Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,554
- 34,481
Kumekuwepo na mjadala mkubwa sana wa kuendelea au kutokuendelea kwa Muungano baina ya Zanzibar na Tanzania bara. Lakini katikati ya mjadala huo kumezuka hoja ya kurudisha matumizi ya jina Tanganyika kama muungano utavunjika. Kwa maoni yangu nadhani hata bila ya kuuvunja Muungano baina ya nchi hizi mbili sisi ni watanganyika na wala si Watanzania Bara.
Hapo mwanzo wakati wa Muungano wa nchi hizi mbili ilifikiriwa kwamba nchi zote mbili zitakubali kuuacha (surender) utambulisho wa nchi zao na hatimaye zitambulike kwa majina ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Lakini kwa bahati mbaya Wazanzibar wakabakia na Jina lao la Zanzibar na Watanganyika wakakubali kuitwa Tanzania Bara bila ya kuwepo kwa Tanzania Visiwani.
Kosa kubwa walilolifanya Watanganyika ni kukubali kwao kujizoeza kujiita Watanzania Bara bila watu wa upande wa pili kukubali kuitwa Watanzania Visiwani. Wakati watanganyika waliamini wao ni nchi moja na Zanzibar, Wazanzibari waliamini kwamba wao na Watanganyika ni nchi mbili tofauti wenye haki zisizofanana.
Wazanzibari waliamini kwamba Watanganyika ni wakaliaji kimabavu nchi yao lakini wao Wazanzibari wana haki ya kuishi, kushika madaraka na kumiliki mali Tanganyika. Mzanzibari aliamini ana haki ya kuwa Diwani wa Buguruni lakini si ruhusa kwa Mtanganyika kuwa Sheha kwenye mitaa ya Mji Mkongwe Zanzibar.
Watanganyika walitoa haki zao kwa Tanzania lakini Wazanzibar wakachukua haki za Tanzania wakakataa kuzitoa haki zao za Zanzibar. Kwenye makubaliano ya uundaji wa Tanzania hakuna mahali kunapotajwa kwamba ili Tanzania iwepo kunamaanisha kuua Tanganyika na Zanzibar. Kinachotajwa ni kuvunjwa kwa nguvu za kidola za nchi hizi mbili na wala si majina ya nchi mbili hizi.
Mfano rahisi ni United States of America ambako nchi zilizoingia kwenye shirikisho hilo hazikubadili majina yao na kuwa labda Amerika ya Pwani, Amerika ya Nyanda za Juu bali kila nchi ilibakia na jina lake ila kilichobadilika ni kutoa baadhi ya mamlaka yake kwa Serikali Kuu ya shirikisho na dola ikawa ni moja USA. Kwa hiyo kwa maoni yangu si lazima tuuvunje Muungano ndiyo tuwe na haki ya kuitwa Tanganyika, hata sasa tunaweza kujiita Tanganyika kama tunaona inafaa.