au kaharibu ubora wa kile cha mwanzo. Tanzania ni zao la uboreshaji wa Tanganyika na Zanzibari na huu ndio msingi mkuu wa muungano, na swali kuu la kujiuliza ni je uboreshaji umetoa tija kubwa kuliko Tanganyika na Zanzibar katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa?.

Nakubaliana na wachangaaji wengi walionitangulia kwa hoja zao lakini natamani kungekuwa na uchmbuzi zaidi kujua ni kwa kiasi gani muungano umechangia kuongeza kasi ya maendeleo ya Tanzania. Kuna hoja nyingi kuhusu kubinywa kwa zanzibar kujitafutia fursa za kimaendeleo ndani na nje ya mipaka Tanzania, pia yapo maneno juu Tanganyika kuubeba Muungano kiuchumi kuliko Zanzibar, mambao ambayo nahisi hayajajibiwa vyema na katiba pendekezwa.

Mungano bora ni ule unaotoa fursa za kiuchumi zaidi kwa wananchi wake, wakati katiba pendekezwa ya Tanzania naona kama inatoa fursa za Kiasa na haki za binadamu zaidi, nadhani nguvu ya kulinda muungano ni kubwa mno kuliko kujibu kero za kiuchumi na kimuundo, kwenye katiba pendekezwa upo ulegezaji wa masharti ya Zanzibar kujitafutia uchumi wake kwa majirani kwa msaada wa Tanzania, jambo hili linaonekana kama rahisi kwa sababu wanasiasa wamelizika lakini utekelezaji wake waweza kuwa kero nyingine ya muungano, na nafikiri hili limefanywa ilikunyamazisha kelele za wanzanzibari kudai uhuru wao wa kiuchumi na sidhani kama kweli hiyo ndiyo suruhu kamili.

Lakini swala la Tanganyika kimuundo limejibiwa kwa kuongezwa Makaumu wa Rais, bado nafikiri kuna haja ya kufanya mambo zaidi hasa kutiririsha muundo wa kiutawala hadi ngazi za chini ili raia wajue wakati gani wanafanya ya Tanzania na wakati gani wanafanya ya Tanganyika hili litawasaidia hata watendaji wa serikali. Na ukitazama kwa macho matatu muundo unaopendekezwa unonyesha pasipo shaka umuhimu wa serikali tatu haswa kwenye muundo wa Tanzania jambo ambalo limefunikwa ili mwanaharamu apite.

Katika Muungano huu kupo kutoaminiana sana, kiasi kwamba uoga usio muhimu umeingia kiasi kwamba wanasiasa wana tamani kuulinda Muungano hata kwa damu, hii ni hofu mbaya kwani kama hili litaendelea muungano utabaki kwenye bunduki na mabomu wakati mioyoni mwa watu huopo. Na utakuwa muungano wenye gharama sana na unaweza kudumaza maendeleo zaidi, ni dhairi kwenye muungano wowote yapo mambo ya kupoteza na yapo ya kupata, nahisi hatutaki kupoteza baadhi ya mambo kisiasa lakini tupo radhi uchumi uumie ili mradi tuu tupo poa kisiasa na tunadumisha Muungano.Nadhani si nadharia nzuri kwa maendeleo ya Tanzania. Muungano ndio siasa ya dunia kwa sasa hivyo tunahitaji kuuimarisha kwa muundo sahihi bila hofu ya kuonyesha kuvunjika kwa sababu ya muundo fulani, wanufaika wakikubaliana na muundo huo utaimarika zaidi hata ukiwa wa serikari mmoja, wanasiasa msigawane madaraka, kubalini kupoteza kwa manufaa yetu sote.
 
kujiita Mtanzania maana yake wewe ni mtanganyika+mzanzibar,Tanzania ni muungano wa nchi mbili au ndoa ya nchi mbili(ikawa mwili mmoja) ndizo zikamzaa mtanzania,wazazi wangu wote wana asili ya Tanganyika hivyo mimi ni Mtanganyika ila sina ubaguzi,kujiita mtanganyika sio ishara ya ubaguzi,mbona mtu anajiita mzigua na anaoa mbondei.Tanganyika nakuita popote ulipo urudi,nimekumisi sana Baba,ingawa walikuzika ila Mungu amekufufua,ameeenii!!

!
!
na mimi ni mtanganyika pua
 
historia, nimesoma japo si sana inaonekana hukunielewa vizuri kwa vile post imekaakaa kaa shairi fulani hivi, laki my point is:

1. Tanganyika ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wakoloni

2. Tanzania ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wazalendo

3. mimi na wingine wenye umri usiofikia miaka 47, tumezaliwa Tanzania na sio Tanganyika

4. muungano ni kielelezo cha umoja wetu na licha ya mapungufu yake, ni bora kuliko kutengana

5. changamoto tuliyonayo ni kuondoa mapungufu yake, iwe ni kwa kuunda serikali moja, tatu au kubaki na mbili za sasa, vyovyote vile, muhimu tuondoe kero zinazohusiana na muungano

kilichotufanya tusindwe kuijenga Tanzania si muungano uliopo, bali masuala mengi tu tunayojadili hapa kila siku kama ufisadi nk. kwa hiyo hata tukiuvunja muungano, tutashindwa kuijenga Tanganyika pia kama hatutapambana na matatizo haya (ufisadi nk)

Kesho ukiolewa na Makonda milele hutaitwa tena Judith bali Mrs. Makonda
 
mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui

nilizaliwa Tanzania,
nilizaliwa Afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu

kwa hiyo;

mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mdunia
mimi ni mwanadamu

maana ya Tanzania, najua
maana ya Afrika, najua
maana ya Dunia, najua
maana ya mwandamu, najua

nawauliza wazanzibari,
nini maana ya Zanzibari,
nani aliipa jina Zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
kwa nini wasijivunie utanzania?

zanzibar = zunjbar
 
Nasikia mara ohhhh, wabara wanatuonea, wabara wanatudharau. Sisi si wabara, ni watanganyika bana!

Muungwana haachi asili. Nia yangu si kuanzisha thread ya kupinga muungano, bali sipendi kuitwa mbara na ndio maana ninasema sisi sio wabara, ni watanganyika.

Ukisema Tanganyika ni jina la kikoloni, basi kataa pia majina ya Tabora, Mwanza, Dar es salaam, Tanga na mengine mengi yanayopatikana katika ramani iliyochorwa na mkoloni.
Hakika wewe ni mzalendo wa kweli sana , sasa ngoja nikutoe wasiwasi , Tanganyika IMERUDI RASMI .
 
NCHI YETU TANGANYIKA mkoa wangu tabora, kijiji changu itonjanda, tunapakana na ipuli, isukamahela, isikizya, ilolangulu, itetemya, igoko, ibelamilundu, itobela, ilolansimba nk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom