Nchi inawaza kushinda uchaguzi tu

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,667
1,566
Ukiangalia mwenendo wa siasa wa nchi yetu kwa sasa, ni dhahiri shairi viongozi wetu wanawaza kushinda uchaguzi tu hakuna lingine. Tangu wamechaguliwa akili na mawazo yao yapo kwenye namna gani watashinda tena uchaguzi.

Hii inadhihirishwa hata namna ya maendeleo wanayotuletea. Ni yale maendeleo ya vitu vya kuonekana ili tuone kweli wanafanya kazi. Ununuzi wa ndege, ujenzi wa madarajja nk. Lakini kimsingi tuna shida na vitu zaidi ya hivyo. Tuna shida na huduma bora za afya, elimu bora, upatikanaji wa ajira nk. Leo hii kuna wimbi kubwa la wagonjwa wanaokimbiwa Muhimbili sababu ya gharama kubwa za matibabu, ukiwa na maiti Muhimbili mnaweza ghaili kuzika.

Tuache kuwaza ushinda uchaguzi kila kukicha kwa kufanya vitu vya kuwafurahisha wapiga kura, twende kwenye uhalisia wa maisha ya Watanzania na mahitaji na matazamio yao kwa serikali yao. Lakini serikali nzima ipo kwenye kampeni muda wote. Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, watendaji kata wote wanahaha kutafuta kura na mhishimiwa. Haifai namna hiyo

Nikosolewe kwa staha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili matope za CCM ni kuona upunzani unakufa. Wanajua umuhimu wa upinzani, lakini hawataki kuuelewa.
Lile li jini la zidumu fikra za mwenyekiti linawaandama mpaka leo, ndio maana wanatumia mabilioni mengi kwenye mwenge usio na tija badala ya kuyatumia hayo mabilioni kuboresha miundombinu na hali za uchumi wa mwananchi
 
Na siku hizi mkutano au mkusanyiko wa jambo lolote ni nafasi ya kampeni ya ushindi kwa uchaguzi
ujao
 
Yani ni zaidi ya hovyo. Wakuu wa mikoa na MaDc wamekuwa wapiga kampeni. Hata jambo lililofanywa kwa nguvu za wananchi lakini jina la mhishimiwa lazima litatajwa kwa mbwembwe zote na shukrani atapewa yeye utazani kafanya yeye
Na siku hizi mkutano au mkusanyiko wa jambo lolote ni nafasi ya kampeni ya ushindi kwa uchaguzi
ujao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti vijana wajiajiri. Hivi huko shuleni wanafundishwa kujiajiri! Kuna wahitimu wengi sasa hawajui wafanye nni.
Ni lazima mipango yetu iwezeshe vijana kujiajiri.
Kilimo mdio lakini unaingia tu bila kuandaliwa? Biashara ndio lakini mitaji inakufa wamama wanafilisiwa. Mambo hayaji kwa matamko pekee. Kuna mahali tunakosea!
Akili matope za CCM ni kuona upunzani unakufa. Wanajua umuhimu wa upinzani, lakini hawataki kuuelewa.
Lile li jini la zidumu fikra za mwenyekiti linawaandama mpaka leo, ndio maana wanatumia mabilioni mengi kwenye mwenge usio na tija badala ya kuyatumia hayo mabilioni kuboresha miundombinu na hali za uchumi wa mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAWA,
Nasikia wanapanga kumuita Membe kwenye kamati ya maadili hivi kosa lake ni lipi kweli? Tuanzie hapo
 
Inatia Aibu kweli

Vyama vya upinzani vinawaza kushinda Uchaguzi tu badala ya kuwatumikia Watanzania

Hizo siasa za kusaka kura ni za Magufuli, kibaya zaidi hawezi kushindana bali kulazimisha yeye kuwa mshindi bila hata ridhaa ya wengi. Kwa maneno marahisi ni mtu anayeamini kushinda bila kupingwa, na sasa hizo kazileta kwenye nchi nzima.
 
Nitafurai siku mmoja ukiandika jambo lenye akili na manufaa kwa Taifa kuliko ujinga na utoto unao andika kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka jamaa anaishi kwa shemeji yake
Kula, kula yote hapo.....
Hadi miguno ya dd yke na shemeji usiku anaipigia chabo..... Mpk hpo unafikiri kichwani Atakuwa mzima

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom