TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,667
- 1,566
Ukiangalia mwenendo wa siasa wa nchi yetu kwa sasa, ni dhahiri shairi viongozi wetu wanawaza kushinda uchaguzi tu hakuna lingine. Tangu wamechaguliwa akili na mawazo yao yapo kwenye namna gani watashinda tena uchaguzi.
Hii inadhihirishwa hata namna ya maendeleo wanayotuletea. Ni yale maendeleo ya vitu vya kuonekana ili tuone kweli wanafanya kazi. Ununuzi wa ndege, ujenzi wa madarajja nk. Lakini kimsingi tuna shida na vitu zaidi ya hivyo. Tuna shida na huduma bora za afya, elimu bora, upatikanaji wa ajira nk. Leo hii kuna wimbi kubwa la wagonjwa wanaokimbiwa Muhimbili sababu ya gharama kubwa za matibabu, ukiwa na maiti Muhimbili mnaweza ghaili kuzika.
Tuache kuwaza ushinda uchaguzi kila kukicha kwa kufanya vitu vya kuwafurahisha wapiga kura, twende kwenye uhalisia wa maisha ya Watanzania na mahitaji na matazamio yao kwa serikali yao. Lakini serikali nzima ipo kwenye kampeni muda wote. Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, watendaji kata wote wanahaha kutafuta kura na mhishimiwa. Haifai namna hiyo
Nikosolewe kwa staha.
Sent using Jamii Forums mobile app