Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Nasikia mara ohhhh, wabara wanatuonea, wabara wanatudharau. Sisi si wabara, ni watanganyika bana!

Muungwana haachi asili. Nia yangu si kuanzisha thread ya kupinga muungano, bali sipendi kuitwa mbara na ndio maana ninasema sisi sio wabara, ni watanganyika.

Ukisema Tanganyika ni jina la kikoloni, basi kataa pia majina ya Tabora, Mwanza, Dar es salaam, Tanga na mengine mengi yanayopatikana katika ramani iliyochorwa na mkoloni.
 
mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui

nilizaliwa Tanzania,
nilizaliwa Afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu

kwa hiyo;

mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mdunia
mimi ni mwanadamu

maana ya Tanzania, najua
maana ya Afrika, najua
maana ya Dunia, najua
maana ya mwandamu, najua

nawauliza wazanzibari,
nini maana ya Zanzibari,
nani aliipa jina Zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
kwa nini wasijivunie utanzania?
 
Haya sasa
badala ya wote kuangalia jinsi
serikali yetu inavyoharibu nchi yetu
sisi tunagombana wenyewe kwa wenyewe
tutafika mahali kweli kwa mtindo huu

Mtanganyika ni Mtanzania
na Mzanziber ni Mtanzania
Hivyo ndo ilivyo na hivyo ndivyo ilivyokuwa..
 
we waache tu wazenz waondoke, watanganyika tutaendelea, bali soon wao watakuwa wapemba na unguja, si nyerere alitabiri?
 
naipenda Tanzania hata bila zanzibar, na watanganyika tutaendela mbele tu.
 
Hapana sisi sio watanganyika kwa kuwa Tanganyika ilikufa toka tarehe 26 aprili 64, hata kama wao ni waznz sisi ni watz tu, tuidumishe tz hata bila znz.

Tanganyika haijawahi kufa kwani hata neno TANZANIA ni kifupisho cha maneno TANganyikaZANzibar(IA). Hayo maneno ya mwisho waliyaongeza tu kufanya jina litamkwe ki-pan african zaidi. Hivyo kimsingi huwezi kuongelea Tanzania bila kuzitaja Tanganyika na Zanzibar.
 
Ni muda wakuwaacha wenzetu hawa wanzibari kujiondoa kwenye muungano .kila moja wetu anakubali umoja ni nguvu utengano ni udhaifu lakini swali la msingi kwanini wao waone wanaonewa sana? Sasa kwa mantiki hiyo basi sisi wa tanganyika tupige kura ya kuvunja muungano kwa muda hili wenzetu hawa wanaona wanaonewa wakajifikirie mbona hata ndoa huwa zina makwazo mke anarudi nyumbani kutafakari
even european union hakuna even distribution .
 
why do u people waste ur time with nonsense!?? sio lazima kuanzisha thread humu kama huna lakusema.
 
why do u people waste ur time with nonsense!?? Sio lazima kuanzisha thread humu kama huna lakusema.
mkuu nonsense kusema ukweli ,kwani uongo wanzibari hawalamiki ?wewe uko nchi gani hii ni fact na ndo maana kuna kero za muungano na zinatumbulika na sisi kama part ya muungano lazima tuargue bana
 
nyeyerere alitabiri hivyo tu ? hata bara alitabiri itakuwa wanyamwezi na wamakua na wachanga na wamasai
 
kwani muliambiwa mtarudi nyuma ? Lengo ni kuwa sawa na sio kuwaonea walio kidogo...
kama ni usawa kwenye revenue kwa kweli wasahau watapata kwa proportionality tu not otherwise hakuna haja ya kufavourana hapa so what? Usawa wa kisiasa huo wanao tena nadhani unaona wanvyotamba huku tanganyika
 
Hivi kwanini Utanganyika inaonekana kama dhambi? Hata CCM wanalikana sana hilo jina. Mimi nadhani kila nchi ina historia yake. Mimi ni Mtanganyika zaidi kuliko Mtanzania.
 
Tanganyika iko, waliojaribu kuiua hawapo so T'nyika itarudi pahala pake.
Miss Judith anasema anaijua Tz lakini haijui T'nyika. Ni kutojua historia, ajaribu kujifunza na kujisomea zaidi.
Angalia eti suala la Muugnano kwenye muswada tata wa kutunga sheria ya Katiba mpya halitakiwa kujadiliwa kabisa. Kuna ujing zaidi ya huo? Watu wanalazimisha mambo, uongo wao umekuwa bayana kama jua hawana pa kujificha tena lakini wanatumia nguvu uchwara eti suala la 'muungano' sic ni nyeti sana.

Kama WaTz watataka kuendelea na ushirikiano, nchi mbili hizi lazima zichagua mambo zitakayoshirikiana na mfumo wa kuendesha shirikisho lao. Nasema shirkisho makusudi kwa sababu ndio njia pekee sahihi kwenda mbele.
 
Ni kweli usiopingika wazanzibar wanadhulumiwa. kama Ni muungano wa kweli wa nchi mbili lazima mgawo Uwe sawa nusu kwa nusu. Hapa Nina maana Watanganyika acheni kuzubaa pazeni sauti kuutafuta uhuru wenu na hazina yenu TANGANYIKA ILIKOFICHWA NA HAWA WENYE AKILI FINYU. Huu muungano huu Ni wa kihuni tu.

Unaposema Muungano wa nchi unazungumzia nchi hizo zimeungana zenye ku- share ya uchumi wao kwa sawa. Tunazungumzia Muungano wa Mataifa mawili. Lakini uhuni uliopo Ni kuwa tuna SERKALI MBILI TU YA MUUNGANO na ya ZANZIBAR. Je ZANZIBAR imeungano na Serikali ya Muungano. Kwa nini Watanganyika wanaendelea kuficha umwall wa mambo? Kuna siri gani hapo? Mara utasikia Kuna wizara za Muungano na zisizo za Muungano. Hiilo Bunge lisilo La Muungano upande mwingine wa Muungano linakutana lini kujadiri maendeleo Yao kama Wazanzibar? Ina maana BUNGE LA MUUNGANO NDILO HILO HILO LINAJADILI MAMBO YA MUUNGANO NA BAADAYE HUBADILIKA KAMA KINYONGA HUVUA GAMBA WAKIWEMO WANZANZIBAR WANANZA KUJADILI MAMBO YASIYO YAMMUUNGANO KAMA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR.

BAJETI INAPITISHWA YA MUUNGNO HALAFU INBADILIKA AUTOMATICAL KUWA PIA YA TANGANYIKA. CCM ACHENI UNAFIKI TUMEGUNDUA NDIYO MAANA NCHI HAENDELEI KWA SABABU YA KUFANYA KAZI KWA HOFU NA UNAFIKI. JIFUNZE MUUNGANO KAMA WA NCHI ZA KIARABU, ULAYA, N.K.

Hata Nchi zilizoendelea zina Muungano lakini nchi kama nchi imebaki na haadhi yake. Wanayo mambo ya muungano yanayoeleweka lakini Pia kila nchi inafanya mambo yake bila kuingiliwa. Sio kama muungano wa Tanzania uliojaa unafiki na udikiteta. Ndiyo maana wanataka kufanya kama kitu kitakatifu kisichojadiliwa. Muungano gani unakuwa na miaka mingi Mamma hii bila Kufanyiwa Evaluation.

Umefika wakati kizazi hiki kijadili kwa undani kuona tumefaidikaje na muungano huu. Je inafaa tuendelee na mfumo huu Au hapana.
 
Tanganyika iko, waliojaribu kuiua hawapo so T'nyika itarudi pahala pake.
Miss Judith anasema anaijua Tz lakini haijui T'nyika. Ni kutojua historia, ajaribu kujifunza na kujisomea zaidi.
Angalia eti suala la Muugnano kwenye muswada tata wa kutunga sheria ya Katiba mpya halitakiwa kujadiliwa kabisa. Kuna ujing zaidi ya huo? Watu wanalazimisha mambo, uongo wao umekuwa bayana kama jua hawana pa kujificha tena lakini wanatumia nguvu uchwara eti suala la 'muungano' sic ni nyeti sana.

Kama WaTz watataka kuendelea na ushirikiano, nchi mbili hizi lazima zichagua mambo zitakayoshirikiana na mfumo wa kuendesha shirikisho lao. Nasema shirkisho makusudi kwa sababu ndio njia pekee sahihi kwenda mbele.

historia, nimesoma japo si sana inaonekana hukunielewa vizuri kwa vile post imekaakaa kaa shairi fulani hivi, laki my point is:

1. Tanganyika ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wakoloni

2. Tanzania ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wazalendo

3. mimi na wingine wenye umri usiofikia miaka 47, tumezaliwa Tanzania na sio Tanganyika

4. muungano ni kielelezo cha umoja wetu na licha ya mapungufu yake, ni bora kuliko kutengana

5. changamoto tuliyonayo ni kuondoa mapungufu yake, iwe ni kwa kuunda serikali moja, tatu au kubaki na mbili za sasa, vyovyote vile, muhimu tuondoe kero zinazohusiana na muungano

kilichotufanya tusindwe kuijenga Tanzania si muungano uliopo, bali masuala mengi tu tunayojadili hapa kila siku kama ufisadi nk. kwa hiyo hata tukiuvunja muungano, tutashindwa kuijenga Tanganyika pia kama hatutapambana na matatizo haya (ufisadi nk)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom